Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Mwambieni Mengi ataje wale wengine watano alafu tutamuunga mkono kweli kwa sababu watamtesa sana.

Kasome kwenye list of shame ya Dr Slaa. Ni msaada tu.

Sidhani kama wewe ni muungaji mkono mzuri. Kama umeshindwa kwenye hatua moja kwenye hatua tano utaweza wapi?

Kumbuka safari zote huanza na hatua moja.
 
Lipumba angetuambia Mengi alichokosea ni nini, kuwataja hawa jamaa au kumsaidia Mkwere katika hii vita, kama Mengi anatafuta Umaarufu kwa Mkwere basi Nae Lipumba anatafuta umaarufu kupitia Mengi

lipumba kasahau "Never does a man portray his character more vividly than when he is proclaiming the character of another…! Winston Churchill 1874-1965, Former British Prime Minister"

Sasa hapa anajianika vizuri kama sophia na wengne watakaofuata.
 
sidhani kama ni kijana wa Usalama wa Taifa, but what I know for sure ni kwamba angecheza karata zake vizuri kabla ya 1995, angekua mtu mkubwa kwenye system (inasemekana possibly Prime Minister)...that was thru connection ya Chairpesron ambaye alikua ni "heavyweight" ndani ya CCM kutoka mkoa mmoja wa kanda ya magharibi (he is now deceased) ambaye alikua guardian/godfather wake somehow...but before they sat down with him, nadhani offer ya CUF ikawa more tempting.....
 
sijaona kosa la LIPUMBA mimi..from the best of my knowledge, a mistake is taken into record if committed by someone who is CAPABLE OF DOING THE SAME....nafuatilia siasa za BONGO tangu miaka ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi..ajitokeze mtu anikumbushe LIPUMBA kaongeza nini cha maana kwa WATANZANIA,na pia kwa USOMI wake kama 'MCHUMI ALIYEBOBEA' ametoa mchango gani hata wa kuamsha UMMA juu ya matatizo MAKUBWA yanayoendelea katika nchi yetu..KUNA MTU AMEFIKA NYUMBANI (kijijini) ANAPOTOKA LIPUMBA? haihitaji ushahidi wa ziada kwa nyinyi wadau kufahamu kwamba LIPUMBA is just another LI-PUMBA in TANZANIA,hana mchango wowote wa ziada,ni aina ya wanasiasa uchwara walioingia kwenye siasa UKUBWANI kwa SHAUKU na si MIKAKATI..he is a good chap in HATE-POLITICS (AM TEMPTED TO LABEL HIM A RELIGIOUS FUNDAMENTALIST).USHAURI WANGU KWAKE NI RAHISI SANA,2010 ATULIE, AJARIBU KUGOMBEA UBUNGE NYUMBANI KWAKE, AKAPAMBANE BUNGENI SO THAT WE MAY PROVE IF AT ALL HE IS WORTH ANYTHING...ndugu zangu CUF wanatakiwa wawe makini na huyu mheshimiwa, otherwise their diminishing chances of reviving dwindling popularity in the MAINLAND shall never be realized...

KWA MAMA YANGU SOPHIA SIMBA.....
"POLITICS IS A DIRTY, VERY DIRTY GAME...FROM WHAT I CAN SEE IN YOU, YOUR NOT ENTITLED TO EAT EVEN WITH THEIR HOUSEGIRL...namaanisha, if at all wanakutumia, amini kwamba hawana COMMON GOAL na wewe, utadondoshwa njiani"

MY HONOURABLE PRESIDENT:
"LET ME TELL YOU ONE THING; EVEN THE LAYMEN, OR TERM THEM SOLID MAJORITY, KNOW WHO IS WITH YOU AND WHO'S NOT WITH YOU IN YOUR VERY OWN CABINET...2010 SIO MBALI, UKIMYA NA UPOLE WAKO UNATUTIA MASHAKA MAZITO SANA WHEN CONSIDERING THE FATE OF OUR BELOVED MOTHERLAND...HIVI TUPO PAMOJA KWELI!??..."

am out....

