Jacob Boniface: Kura yangu ya Mwenyekiti nitampigia Mbowe na mimi nitagombea Ubunge Ubungo 2025!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,036
142,106
Meya mstaafu wa Ubungo mh Jacob Boniface amesema kwenye Uchaguzi wa Chadema kura yake kwa nafasi ya Mwenyekiti Taifa atampa mwenyekiti wa sasa mh Freeman Mbowe

Bonny amesema yeye atagombea Ubunge

Chanzo: Star tv Medani za Siasa

My take; Huyu Bonny hajui Mbowe anang'atuka!
 
Mmh..

Inawezekana ndio maana sisikii tena habari za Mbowe kujiuzulu mwaka huu, naanza kuona ubaya wa maridhiano kufanyikia chumbani kati ya watu wawili.

Mbowe atabaki Chadema kwa kigezo cha kuendelea na maridhiano aliyoanzisha na Samia, wakati huo Chadema wakiendelea kuwa wapole kwa serikali..

Huku wakina Boniyai, Lema, Sugu na wengine wakiendelea kuwaza ubunge licha ya Katiba Mpya waliyoitaka mwanzo iwepo kutokuwepo mpaka sasa, no wonder hawaililii tena!.

Mpaka kufikia hapo, kwa wale watakaobahatika kushinda ubunge washinde, ili Samia nae kama akienda kwenye uchaguzi mkuu 2025 asiwe na upinzani mkali, na hiyo ndio itaitwa " a win win situation " kwenye maridhiano yao.
 
Wa vyama vingine wangeongea hivyo wangewasema. Kura si ni siri ya mtu. Sisi nini maana ya kupiga kura. Maana kila mtu akihojiwa hakuna atakayesema simpi Mbowe.

Ndio tatizo la viongozi kutojiamini. Ndio maana akili kama za kina Chacha Wangwe hazikutakiwa Chadema.
Wangapi walitamka hadharani kwamba wanasimama na raisi magufuli?
Wangapi walisema mitano tena?
Wangapi walisema awake asitake?
Kama Huna kumbukumbu usibweke
Unaonekana kikaragosi kisa wamesema chadema
 
Ya ngoswe tumwachie ngoswe .Hata angesema atakuwa akimlamba lamba miguu ni hiari yake na shauri yake. Hoja kuu Kwa Watanganyika na watanzania ni katiba ya Warioba kwenye uchaguzi wa 2025
 
Ni chama cha kidemokrasia, wanachama wanaruhusiwa kuchukua form kugombea Uwenyekiti, si kama mtaa wa saba ambao wao ni watu wa kuidhinisha tu. :D :D
 
Meya mstaafu wa Ubungo mh Jacob Boniface amesema kwenye Uchaguzi wa Chadema kura yake kwa nafasi ya Mwenyekiti Taifa atampa mwenyekiti wa sasa mh Freeman Mbowe

Bonny amesema yeye atagombea Ubunge

Chanzo: Star tv Medani za Siasa

My take; Huyu Bonny hajui Mbowe anang'atuka!
Huyu katumwa kuja kuleta joto ndani ya chadema ,katumwa na kina mbowe
 
2025 CCM wengi watamlilia JPM,yaani mama kule kwenye Urais,atapita,ila kwa wabunge na madiwani,aisee,naona yaani hadi sasa wanaomboleza kifo cha kiongozi wao,hawajipangi kivile.Ngoja tuone.
 
Meya mstaafu wa Ubungo mh Jacob Boniface amesema kwenye Uchaguzi wa Chadema kura yake kwa nafasi ya Mwenyekiti Taifa atampa mwenyekiti wa sasa mh Freeman Mbowe

Bonny amesema yeye atagombea Ubunge

Chanzo: Star tv Medani za Siasa

My take; Huyu Bonny hajui Mbowe anang'atuka!
Kama Mbowe atagombea Tena uwenyekiti nitakaa pembeni Kwenye active politics ila nitaendelea kuwa mwanachama wa Maisha wa CHADEMA. Mbowe must go please, tuache ujinga.
 
Back
Top Bottom