JonBenet Ramsey: Mauaji yake yalikuwa ni ya ajabu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JonBenet Ramsey: Mauaji yake yalikuwa ni ya ajabu!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jun 15, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jun 15, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  tumblr_kv644rishd1qaqwsn.jpg
  jonbenet_ramsey (1).jpg
  1283062307JonbenetRamsey3.jpg
  Mtoto JonBenet Ramsey
  Ramsey1.jpg
  John na Patsy Ramsey
  patsyramsey_wideweb__470x452,2.jpg
  Patsy Ramsey
  normal_6.jpg
  JonBenet, Melinda, Burke na John Andrew Ramsey
  John_Ramsey_looks_on_as_his_wife_Patsy_holds_a_flier_promising_a_100000_reward.jpg
  John na Patsy Ramsey wakitangaza zawadi
  jonbenet_ramsey.jpg
  John Mark Karr mtu aliyejipachika tuhuma za mauaji ya mtoto JonBenet Ramsey


  Mnamo Desemba 26, 1996 mwili wa mtoto JonBenet Patricia Ramsey aliyekuwa na umri wa miaka sita wakati huo ulikutwa ghorofa ya chini (Basement) ya nyumba yao, ikiwa ni karibu saa nane tangu aliporipotiwa kutekwa nyara na watu wasiojulikana. Tukio hilo liliibua hisia tofauti miongoni mwa jamii ya Wamarekani kwa sababu, JonBenet pamoja na kuwa na umri mdogo, lakini alikuwa anashikilia mataji takriban 50 ya urembo kwa watoto aliyoshiriki katika maeneo tofauti nchini humo.


  Jina la JonBenet ni muunganiko wa majina ya baba yake John Bennet Ramsey 53, bilionea na mmiliki wa viwanda nchini Marekani na mama yake Patricia (Patsy) Ramsey ambaye naye aliwahi kushikilia taji la West Virginia mwaka 1977 nchini Marekani. Kutokana na mama yake kushiriki mashindano ya urembo enzi ya usichana wake, vivyo hivyo alitaka na mwanaye pia afuate nyayo zake.

  Awali John alifunga ndoa na mwanamke aliyetajwa kw ajina la Lucinda Pasch Ramsey “Cindy” mnamo July 1966 na walibahatika kupata watoto watatu ambao ni Elizabeth Ramsey ambaye alizaliwa mwaka 1969, lakini alikuja kufariki mnamo agosti 1, 1992 kwa ajali ya gari huko Illinois, Melinda Ramsey alizaliwa mwaka 1972 na John Andrew Ramsey aliyezaliwa mwaka 1976. Kati ya mwaka 1977 na 1978 John Bennet Ramsey na mkewe Lucinda Pasch Ramsey “Cindy” waliaachana kisheria.

  Mnamo Novemba 5, 1980 John Ramsey alifunga ndoa na Patricia Paugh Ramsey (Patsy) huko Atlanta Georgia na mtoto wa kwanza Burke Hamilton Ramsey alizaliwa mwaka 1987 na mtoto wao wa pili na wa mwisho JonBenet Ramsey alizaliwa mnamo Agosti 6, 1990 huko Atlanta Georgia.

  Alikuwa ni Patsy Ramsey mama wa mtoto JonBenet aliyeamka asubuhi na mapema na siku ya Desemba 26, 1996 na kukutana na barua ndefu sebuleni yenye kurasa tatu iliyoandikwa kwa mkono ikiwafahamisha kwamba mtoto wao JonBenet ametekwa nyara na watekaji hao walikuwa wanahitaji kiasi cha dola za marekani zipatazo 118,000 ili wamrejeshe akiwa salama. Pia barua hiyo ilikuwa na tishio la kutahadharisha familia ya JonBenet kwamba iwapo watawajulisha Polisi au FBI, Binti yao hatakuwa salama.
  626925_com_ransomnote.jpg

  Kwa mujibu wa Patsy Ramsey, haraka sana alianza kuchunguza hapo nyumbani kwao akianzia chumbani alipolala JonBenet na kwingineko, lakini hakuweza kumwona mwanaye zaidi ya kumkuta mwanaye mwingine wa kiume aitwae Burke aliyekuwa na umri wa miaka 9, akiwa amelala. Aliamua kwenda kumuamsha mumewe na kumpa ile barua ya watekaji. Pamoja na kwamba barua ile ilikuwa na tishio la kuitaka familia ile kutowajulisha Polisi juu ya suala lile, John Bennet Ramsey aliwajulisha Polisi na wakat huo huo aliwasiliana na meneja wa Bank anakoweka fedha zake ili akamilishe mipango ya kumpatia hizo fedha zinazotakiwa na watekaji haraka iwezekanavyo.

  Polisi walifika katika eneo la tukio muda mfupi baada ya kujulishwa. Utekaji nyara na mauaji siyo jambo la kutarajiwa sana katika mji wa Boulder, Colorado. Ukweli ni kwamba, hadi kufikia tarehe hiyo ya 26, Desemba, kulikuwa hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kuuawa kwa zaidi ya mwaka. Polisi wa Boulder walilazimika kuomba msaada kutoka kwa Polisi wa Denver na FBI. Muda si mrefu Polisi wale walifika na kwa kushirikiana na FBI walikagua nyumba yote iliyokuwa na vyumba 15, huku ikiwa imezungukwa na eneo la bustani la eka mbili, lakini hawakumpata mtoto JonBenet.
  Walipomaliza kukagua nyumba hiyo waliihoji familia ya JonBenet kwa saa kadhaa na pia walikaa na familia hiyo kwa muda kiasi wakisubiri simu kutoka kwa watekaji, ambapo hata hivyo hakuna simu iliyopigwa na ilipofika saa saba mchana maafisa wa Polisi na FBI waliondoka katika eneo la tukio wakiacha maagizo kwa familia ya John Ramsey kuendelea kumtafuta mtoto wao JonBenet, pale pale kwenye eneo la nyumbani kwao.