Very nice.... honest said
 
kwa mlengo wa sasa wa siasa za Tanzania zinavyoelekea, Lipumba ndio hivyo dhoruba ya kupotea kisiasa inamchemelea kwa kasi, same kama Mrema, Zitto, kwa hiyo anachojitahidi kufanya yeye ni kupinga tu, chochote kitachosemwa au kufanywa na watu wasio kwenye serikali au CCm yeye ni lazima apinge tu, kwa maneno ua vitendo, mimi sidhani kweli kiongozi wa chama kama CUF, anashindwa kujua ukweli wa nani Fisadi au sio fisadi, itakuwaje kwa watu wale wa kule vijijini ambao upeo wao wa kisiasa ni mdogo.
mimi nadhani hata kama watu kwenye upinzani na CCM inabidi ifikie point vyama vya upinzani vikubaliane kwenye maswala muhimu yenye kugusa wanachi wote na sio kupinga tu ili mradi uonekane na wewe umesema
nguvu ya kupinga upinzani ikifanywa ni ya vyama vyote conclusion ya maana ingefanyika na solution ya maana pia ingekuwepo
Please Lipumba acha hizo siasa za kutumiwa,, mimi nashangaa msomi kama Lipumba anatumiwa na Seif kwenye nguvu ya kuigawa Pemba kutoka Unguja na Tanzania bara, bila kutafakari anachofanya
 
mimi nafikiri kunawatu kama Lipumba inabidi wakae kimya maana watanzania tumekuwa tukiwatengemea kwa miaka mingi sana wabadirishe nchi, walete maendeleo, usawa, wapungunze rushwa lakini they have done nothing, for almost s10 years!!!

nafikiri mkae pembeni na muwapishe watu ambao wanauchu na nchi at least babu Mrema anasimamaga na kusema mauvu ya hawa CCM sasa wewe Babu Limpumba na usomi wako wote what have you challenge in Tanzania kama sio kuleta udini na ubaguzi?

Watazania sio wale wa miaka ya 1980's-1990's ambao tulikuwa tunakubali ujinga.. tumeamka na hatulali mzeee tafuta sehemu nyingine kuwatete hao mafisadi. Kama unaota watu wanawaonea hao marafiki zako kwasababu ya rangi zao waambie waridishe hela zetu alafu wahame nchi ila hatutakaa kimya tunaibiwa na kuendelea kuwa masikini for only few people ambao ukiwataja ohh tunawaonea kwa ajili ya rangi zao..

mbona kunawahindi (asians origional) wengi wanafanya biashara tanzania na hawatajwi?
 
mimi nafikiri kunawatu kama Lipumba inabidi wakae kimya maana watanzania tumekuwa tukiwatengemea kwa miaka mingi sana wabadirishe nchi, walete maendeleo, usawa, wapungunze rushwa lakini they have done nothing, for almost s10 years!!!

nafikiri mkae pembeni na muwapishe watu ambao wanauchu na nchi at least babu Mrema anasimamaga na kusema mauvu ya hawa CCM sasa wewe Babu Limpumba na usomi wako wote what have you challenge in Tanzania kama sio kuleta udini na ubaguzi?

Watazania sio wale wa miaka ya 1980's-1990's ambao tulikuwa tunakubali ujinga.. tumeamka na hatulali mzeee tafuta sehemu nyingine kuwatete hao mafisadi. Kama unaota watu wanawaonea hao marafiki zako kwasababu ya rangi zao waambie waridishe hela zetu alafu wahame nchi ila hatutakaa kimya tunaibiwa na kuendelea kuwa masikini for only few people ambao ukiwataja ohh tunawaonea kwa ajili ya rangi zao..

mbona kunawahindi (asians origional) wengi wanafanya biashara tanzania na hawatajwi?

