Mwita Waitara: Apigilia msumari umeya Ubungo, asema Boniface Jacob siyo Meya tena

Libya

JF-Expert Member
Nov 11, 2016
783
1,918

Sent using Jamii Forums mobile app

Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mwita Waitara amesema kwa mujibu wa Barua iliyodaiwa kuwa ni ya Chadema iliyoandikwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo na kueleza kuwa chama hicho kimemfuta uanachama Boniface Jacob, tayari amepoteza sifa za kuwa Diwani na Meya.

"Nimeiona barua ya Chadema, nimeona barua aliyowajibu Mkurugenzi wa Manispaa, nimesikia sauti ya Mnyika akizungumzia suala hilo, niseme tu kwamba si kazi ya Mkurugenzi kusoma na kuelewa katiba ya Chadema inasemaje, ameshapokea barua ya Chadema na akawajibu kwa maandishi kuridhia maamuzi yao, ameshamaliza kazi yake, wala wasitegemee ataandika batua ya kukanusha, hivyo Jacob si meya tena wa Ubungo.

Kama anaona haikuwa halali aandike barua kwa waziri mwenye dhamana kuomba marejeo, waziri atapitia na kutoa majibu au aende mahakamani," amesema Waitara.
---

"Nimeona Chadema ikikanusha barua aliyoandikiwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo kwamba kwa mujibu wa Katiba yao Meya hawezi kuvuliwa uanachama na ngazi ya Kata.

Nimesoma mitandaoni kwamba Mkurugenzi amekiri kupokea barua hiyo kimakosa na ataandika kutengua barua yake. Mimi kama Naibu Waziri TAMISEMI natoa maelekezo kwamba si kazi ya Mkurugenzi kutafsiri Katiba ya Chadema inasemaje.

Kama alipokea barua kutoka ofisi ya kata, haikua kazi yake kuchunguza kama Jacob anaweza kuvuliwa uwanachama na ngazi ya kata ama lah. Kwahiyo Mkurugenzi hana sababu ya kuifuta barua yake. Yeye ameshafanya kazi yake imetosha, hivyo Jacob sio Meya tena wa Ubungo"

Mwita Waitara, Naibu Waziri TAMISEMI
05/05/2020,
 
Yaani kuna watu walizaliwa kabisa ili kulitumbukiza Taifa kwenye visasi na chuki. Hawakuletwa kwa jambo lolote lingine. Sijui ndani ya mioyo yao wanawaza nini sijui.

Waitara, siku moja jifungie chumbanii peke yako tafakari sana maneno na maamuzi yako. Kaa kimya hata saa nzima ukiwa peke yako kabisa chambua madhara unayoweza/unayotaka kulitumbukiza Taifa wewe as a person.

Unavuruga huko ccm ulikoenda, unavurga Taifa, hebu jiulize dhamira ya wewe kuzaliwa Tanzania alafu muombe Mungu wako yoyote unaemuamini akupe wepesi.
 
Back
Top Bottom