  Kwa mujibu wa maelezo ya John Ramsey ni kwamba aliendesha msako mkali katika nyumba yao kwa dakika 15 baada ya Polisi kuondoka. Msako huo ulijumuisha kila kona ya nyumba ile na hatimaye waliukuta mwili wa mtoto wao JonBenet akiwa amekwishauawa. Mwili huo waliukuta ukiwa kwenye chumba ambacho kilikuwa hakitumiki na ambacho vioo vyake vya madirisha vilikuwa vimevunjika. Ramsey aliuchukuwa mwili wa mwanae na kukimbia nao hadi sebuleni ambapo aliulaza karibu na mti wa Mkirismas ambapo mkewe alijaribu kutoa huduma ya kwanza ya kumpulizia hewa mdomoni akidhani labda mtoto amepoteza fahamu tu, lakini kumbe likwishafariki. Wakati huo huo majirani waliokuwa pale nyumbani kuwafariji walipiga simu ya dharura na kuwajulisha Polisi juu ya kupatikana kwa mtoto JonBenet akiwa amekwisha kufa.

  Kitendo cha Ramsey kuuondoa mwili wa mwanae kutoka katika eneo la tukio kwa sababu ya kutaka kuokoa maisha yake, kinaweza kueleweka kwamba alikuwa na nia nzuri juu ya maisha ya mwanae, lakini kwa upande mwingine kitendo kile kilikuwa kimetibua kabisa uchunguzi ambao ulitakiwa ufanyike pale pale kwenye eneo la tukio kabla ya kuondoa mwili huo. Hivyo kitendo cha kuondoa mwili huo kilisababisha kikosi cha uchunguzi kushindwa kufanya uchunguzi wa mwili huo ukiwa kwenye eneo la tukio. Hata hivyo Polisi waliuchukuwa mwili wa mtoto na kuondoka nao na baadae usiku huo mwili huo ulifanyiwa uchunguzi katika ofisa ya uchunguzi wa vifo ya wilaya.

  Siku iliyofuata asubuhi Daktari bingwa anayeshughuka na uhalifu dhidi ya watoto Dk. Charles Wecht alisema kwamba JonBenet alifariki saa nne usiku. Alieleza kwamba kifo chake kilisababishwa na kuzibwa pumzi na kupigwa kichwani na pia alikuwa amenajisiwa. Katika majumuisho yake kuhusiana na kifo cha mtoto JonBenet, Dk. Wecht alisema kwamba mtu aliyemuuwa mtoto huyo anaonekana ni mtu ambaye JonBenet alimfahamu na kumuamini. Dk. Wecht aliendelea kusema kwamba, JonBenet alikamatwa kama mateka na kuteswa lakini nia ya mtesaji ilikuwa ni kumnajisi kitu ambacho mtoto huyo hakukikubali, hivyo wakati anaendelea kumtesa ndipo akapoteza maisha. Kitu ambacho mhusika hakukitarajia. “Kwa kifupi ni kwamba, ulikuwa ni mchezo ambao ulitoa matokea mabaya.” Alimalizia kusema Dk. Wecht.

  Kwa kawaida kesi yoyote ya mauaji Polisi huanza kuitupia macho familia husika au mtu wa karibu na rafiki wa familia hiyo. Familia ya Ramsey haikuweza kuepuka hilo. Siku iliyofuata baada ya taarifa za kitaalamu kutolewa kuhusiana na kifo cha mtoto huyo, John na Patsy Ramsey walihojiwa kwa muda mrefu katika kituo cha Polisi cha Boulder na pia walitoa vielelezo vya nywele, damu kwa ajili ya vipimo vya DNA na pia muandiko wao kwa ajili ya kufananisha na muandiko wa kwenye barua ya muuaji. John Ramsey na mkewe waliwaambia polisi kwamba siku hiyo ya Krismas familia nzima ilikwenda kulala mapema kwa sababu siku inayofuata asubuhi walikuwa na mpango wa kusafiri kwenda katika mji wa Minneapolis kwa ajili ya mapumziko ya Krismas. Walimlaza JonBenet saa mbili kamili usiku na usiku huo hawakusikia purukushani yoyote. Kitu kilichowashtua asubuhi ni pale mkewe alipoona barua iliyoachwa na watekaji nyara ya madai ya fedha. Hata hivyo kutokana na Polisi kutokuwa na ushahidi wa kutosha wa kuwafungulia mashitaka ilibidi wawaachie.

  Siku iliyofuata asubuhi ya Desemba 29, baada ya misa ya kifamilia iliyofanyika katika kanisa la St. John’s Episcopal lililoko katika mji huo wa Boulder wanafamilia hao walisafiri kwa ndege na mwili wa JonBenet hadi katika mji wao wa zamani Atlanta Georgia ambapo walifanya mazishi ya mtoto wao ambayo yalihudhuriwa na waombolezaji zaidi ya 200. JonBenet alizikwa na moja kati ya magauni yake aliyowahi kushiriki nalo kwenye mashindano ya urembo.
  12162001patsyatgrave2.jpg img_4950.jpg
  Wakati huo huo Polisi walikuwa wakindelea kuipeleleza familia ya Ramsey kuhusiana na mauaji hayo na baada ya siku kadhaa walikuja na taarifa zenye viashiria ambavyo vilikuwa vinaonesha kwamba kati y John Ramsey au mkewe Patsy Ramsey au wote kuna uwezekano walihusika na mauaji ya JonBenet. Polisi walipata vielelezo kadhaa katika nyumba yao ya Boulder. Mojawapo kilikuwa ni kijidaftari kidogo kilichotumiwa na mtekaji nyara kuandika barua ya ujumbe kwa familia ya Ramsey lakini kukiwa na karatasi kadhaa zlizotumiwa kuandika ujumbe huo lakini zikaachwa kutokana na kukosewa.