Kweli mkuu, kama ni suala la rangi, kuna watu wengi sana mfano, Amir Jamal (aliyekuwa waziri katika awamu ya kwanza) na Arnur Kassam (Chancellor was Sokoine University) ambao hawajawahi kutajwa kwamba ni mafisadi na hakuna mtu aliwahi hata kulalamikia uadilifu wao. Hata Prof Shvji ni mmoja wa hao na anaheshimika sana. Binafsi nilitegemea Lipumba aseme kuwa Mengi ameacha wengine ambao angewataja yeye, mfano EL, BWM, Karamagi n.k. Kuvuruga hamasa ya umma dhidi ya ufisadi nao ni ufisadi mwingine. Katika suala la ufisadi na kushughulikia kero ya wananchi Lipumba hana chochote cha kujivunia, afadhali hata Mrema. Ni vema angekaa kimya tu. Mengi amefanya kazi nzuri sana (hata kama yeye ana mapungufu). Kwa sasa tunahitaji watu kuendelea kuanzia pale alipoishia na siyo kuturudisha nyuma.
 
Lipumba angetuambia Mengi alichokosea ni nini...

Na huyo mleta mada nae angekwambia Lipumba alichosema ni nini. Lipumba kama kawaida yake
1) kaeleza kwa kina ni kwa nini Kikwete, na sio Wahindi papa, wenye tatizo hapa,
2) kaanisha kwa undani ni kwa nini Mengi kachagua Wahindi kujikomba kwa Kikwete, na
3) katoa oni lake Mengi alitakiwa afanye nini kama ana hizo info kweli:

“Bwana Mengi kumsifia Rais Kikwete kuwa mpambanaji dhidi ya ufisadi, si ujasiri, bali ni kujipendekeza kwa bei rahisi, kwa kuwa hivi sasa yuko madarakani na akishamaliza kipindi chake na kuachia wadhifa, bila shaka atamponda vilivyo,” alisema Profesa Lipumba.
Kiongozi huyo wa CUF ambaye anakuwa mwanasiasa wa pili mwandamizi kutoa matamshi ya kumpinga Mengi, baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Sophia Simba, kufanya hivyo juzi, alisema kitendo cha Mengi kuwataja watuhumiwa Wahindi watupu,
kinalenga kuwajengea imani wananchi kuwa tatizo la ufisadi Tanzania limeletwa na ‘Wahindi wachache’, jambo ambalo alisema ni la hatari na lenye nia ya kupotosha.

Lipumba, mmoja wa wachumi wanaoheshimika kimataifa, alisema...“Mengi anacheza karata ya ubaguzi wa rangi, kwa kuwa umma wa Watanzania utakaposikia majina hayo, unashawishika kuamini kuwa tatizo la ufisadi Tanzania limeletwa na ‘Wahindi wachache’,
na kwamba hao watano wakikamatwa na kuzuia wengine wasiibuke, watakuwa wamemaliza tatizo la ufisadi nchini. Hii ni dhana potofu, na ni ya hatari sana, hasa ukizingatia kuwa baadhi ya wananchi wengi wana mashaka na uzalendo wa raia wenye asili ya Kiasia,” alisema Profesa Lipumba.

Alisema kauli ya Mengi haisaidii vita dhidi ya rushwa na kwamba i
nadhoofisha na kupoteza malengo kwa kuwa matatizo ya ufisadi yamesababishwa na udhaifu na ukosefu wa uongozi imara wa rais na kusababisha kuchangia kuenea kwa rushwa nchini.

“Kauli ya Mengi haisaidii vita dhidi ya rushwa na kwa kweli inaidhoofisha na kupoteza malengo.
Udhaifu na ukosefu wa uongozi imara wa Rais Kikwete ndiyo unaochangia kuendelea kwa rushwa,” alisema Lipumba kwa kujiamini.Akitoa mifano, Lipumba alisema, iwapo Kikwete asingekuwa dhaifu, angeweza kuingilia suala la ufisadi wa EPA Agosti mwaka 2006 wakati wakaguzi wa mahesabu ya Benki Kuu, Kampuni ya Delloitte & Touch walipoibua na kutoa ushahidi kuwa Kampuni ya Kagoda Agriculture ilichota kiasi cha dola milioni 30 kwa nyaraka za kughushi.

Alisema pia kwamba, iwapo Kikwete angekuwa imara, basi angeifanyia kazi taarifa ya taasisi ya Uingereza inayochunguza ufisadi mkubwa ya SFI, ambayo katika taarifa yake ya Machi mwaka jana iliwataja kwa majina maofisa wawili wa ngazi za juu serikalini waliohusika katika kashfa ya rushwa inayohusu ununuzi wa rada ya bei ya juu ya dola milioni 40 mwaka 1999.
Awali Lipumba alisema
kitendo cha serikali kuamua kubadili maamuzi ya Baraza la Mawaziri lililotaka kuchukuliwa kwa Kampuni ya CDC Globeleq, kwa ajili ya kazi ya kufua umeme wa dharura na kuipa kazi Richmond, hakiwezi kuwa kilifanywa na (aliyekuwa) Waziri Mkuu (Edward Lowassa) na (aliyekuwa) Waziri wa Nishati na Madini pasipo rais kuafiki uamuzi huo.

“Mengi anatumia vita dhidi ya ufisadi katika kupanda mbegu ya ubaguzi na kwamba
tukipanda mbegu za ubaguzi wa rangi tunaweza kuteleza na kuingia katika ubaguzi wa kidini na kikabila ,” alionya Lipumba.

Alisema
kwa kuwa Mengi ameonyesha kuwa na mahusiano mazuri na rais, ingekuwa ni jambo la busara kwake kuchukua ushahidi alionao kuhusu mafisadi papa hao na kumpelekea rais na TAKUKURU, na iwapo hatua zisingechukuliwa hapo ndipo angeweza kutoa kauli za namna ile alivyofanya.
True to form Professa Lipumba, always detailed and well-reasoned. Sio Simba anasema tu "Mzee kachemka..."
 
Na huyo mleta mada nae angekwambia Lipumba alichosema ni nini. Lipumba kama kawaida yake
1) kaeleza kwa kina ni kwa nini Kikwete, na sio Wahindi papa, wenye tatizo hapa,
2) kaanisha kwa undani ni kwa nini Mengi kachagua Wahindi kujikomba kwa Kikwete, na
3) katoa oni lake Mengi alitakiwa afanye nini kama ana hizo info kweli:

True to form Professa Lipumba, always detailed and well-reasoned. Sio Simba anasema tu "Mzee kachemka..."

Mkuu

Lipumba anauzi watu kwasababu moja, yeye anasema mengi ajamtaja JK kwasababu anajipendekeza, sasa yeye kama mwanasiasa wa opposition party aamuke alipo lala na kusema mafisadi sio kutupa story za kuvunjika kwa muungano na kumfagilia Seif kwa bra bra zake.. at least mengi ameamua kuwa jasiri na kusema. Amemstahadhi raisi maana evidence hana za kusema ndio anawakumbatia mafisadi papa.

Lipumba na viongozi wengine wa upinzani ndio sasa kazi kwao kutoa evidence za kusema raisi anawakumbatia hao mapapa fisadi sio. Na pia miaka yote mpaka nchi inaibiwa matrilion Lipumba alikuwa wapi? anaota au anakula hela na masifadi? Siasa za TZ ni njaa tuu ndugu yangu.

tunaviongozi wachache sana ambao ni wanasiasa wa damu ambao hawafiki 50 na wengi wao utaona hata maisha yao leo hii yanaendana na economy ya nchi yetu sio kama fisadi lowasa au BWM.
 
Jamani, uwe kijana, mtu wa makamo, kikongwe, ajuza ila mradi tu u-mzalendo wa Tanganyika, sasa imefika wakati tuseme IMETOSHA.

Imetosha kwa ufisadi na ubifsi unaofanywa na wa viongozi wetu. Tukiwa na wajibu na dhamana ya kufikiria Tanganyika zaidi ya hii ya leo, hatuna budi kupaza sauti zetu na kuonyesha kwa maneno na vitendo kwamba hatukubaliani na yanayotendeka nchini hivi sasa. Uporaji wa rasilimali za kizazi chetu umefikia hatua mbaya sana na sasa maisha ya wajukuu zetu tayari ni rehani kwa wageni na mapapa wa ufisadi.