  Polisi walishangaa kwa sababu waliamini kwamba mtekaji nyara yeyote angeandaa barua ya ya kudai malipo ya utekaji nyara (Ramsom Letter) muda mrefu kabla ya kutekeleza utekaji nyara. Hivi inawezekana kweli mtekaji nyara huyo akae muda wote huo kwenye nyumba ya mtu aliyemteka nyara na apate muda wa kukaa na kuandika barua yenye kurasa tatu kwa mkono kisha aondoke, tena akiwa amefanya jaribio la kuandika barua hiyo mara mbili baada ya kukosea? Hili ni swali ambalo liliwaumiza Polisi vichwa.

  Polisi pia kupitia picha zilizopigwa kwenye mwili JonBenet ukiwa umevuliwa nguo na kamera maalum inayoweza kusafisha picha hapo hapo muda mfupi baada ya kupigwa (Polaroid Camera) waliona makovu ya michubuko kwenye mikono yake kwa juu karibu na kwapa. Polisi walikuwa walijiuliza kwamba, je JonBenet alikuwa ni mhanga wa unyanyaswaji wa kijinsia na aidha wazazi wake au mtu aliye karibu na familia hiyo?

  Katika nyumba ya Ramsey iliyoko Minneapolis anayoitumia kwa likizo, maofisa wa Polisi walikuta kamba ambayo inafanana kabisa na kamba ambayo ilitumika kumnyongea JonBenet. Swali ni je ilifikaje pale? Utata mwingine uliowapa Polisi wakati mgumu kupata majibu ya kuridhisha ni kiasi cha fedha kilichotajwa na mtekaji nyara. Polisi ilikuwa haiwaingii akilini kwamba mtu bilionea kama John Ramsey aamriwe atoe kiasi cha dola sipatazo 118,000 tu. Kwa nini isiwe milioni moja, au mbili au hata zaidi?

  Ilibainika kwamba kiasi cha hizo dola 118,000 kilichohitajiwa na mtekaji nyara ndicho ambacho John Ramsey alilipwa kama Bonus yake ya mwaka kutokana na faida iliyozalishwa na kampuni yake. Je inawezekana jambo hili likawa ni nasibu (Coincidence) tu? Wapelelezi katika kesi hii iliyojaa utata walikuwa wakijiuliza maswali mengi ambayo hayakuwa na majibu. Wapelelezi wa Polisi waliamini kwamba, kama familia ya Ramsey haikuhusika na kumuuwa mtoto wao, basi inawezekana muuwaji wa mtoto wao ni mtu wao wa karibu ambaye anafahamu kwa usahihi taarifa zao za kifedha.
  Kulikuwa hakuna mahali popote katika nyumba yao kulionyesha kwamba mtekaji nyara alitumia nguvu ili kuingia katika nyumba yao, hapakuwepo na dalili yoyote ya nyumba hiyo kuvunjwa. Lakini hata hivyo Polisi walikuwa wanajiuliza, iweje mtambo maalum wa ulinzi (Security system) ulizimwa?

  Lakini swali ambalo lilikuwa linawatatiza Polisi hao wa upelelezi lilikuwa, ni kwa nini JonBenet Ramsey aliuwawa? Ni jambo lililowazi kwamba aliuwawa muda mrefu tu kabla ya mke wa Ramsey hajaona barua iliyoachwa na mtekaji nyara ya kudai malipo, na mwili wake uliachwa mle mle ndani mahali ulipokutwa. Je ni kitu gani ambacho familia ya Ramsey ingenufaika nacho kwa kuwalipa watekaji wakati wanajua mtoto JonBenet amekwishakufa?

  Wakati kukiwa hakuna mtuhumiwa yeyote ambaye ameshatiwa mbaroni kuhusiana na mauaji ya binti yao, familia ya Ramsey ilikuwa inajua dhahiri kwamba wanatiliwa mashaka kuhusika na mauaji ya binti yao. Mnamo Januari 1, 1997, ikiwa imepita wiki moja tangu binti yao auawe, John na Patsy Ramsey walisafiri kwa ndege wakiwa pamoja na timu ya washauri wao kuelekea Atlanta. Walipokuwa kule, waliaonekana kwenye TV ya CNN, lengo likiwa sio kuomba msaada katika kufanikisha kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa mhusika wa mauaji ya binti yao, bali pia kukanusha tuhuma za kuhusishwa na mauaji ya mtoto wao. Akizungumza kupitia TV ya CNN John Ramsey alisema, “tuhuma hizi zimetutia kichefuchefu” alikuwa akizungumzia habari zilizosambaa kwenye vyombo vya habari zikimtuhumu yeye na mkewe kuhusika na mauaji ya binti yao.

  “Sisi ni familia iliyobobea kwenye ukristo.” Alisema, kisha akaongeza, “na kuhusishwa kwetu katika jambo hilo, ni kitu kisichowezekana”

  Ramsey alisema kwamba, ametoa zawadi ya kiasi cha doal 50,000 kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwa muuwaji wa JonBenet. Aliendelea kusema kwamba amekubaliana na mpelelezi wa zamani wa FBI aliyestaafu John Douglas arudi kazini kushughulikia kesi ya mwanae. John Douglas ni mpelelezi mahiri aliyejijengea heshima katika shirika hilo la upelelezi la nchini Marekani la FBI. Wakati wa mahojiano yao na CNN Patsy hakuwa mzungumzaji lakini baadae alisema kwa kifupi kwamba anaamini muuwaji wa binti yao yupo na hajakamatwa tu.

  Polisi wa mji wa Boulder hawakufurahishwa na maelezo ya familia ya Ramsey wakati wanaongea na CNN, na siku iliyofuata Meya wa mji huo na maofisa wa Polisi waliitisha mkutano na vyombo vua habari ambapo walikanusha kauli iliyotolewa na mke wa Ramsey aliposema kwamba muuwaji wa binti yao yupo na hajakamatwa. Maofisa hao walisisitiza kwamba mauaji ya JonBenet siyo endelevu, hivyo waliwataka wakazi wa mji huo kulala kwa amani bila hofu kwa sababu hakutatokea mauaji kama hayo tena. Maofisa hao walidai kwamba wanamjua aliyemuuwa mtoto JonBenet Ramsey na bado kitambo kidogo watathibitisha madai yao.