Hali hii haipaswi kukubalika hata kidogo. Na si jukumu la watu wachache (Dr. Slaa, Mengi, Kilango, Mwakyembe, Seleli, Sherukindo) kupiga kelele badala yetu. Hata kama baadhi ni wawakilishi wetu, haijalishi wana nguvu kiasi gani, kwa mwendo wa vita hii, na uchache wa askari ni dhahiri karibuni watashindwa. Tukumbuke hakuna ukombozi wa umma (public salvation) na hivyo basi ili kushinda ni lazima kila mmoja awe sehemu ya mapigano.

Tunapaswa kufahamu kwamba watoto wetu na wajukuu wetu hawatawalaani mafisadi kwa ulafi wao, pale ambapo Tanganyika wataikuta, bali hata sisi kwa ukimya wetu.

Ebu tupaze sauti zetu, kila mtu kwa jinsi yake. Tuukatae ufisadi na ulafi unaolitafuna taifa letu. Tushiriki jitihada za kurudisha umiliki wamali, maziwa na asali tuliopewa na MUNGU kwa jamii na si mafisadi. Hatuna hata chembe ya sababu kujitetea mbele za MUNGU kwa nini ndugu zetu, jamaa zetu na marafiki zetu ni maskini wa kutupwa ndani ya nchi hii zaidi ya kukiri udhaifu wa fikra na umoja wetu.

Kwa kuanza katika hatua hii mpya ya mapambano, nashauri wanachama wa Jamii Forums tuache kukaa mbele ya sceen zetu kuhabarishana na watu ambao tayari wengi tuna upeo na tunavifikia vyombo na kupata hata bila kuja hapa.

Hebu nasi kwa mara ya kwanza tujitokeze mbele ya jamii kwa sura zetu halisi kuunga mkono vita iliyoanzishwa na inayoendelezwa na wazalendo wachache wa nchi hii.

Na hebu kampeni yetu iwe tofauti ikiwasha moto toka mkoa mmoja kwenda mwingine maana tuna wanachama karibu kila mkoa. Wale wachache wanaofika hapa kwenye jamvi saidieni kuhamasisha wengi wasiofika.

Na tutoe MATAMKO kupinga ufisadi na kuunga mkono Wapiganaji-Wazalendo kwa nguzu zetu zooote.

Iwapo waraka huu utapata mwitikio chanya, nipo tayari kuhamasisha mkoa mmoja wa kanda ya ziwa na baadhi ya wilaya za Dar es Saalam.

HEBU SASA SOTE TUAMKE NA KUSEMA IMETOSHA, NA TUSEME KWA MOYO NA VITENDO KWAMBA IMETOSHA KWA UFISADI.
 
Mwambieni Mengi ataje wale wengine watano alafu tutamuunga mkono kweli kwa sababu watamtesa sana.

hao wengine watano hana ushahidi wa kujitetea lakini hao aliowataja anao ushahidi na yuko tiyari kwa mahakamani
shida ni kupata ushahidi mtu kama mkapa alikuwa msafi mpaka alipomaliza watu ndio wakapata maovu yake.....
 
whatever happened to presumption of innocence?
If you think you are aggrieved, you have the right to seek redress in a court of law where your innocense or guilt will be proved. GT, waambie hao mafisadi wako kama wana ubavu waende mahakamani. Muulize Rostam mkikutana; kwanini hakumpeleka Slaa mahakamani hadi leo?
 
LIPUMBA kiukweli haeleweki ni aina ya kiongozi gani. Moja ya dhana ya Kiongozi bora ni kujua wajibu wake na jamii nzima kwa wakati ule, ujao, kwa kuzangatia matatizo yaliyopita. Tusitake kuleta siasa uchwara kwenye mambo yanayogusa walipa kodi zaidi ya milioni 45 ambao karibu milioni 42 wanaishi kwa pato la sh. 460 kwa siku(household analysis 2008 aliyoitoa Mkulo),wakati watu 10 wanayumbisha nchi na kumfanya raisi wetu mfano wa URAIS. Angalia alivyoilukia hoja ya MWAKYEMBE kuhusu RA na kumfanya aonekana kama anafanya kamati anayoiongoza yye pamoja na Shalukindo kuwa kichaka cha uhaini. Lipumba apimwe akili , licha ya uhuru wa kuongea na kutoa habari pia ni jukumu la kila mtu kupiga vita maovu ikiwemo kuwataja wahalifu kama hao. TAKUKURU kila siku wanAENDESHA SEMINA KWA kutumia pesa za walipa kodi na Lipumba mhudhuliaji mzuri sana , kila semina wanahimiza kuwa jukumu la kupiga vita maovu katika jamii ikiwemo ufisadi ni la kila mwanajamii Mengi ni mmojawapo.
 
Na huyo mleta mada nae angekwambia Lipumba alichosema ni nini. Lipumba kama kawaida yake
1) kaeleza kwa kina ni kwa nini Kikwete, na sio Wahindi papa, wenye tatizo hapa,
2) kaanisha kwa undani ni kwa nini Mengi kachagua Wahindi kujikomba kwa Kikwete, na
3) katoa oni lake Mengi alitakiwa afanye nini kama ana hizo info kweli:

True to form Professa Lipumba, always detailed and well-reasoned. Sio Simba anasema tu "Mzee kachemka..."

Dilunga, hayo uliyosema sawa mkuu!

Swali. Je, Yeye Lipumba kama Kiongozi wa upinzani amefanya nini kuhusu mafisadi?
 
Ufisadi unatumaliza na ni uadui Mkubwa kwa Nchi yeyote iwe Imeendelea au imo katika Kuendelea kama yetu hii Tanzania.

Kilio cha Ufisadi ndani ya Nchi hii hakikuanzwa leo ni kwa siku Nyingi na Mtu ambae kwa Upande wa Upinzani alieushupalia Kuuanika Ufisadi tokea katika awamu ya Mkapa ni LIPUMBA. Huyu alikuwa yuko mbele kusema, alianzia Ndege ya Rais, Mrahaba, IPTL. SONGAS nk kwa kipindi kirefu akiwa peke yake wakati Huo DJ MBOWE akiwa BILICAN CLUB Akichezesha DISCO habari ya Nchi hakuwa nayo kabisa, lakini Mzee MREMA tumemshuhudia ndani ya Nchi hii akipambana na MAFISADI bila ya Woga na hata kufikia Kufunguliwa kesi kubwa kubwa na kumuandama lakini hakurudi nyuma na alionyesha Njia.

Sasa na tuangalie huyu MENGI ni nani? ni Fisadi aliekubuhu, Mbaguzi, Mdini, Mnafiki ambae Uchafu wake utakapowekwa hadharani kila mtu mwenye akili timamu sio WEHU Watamtemea mate ya uso.Hivi mengi MRAMBA, ANNA MKAPA, KARAMAGI, MKAPA, MZINDAKAYA, NIMROD MKONO, IDDI SIMBA, LOWASSA, SUMAYE, MAHITA, APSON, YONA, CHENGE, MGOJA Hawa kwa nini hakuwataja? au kwa sababu wengi ni WAKWAO na Wengine ni SHEMEGI ZAKEEEEEEEEE.

Ukitaka Kuuwa Nyani usimtizame Usoni
 
Dilunga, hayo uliyosema sawa mkuu!

Swali. Je, Yeye Lipumba kama Kiongozi wa upinzani amefanya nini kuhusu mafisadi?

Hapo ndo ninapo ona kaongea pumba tu, Yeye utendaji sifuri anasubili kushadadia migongo ya wenziwe!

Aanzishe nayeye mdundiko wake tuone unaliaje?
 
Dilunga, hayo uliyosema sawa mkuu!

Swali. Je, Yeye Lipumba kama Kiongozi wa upinzani amefanya nini kuhusu mafisadi?


Very good question. Maana mimi sielewi yeye kama mkeleketwa wa siasa na msomi hajui nchi imetawaliwa na rushwa na wizi wa mali za wananchi? amefanya nini so far? Please can someone tell us
 
Mawazo ya lipumba ni chakavu....nashangaa hata wana CUF wanamuamini nini.....Lipumba kwa nafasi yake ilibidi awe mstari wa mbele kulaani wanyonya uchumi wetu..a.k.a mafisadi...lakini yeye amekuwa kiongozi wa majukwaani..anafrahi kushikana mikono na viongozi mbalimbali wanaotembelea nchi yetu....
 
Back
Top Bottom