  Kwa muda mfupi Polisi walihamisha hisia zao kuwatuhumu John na Patsy Ramsey na mauaji ya binti yao na kulekeza hisia zao kwa watoto wake aliowazaa katika ndoa yake ya awali waitwao Melinda na John Andrew Ramsey.
  Pamoja na minong’ono iliyoenea kwamba walionekana katika mji huo wa Bouliver siku ya Krismas, lakini wote walidai kwamba walikuwa Atlanta siku hiyo ya tarehe 25 Decemba na siku iliyofuata yaani tarehe 26 Desemba waliondoka katika mji huo kuelekea katika mji wa Minneapolis ambapo walipanga kukutana na baba yao pamoja na mama yao wa kambo na wanae katika nyumba yao wanayoitumia wakati wa likizo hapo Minneapolis, hata hivyo rafiki mmoja wa familia aliwapigia simu na kuwajulisha kwamba mtoto JohnBenet ametekwa nyara na hajulikani alipo. Walipanda ndege hadi katika mji wa Denver na hapo walichukuwa taxi hadi Boulder.

  Polisi waliyachukuwa maelezo yao na kutokana na kutokuwa na muunganiko na tukio hilo, walibadilisha hisia zao kutoka kwa watoto hao na kuwageukia John na Patsy Ramsey wazazi wa mtoto JonBenet.

  Mnamo Februari 8. 1997 Kitengo cha kuzuia uhalifu cha Boulder kilitangaza kwamba familia ya Ramsey itatoa awadi ya dola 100,000 kwa mtu yeyote atakayejitokeza kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa muuaji na kuhukumiwa. Rais wa kitengo cha kuzuia uhalifu cha kimataifa Larry Wieda alifafanua juu ya hatua hiyo. “Tunachofanya ni kuhakikisha hakuna taarifa zinazotupita juu ya tukio hili.” Aliendelea kusema kwamba kwa kawaida taasisi anayoiongoza huwa inatoa zawadi inayofikia dola 10,000, lakini akaongeza, “Siwezi kukumbuka kesi yoyote ambayo ilipatiwa ufumbuzi kutokana na kiasi kikubwa cha zawadi kilichoahidiwa.”

  Hata hivyo kiwango hicho kilichotangazwa na familia ya Ramsey kiliamsha mwamko kutoka kwa jamii ya Wamarekani kutoa taarifa kwenye taasisi hiyo ya kuzuia uhalifu. Kwa muda mfupi taasisi hiyo ilipokea simu zaidi ya 1,500 kutoka kwa raia wema ambao walidai kwamba wana taarifa ambazo zitasaidia kupatikana kwa muuaji. Mpaka kufikia katikati ya Februari Polisi walikuwa wamepokea barua zipatazo 1,000 na simu zapatazo 3,000. Polisi walisema kwamba kati ya hizo taarifa ni asilimia 5 to ambazo zinaonekana huenda zikazaa matunda, lakini pia waliwatahadharisha wananchi kutowapotezea Polisi muda. Kauli hiyo ilitokana na baadhi ya taarifa kuonekana zisizo na mashiko. Akitolea mfano baadhi ya taaarifa hizo ni pamoja na zile ambazo wapo waliodai kwamba wana uwezo wa kufanya miujiza na kumbaini muuaji.

  Kuanzia hapo, Polisi wakawa hawatoi taarifa zozote kwenye vyombo vya habari kuhusiana na kesi hiyo, na upelelezi wa kesi hiyo ulionekana kufanywa kwa siri sana. Wakati John Meyer wa kitengo cha uchunguzi wa maiti katika wilaya ya Boulder alipomaliza uchunguzi wa mwili wa JonBenet Ramsey hapo mnamo Februari 11, 1997, alikataa kutoa taarifa kwa undani kuhusiana na matokeo ya uchunguzi wake akidai kwamba askari wa upelelezi wa mji huo wa Boulder na waendesha mashitaka wanaohusika na kesi hiyo walimuonya kwamba, iwapo atatoa matokeo ya uchunguzi wake itaathiri kwa kiasi kikubwa mwenendo wa upelelezi wao katika kumtafuta muuaji.

  Msemaji wa kitengo hicho cha uchunguzi wa maiti alisema kwamba, miongoni mwa taarifa za uchunguzi wa mwili wa binti huyo ambazo Polisi na ofisi ya mwanasheria wa wilaya ambazo wasingependa ziwekwe hadharani ni kuhusu majeraha mangapi yamekutwa kwenye mwili wa marehemu, idadi ya vielelezo vilivyokusanywa baada ya uchunguzi, na mbinu iliyotumiwa na muuaji kutekeleza mauaji hayo (details of the Modus operand of the killer)
  Hata hivyo kuna taarifa iliyovuja kufuatia uchunguzi wa mwili wa binti huyo ni kwamba, mwili wa binti huyo ulikutwa ukiwa na michubuko ya muda mrefu katika uke ambapo ripoti hiyo ilieleza kwamba michubuko hiyo inawezekana ilitokana na binti huyo kunajisiwa mara kwa mara.

  Haraka sana msemaji wa familia ya Ramsey Pat Korten alizungumzia tuhuma hizo na alimshirikisha aliyekuwa daktari wa binti huyo ambaye alikanusha kwamba hajawahi kuona ushahidi wowote kwa binti huyo unaoonyesha kwamba alikuwa akinyanyaswa kijinsia. Mwezi huo wa Februari haukuwa mzuri sana kwa familia ya Ramsey, kutokana na jinsi Polisi walivyokuwa wakiizungumzia kesi ya binti yao na hiyo ilisababisha mahusiano ya familia ya Ramsey na Polisi kutokuwa mazuri.

  Ilipofika Februari 12, 1997, Polisi waliwataka John na Patsy Ramsey kuripoti makao makuu ya Polisi kwa ajili ya kutoa sampuli nyingine ya muandiko wao kwa mkono. Msemaji wa familia hiyo Pat Korten akizungumza na vyombo ya habari aliwaambia waandishi wabari kwamba wateja wake wamekataa kukubaliana na matakwa hayo ya Polisi kwa sababu walishatoa sampuli zao za muandiko wao, pamoja na damu na sampuli ya nywele zao. Ofisi ya mwanasheria wa wilaya ilijibu hoja hiyo na kutishia kutumia mamlaka ya mahakama kumshurutisha John na Patsy Ramsey kutekeleza matakwa ya Polisi.

  Kutokana na tishio hilo Ramsey na mkewe walikubali kutoa ushirikiano kwa Polisi, hivyo walikwenda kutoa sampuli ya mwandiko wao. Hata hivyo siku chache baadae Polisi waliwasiliana na Ramsey na mkewe wakihitaji tena sampuli ya miandiko yao. Kitendo hicho kilisababisha msemaji wa familia ya Ramsey Pat Korten kuzungumzia jambo hilo kwenye vyombo vya habari. Akiongea na vyombo vya habari msemaji huyo alisema, “walileta maombi yao yasiyo na maandishi kwamba wanahitaji sampuli nyingine ya muandiko, na tulitoa ushirikiano, hivi sana wanahitaji tena sampuli nyingine, sisi tunawaambia watupe sababu ambayo itatuingia akilini ya kuhitaji sampuli hiyo mara kwa mara. Tumekuwa na ushirikiano na Polisi tangu awali, lakini sasa sidhani kama tunaweza kuendelea……. Nadhani, lakini sina uhakika.”

  Kutokana na John na Patsy Ramsey kuonekana makao makuu ya Polisi mara kwa mara, waandishi wa habari walijenga nadharia kwamba wao ndio washukiwa wakuu wa mauaji hayo. Kuanzia hapo wakawa wanawindwa na vyombo vya habari kila waendapo ambapo nao wakawa wanawakwepa kwa kuhama kutoka eneo moja la siri walipokuwa wamejificha hadi jingine ili kuwakwepa waandishi wa habari.

  Mnamo Februari 24, 1997, mwanasheria wa wilaya ya Boulder Alex Hunter aliiwasilisha maelezo mafupi kuhusu kesi hiyo katika mahakama ya wilaya kuhusiana na shauri hili ambalo bado lilikuwa likiwaumiza vichwa wapelelezi wa Marekani. Kwa kifupi mwanasheria huyo alisema, “John na Patsy Ramsey bado hawajaondolewa kwenye tuhuma za mauaji ya binti yao.”

  Msemaji wa familia ya Ramsey hakuikalia kimya taarifa ile. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari hapo mnamo Februari 25, Pat Korten alisema, kinachotakiwa ni kusikiliza kile Polisi na ofisi ya mwanasheria wa wilaya walichokisema kwamba wanaichukulia familia ya Ramsey kama watuhumiwa namba moja katika orodha yao. Hata hivyo Polisi waliwataka tena John na Patsy Ramsey kwenda kutoa sampuli nyingine ya muandiko wao kwa mkono, lakini hata hivyo walionekana kukosa ushahidi makini wa kuwafikisha mahakamani.

  Mnamo June 24, 2006 Patricia Ramsey (Patsy) alifariki akiwa na umri wa miaka 49 huku akiacha kitendawili cha kukamtwa kwa muuaji wa mwanae hakijateguliwa. Mama huyu alifariki kwa ugonjwa wa kansa ya kizazi, ambayo aligundulika kuwa nayo mwaka 1993. Alizikwa pembeni ya kaburi la mwanaye JonBenet Ramsey huko Georgia.
  [h=3]Mnamo Agosti 16, 2006 mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la John Mark Karr raia wa Marekani aliyekuwa akifundisha Kiingereza nchini Thailand alikamtwa baada ya kukiri kwamba ni yeye aliyemuuwa mtoto JonBenet Ramsey. John Mark Karr alikuwa akiwasiliana kwa njia ya barua pepe (email) na mwandishi mmoja wa habari na profesa wa chuo kiku cha Colorado aitwae Michael Tracey. John Karr Alikuwa akitumia anuani ya barua pepe ya December261996@yahoo.com . tarehe hiyo ndiyo ambayo mtoto Jonbenet aliuawa.[/h][h=3]Alirudishwa nchini Marekani lakini baada ya uchunguzi wa vipimo vya DNA vikaonyesha kwamba havifanani na vile vilivyokutwa kwenye mwili wa mtoto JonBenet.[/h]Mnamo Agosti 28, 2006 ofisi ya mwanasheria ya wilaya ya Boulder ilisema kwamba John Mark Karr hatashitakiwa kwa kusababisha usumbufu na alitaja gharama za upelelezi wa tuhuma zake alizojipachika kuwa zilifikia kiasi cha dola 13,000 na kiasi kingine kinachookadiriwa kufikia dola 30,000.

  Rafiki wa karibu wa familia ya Karr aitwae McCrary alisema kwamba Karr hakuhusika na mauaji hayo, “huyu ni mtu mwenye tabia ya kubaka watoto wadogo (Pedophile) na sio muuaji” alisema McCrary. McCrary alimuelezea John Karr kama mtu mwenye akili za ziada (Genuis) ambaye alitumia mbinu hiyo ya kukiri Kumuua mtoto JonBenet ili kukwepa kifungo nchini Thailand ambapo alikuwa kikabiliwa na tuhuma mbalimbali za ubakaji wa watoto. Na alijua kwamba kwa kukiri kwake kuhusika na mauaji hayo atarudishwa nchini Marekani ambapo alijua wazi hatakutwa na hatia ya kosa hilo.

  Mnamo mwaka 2010 Johna Mark Karr alitangaza rasmi kutaka atambuliwe kama mwanamke (Trans Woman) ingawa hakufanya upasuaji wa kubadili jinsia. Alitaka atambuliwe kwa jina la Alexis Valoran Reich na alipata kitambulisho rasmi chenye utambulisho huo mpya na alibadilisha muonekano wake na mavazi kwa kuvaa kama mwanamke
  image.jpg
  Alexis Valoran Reich

  John Bennet Ramsay na familia yake walihamia katika jimbo la Michigan na kuanza maisha mapya baada ya misukosuko ya kesi hii.

  Hata hivyo bado Polisi wanaendelea na upelelezi wa kesi hii.
   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Jun 15, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Wasomaji na washabiki wa kipengele hiki cha kesi za kila Ijumaa, leo nimewaletea kesi hii ambayo mpaka leo hii haijapatiwa ufumbuzi na FBI. Pengine unaweza kushangaa inakuwaje nchi kama Marekani ambayo inatisha kwa upelelezi lakini inashindwa kupata ufumbuzi kwa kesi hii ambayo mauaji yake yaliacha maswali mengi sana yasiyo na majibu.

  lakini labda utakaposoma mkasa mzima unaweza kujua sababu ya kushindwa huko. Kesi hii ni ndefu sana na inapatikana katika vyanzo vingi sana vya habari vya mtandaoni. nimejitahidi kadiri ya uwezo wangu kuiandika kwa umakini bila kuacha eneo hata moja ambalo linahusiana na kesi hii. labda niseme tu kwamba huenda mtiririko wa mkasa huu usiupende, lakini kwa kweli nimejitahidi sana kuiandika kwa umakini ili nisipoteze ladha.

  Ninawatakia usomaji mwema na mapumziko mema ya mwishoni mwa Juma.
   
 3. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  LOL....Yaani umepiga teke glass ya Jack Daniel ikiwa imefikia lips zangu. Nina wasi wasi na watoto wa mtalaka wa bwana Bennet.

  Inasikisha sana kuona watoto wadogo wakinyanyaswa na kupotezewa maisha na watu wenye roho mbaya na ukaliti wa hali ya juu. Pumzika Kwa Amani JonBennet.
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Jun 15, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  TaiJike , hilo unalosema limeshazungumziwa sana, lakini bado ushahidi hauwakamati kabisa, hebu soma huu mtiririko kuhusiana na tuhuma hizo

  John Andrew Ramsey
  The JAR Did It Theories

  • Motivation. Motivations for JAR to kill JBR range from jealousy to cover-up of prior sexual abuse.
  • JAR as Killer. The most clearly stated JAR did it theory is from Internet poster BlueCrab who believes this would account for a) prior sexual abuse; b) use of erotic asphyxiation device; and c) Barnhill's account of seeing JAR on Christmas afternoon. One of JAR's friends who provided an alibi for him was a pilot.
  • JAR as Accomplice. Because JAR has a fairly strong alibi for being in Atlanta on Christmas Day, some believe JAR may have helped plan a kidnapping with friends and even written the ransom note, but the two friends screwed up and killed JBR accidently.

  Incriminating Evidence Related to JAR

  • A neighbor (Barnhill) saw someone who looked like JAR walking up the hill near the Ramsey house on Christmas afternoon. Internet posterBlueCrab claims that Barnhill later recanted his story about this sighting.
  • A blanket with semen sourced to JAR was found in the suitcase in the basement room close to where JBR's body was found.
  • While the time window is narrow, some believe JAR had sufficient time to fly to Boulder, kill JBR and return to Atlanta in time for his planned flight to Charlevoix on December 26 (source?). These individuals believe it was a little too convenient for JAR to have kept for months a movie ticket that was helped to establish that he was in Atlanta on Christmas night 1996, hence this alibi must have been pre-planned.
  Exculpatory Evidence Related to JAR

  • Alibi.

  1. Police-Established JAR Timeline. According to Schiller, police ascertained that on Christmas Day, "at about 8:30 P.M., John Andrew went to his friend Brad Millard's home in Marietta to play video games. After an hour, they left to catch a 10:30 show at the Town and Country Movie Theater in Marietta with another friend, Chris Stanley. John Andrew said that after the movie he went back to Brad Millard's house to get his car and arrived back at his mother's house at 1:00 A.M. The next morning he left his mother's house with Melinda, who had come there to pick him up. Together they boarded a flight to Minneapolis at 8:36 A.M. local time. That was forty-four minutes after Patsy called 911 to report that JonBenetwas missing." (Schiller, 1999a:67).
  2. No Record of Commercial Airline Travel. Schiller later states that police "finished their background checks on John Andrew and Melinda and had verified commercial airline schedules and private flight plans and found no record that either of them had traveled the night of December 25. Their alibis were solid." (Schiller 1999a:257). Any theory of John's flying back in a private plane would have to explain how he managed to avoid detection and whose plane he used to go back and forth several thousand miles.
  3. Alibi Verified by JAR's Mother. Internet poster BlueCrab has stated that "JAR's mom, Lucinda, also verifies that JAR was home with her on the 24th and 25th and left on a flight to Minneapolis on the morning of the 26th."
  4. Implausibility of Conspiracy. Thus, for BlueCrab's theory to be correct, at least three people would have to be lying. Moreover, if BlueCrab's account of JAR being in Boulder and attending the December 23 party were correct, many more people than Joe Barnhill would have seen JAR; it seems implausible that after 10 years, not a single one of the 30 or so people at that party would have come forward to authorities to report what they saw. Fleet White, in particular, had a falling out with the Ramseys and would have no particular incentive to facilitate their trying to cover up JAR's involvement if that's what happened.

  • DNA Not a Match. JAR's DNA does not match DNA collected at the scene.
  • JAR Officially Cleared. John Andrew Ramsey (JAR) has been officially cleared by law enforcement based on evidence that he was in Atlanta on December 25, 1996 (Zaret 1997).
  Melinda Ramsey Long
  The Melinda Ramsey Long Theory
  Melinda Ramsey, John's daughter from his first marriage, only comes under suspicion because she was JonBenet's half-sister. Possible motivations relate to jealousy or perhaps anger toward either John Ramsey or Patsy Ramsey. Because she was a family member, law enforcement felt compelled to investigate her alibi to confirm there was no reason to suspect her.

  Incriminating Evidence Related to Melinda

  • Palmprint on Wine Cellar Door Frame. A palmprint was found on the door-jam to the wine cellar room in which JBR's body was found.According to a "source close to the case" police later determined this print belonged to Melinda Ramsey.
  Exculpatory Evidence Related to Melinda

  • Alibi. According to Schiller, "Melinda. who had worked at a hosptial in Marietta, Georgia, finished her shift at about 7:00 A.M. on Christmas day. That afternoon, John Andrew, Harry Smiles, Melinda, and her boyfriend, Stewart Long, exchanged gifts at Lucinda's home in Marietta. In the afternoon, they all went across the street to a neighbor's for dinner. Melinda and Stewart Long left the dinner party about 7 P.M., and Melinda started to pack for an early flight the next day. At 9:00 P.M. they went to visit Guy Long, Stewart's uncle, and after visiting other friends, were home by midnight" (Schiller, 1999a:66-67).He later states that police "finished their background checks on John Andrew and Melinda and had verified commercial airline schedules and private flight plans and found no record that either of them had traveled the night of December 25, Their alibis were solid." (Schiller 1999a:257).
  • DNA Not a Match. Melinda Ramsey's DNA does not match.
  • Melinda Officially Cleared. Melinda Ramsey has been officially cleared by law enforcement based on evidence that she was in Atlanta on December 25, 1996 (Zaret 1997).
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Jun 15, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Halafu tena kuna huyu mchambuzi alizungumzia tuhuma hizo akiambatanisha na vidokezom kadhaa:

  John Andrew Ramsey
  [HR][/HR]
  Here are some things I feel pecuilar about JAR:

  1.) The R's neighbor, Joe Barnhill, reported seeing John Andrew walk up to the R's house, on 12/25. Does anyone know if this sighting was when the R's had already gone to the Whites house? Barnhill later changed his statement to say that he might have been mistaken.

  2.) There is no home video footage of Christmas morning. There are only two pictures. Was JAR in any of those pictures and videos that they had to be erased?

  3.) One of the original people that John has stayed close to throughout the years was his pilot, Mike Archuletta. Did Mike give JAR the plane ride to and from Boulder?

  4.) Why did John and Patsy say that they wouldn't answer any questions until the police cleared JAR and Melinda?

  5.) JAR's suitcase with his blanket, book, and semen were found near JonBenet's body.

  6.) It's been said that JonBenet was being molested but not on a regular basis. Since JAR was in Boulder but not always at home, he would of had irregular access to JBR. Didn't she go to the school nurse on Mondays? Did JAR make a stop at home during the weekend?

  7.) Why did John lawyer up his family like his ex-wife and not Patsy's family? (I'm not positive about this; but I'm pretty sure Lucinda got a lawyer and Nedra didn't)

  8.) LE cleared JAR because of a picture of him at an ATM. Wouldn't that picture be really grainy? If he spent Christmas with his mom's family, then why aren't there any pictures of him there? Also, didn't he go to the movies too on 12/25? So he went to his mom's house and the movies on 12/25? Or was his mom's house on 12/24?

  Now, I know that someone will say that Patsy would have never covered up for JAR but John was the one with money and connections. He could have told Patsy that she keeps her mouth shut about his son, or he'll throw her under the bus.

   
 6. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Hapo ndo nashindwa kuelewa kwa nini hawa askari/wapelelezi wanashindwa kuunganisha matukio ambayo hata mimi ambaye sijasomea shushu naweza mpata muuaji.
   
 7. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  Mbona kama hiyo familia inahusika na hayo mauhaji ya mtoto wao?, ili kuwaje polisi walipekua hiyo nyumba na viunga vyake na washindwe kuupata mwili wa Marehemu (nadhani walikuwa na mbwa pia) na walipoondoka tu ndio mwenye mji akaupata?

  Kitendo cha Alarm kuzimwa na nyumba kutokuwa na dalili zozote za kuvunjwa inatia shaka pia,

  kama huyo mtoto alikuwa amelazwa na akachukuliwa mpaka basement na kubakwa (ambayo iko ndani ya nyumba hiyohiyo) bila kupiga kelele yoyote?

  Hiyo ya note ya kudai fedha ndio yenye mashaka makubwa sana, mtekaji aliingia saa ngapi ndani na kupata muda wa kuandika page tatu? na kuna zingine mbili alikosea ni mtekaji gani ambaye hakuwa na wasiwasi kabisa na kumbuka pia alitumia muda huohuo kubaka
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Jun 15, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kituko kuna madai kwamba muuaji ni mtoto wa mzee John Ramsey aitwae John Andrew Ramsey kama anavyoelezewa hapo juu na wachambuzi na inadaiwa kwamba John Ramsey alimuonya mkewe Patsy kutosema lolote la sivyo angekiona cha moto.......... hiyo ni kutaka kuisitiri familia na fedheha ambayo ingeipata.........
  Kuna mengi yanasemwa lakini Polisi hawana ushahidi makini wa kumkamata muuaji.
   
 9. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi,
  Kuna kipande ambacho umekiandika kinasema Daktari aliona kuwa huyo mtoto alishanajisiwa tangu siku nyingi na inaonekana kabisa hata alipochukuliwa hapo kitandani hakupiga kelele kwani alichukuliwa na mtu anayemjua

  Mtambuzi swali linabaki palepale, huo waraka Uliandikwa saa ngapi?, au Andrew alikuja na kidaftari chote chenye huo waraka+ hizo page mbili alizokosea?
  kwa nini polisi hawakumwambia Andrew atoe sample zake za maandishi ili waone kama sio yeye ni mwandishi?
   
 10. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,029
  Trophy Points: 280
  Hii kesi ina utata sana......... Kwanini polisi na ofisi ya mwanasheria wa wilaya hawakutaka taarifa hizi ziwekwe hadharani??
   
 11. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mtambuzi hebu elezea vizuri naona kama umenichanganya hapo juu!!! Alinyongwa na sio kuzibwa pumzi????
   
 12. k

  kaeso JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Asante sana Mtambuzi kwa mkasa huu. Kwa mtazamo wangu familia yenyewe ya huyo mtoto ndio inahusika na mauaji haya.
  Uwe na wikendi njema.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,029
  Trophy Points: 280
  Ndo maana nasema hii kesi ni Full utata..... Ila baba yake binti anaweza akahusika na mauaji? Kama siye, ni nani aliyezima mtambo wa security system ambao naamini lazima unazimiwa ndani ya nyumba.


  Kulikuwa hakuna mahali popote katika nyumba yao kulionyesha kwamba mtekaji nyara alitumia nguvu ili kuingia katika nyumba yao, hapakuwepo na dalili yoyote ya nyumba hiyo kuvunjwa. Lakini hata hivyo Polisi walikuwa wanajiuliza, iweje mtambo maalum wa ulinzi (Security system) ulizimwa?

   
 14. mbalu

  mbalu JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mtambuzi hii dhambi ni kubwa mno baba wa mtoto ndiye muuaji pengine mama alizunguka mbuyu na digi akashitukia hivyo kuazinsha mateso na udhalilishaji kwa kid huyu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Asnam

  Asnam JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 4,268
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  haya wababa wengine nuksi mtu anaamua kula kuku na mayai yake bila haya mweh!!!!!!!!maskini princess patricia R.I.P.
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Jun 15, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Huu mkasa unasikitisha sana lakini ushahidi unaonyesha familia imehusika kwa namna fulani.
   
 17. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #17
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  That is one, another thing ina maana huyo baba alikua anatabia ya kumfanya mwanae?!mpaka kumletea hiyo michubuo???
  Na kama ni kaka mtu, aliingia akazima alarm akamchukua mdogo wake na kumfanyia hivyo mpaka akasahau suitcase yake, je alikua anatabia ya kwenda kwa baba yake mara kwa mara na kumnajisi mdogo wake???!!!

  Natamani kumjua muuaji daaah
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Jun 15, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi, ukipata muda itafute kesi ya mauaji ya James Byrd, Jr.

  Hii ni moja ya kesi ambazo siwezi kuzisahau.
   
 19. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #19
  Jun 15, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,029
  Trophy Points: 280
  Unataka kumjua muuaji? Muuaji ni huyu hapa: (Usisahau mwanae wa kiume alikuwa na miaka 9 tu, asingeweza fanya mambo makubwa namna hii)

  Walipomaliza kukagua nyumba hiyo waliihoji familia ya JonBenet kwa saa kadhaa na pia walikaa na familia hiyo kwa muda kiasi wakisubiri simu kutoka kwa watekaji, ambapo hata hivyo hakuna simu iliyopigwa na ilipofika saa saba mchana maafisa wa Polisi na FBI waliondoka katika eneo la tukio wakiacha maagizo kwa familia ya John Ramsey kuendelea kumtafuta mtoto wao JonBenet, pale pale kwenye eneo la nyumbani kwao.

  Kwa mujibu wa maelezo ya John Ramsey ni kwamba aliendesha msako mkali katika nyumba yao kwa dakika 15 baada ya Polisi kuondoka. Msako huo ulijumuisha kila kona ya nyumba ile na hatimaye waliukuta mwili wa mtoto wao JonBenet akiwa amekwishauawa. Mwili huo waliukuta ukiwa kwenye chumba ambacho kilikuwa hakitumiki na ambacho vioo vyake vya madirisha vilikuwa vimevunjika. Ramsey aliuchukuwa mwili wa mwanae na kukimbia nao hadi sebuleni ambapo aliulaza karibu na mti wa Mkirismas ambapo mkewe alijaribu kutoa huduma ya kwanza ya kumpulizia hewa mdomoni akidhani labda mtoto amepoteza fahamu tu, lakini kumbe likwishafariki. Wakati huo huo majirani waliokuwa pale nyumbani kuwafariji walipiga simu ya dharura na kuwajulisha Polisi juu ya kupatikana kwa mtoto JonBenet akiwa amekwisha kufa.

  Kitendo cha Ramsey kuuondoa mwili wa mwanae kutoka katika eneo la tukio kwa sababu ya kutaka kuokoa maisha yake, kinaweza kueleweka kwamba alikuwa na nia nzuri juu ya maisha ya mwanae, lakini kwa upande mwingine kitendo kile kilikuwa kimetibua kabisa uchunguzi ambao ulitakiwa ufanyike pale pale kwenye eneo la tukio kabla ya kuondoa mwili huo. Hivyo kitendo cha kuondoa mwili huo kilisababisha kikosi cha uchunguzi kushindwa kufanya uchunguzi wa mwili huo ukiwa kwenye eneo la tukio. Hata hivyo Polisi waliuchukuwa mwili wa mtoto na kuondoka nao na baadae usiku huo mwili huo ulifanyiwa uchunguzi katika ofisa ya uchunguzi wa vifo ya wilaya.
  1. Polisi na uzoefu wao wameusaka mwili nyumba nzima wakaukosa
  2. Baada ya polisi kuondoka, baba mtu akauona mwili (Usisahau alishautafuta akaukosa kabla polisi hawajafika)
  3. Baada ya kuuona, badala ya kuwaita polisi akauchukua na kuupeleka sebuleni (ofkoz ili alama zake zikionekana kwenye mwili wa marehemi, ionekane ni wakati anauchukua mwili na kuupeleka sebuleni)

  Ningekuwa mimi ningemtia hatiani baba wa marehemu.
  Haki ya wallah tena.
   
 20. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #20
  Jun 15, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  @Yummy hapo kuna utata wa lugha, Daktari alitumia neno "asphyxiated"
  Kwa mujbu wa kamusi ya kiswahili ya TUKI neno hilo linatafsiriwa kama "asphyxia n hali ya kukosa hewa yakutosha. asphyxiate vt kaba, nyima pumzi.~tion n."
  Lakini ukiona picha ya mchoro wa mtoto JonBenet ina kamba shingoni..


  [​IMG]

  Je ilipaswa litumike neno gani hapo?
   
Loading...