nokwenumuya
JF-Expert Member
- Jun 29, 2019
- 810
- 2,851
Kheri ya Pasaka kwa Watanzania wenzangu.
Kama tunavyojua mwaka huu kuna harakati za Uchaguzi Mkuu na tayari wanasiasa wameanza kuzunguka hapa na pale katika kutafuta kuungwa mkono.
Na kila chama kina taratibu, miiko, makatazo na kanuni katika kuelekea katika uchaguzi huo.
Chama Cha Mapinduzi kilitoa katazo kwa makada wake kujizungusha majimboni kabla ya Wakati na mara kadhaa kupitia Katibu Mkuu na Makamu Mwenyekiti wamekuwa wakisisitiza hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wanaokiuka makatazo hayo.
Lakini kama kawaida sio watoto wote huwa na utii. Wengine hukiuka na kutumia njia za ujanja ujanja.
Moja ya watu waliokumbana na pitapita hiyo ni Mh. Mwita Mwikwabe Waitara, Mbunge wa Ukonga na Naibu Waziri wa TAMISEMI.
Baada ya kujitangaza hadharani kuwa atagombea Ubunge jimbo la Tarime Vijijini hapo January Mosi, 2020, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Ndugu Samwel Keboye alimkemea kwa kufanya hivyo kabla ya wakati na akasema kuwa ataitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Mkoa kujibu tuhuma za kuanza kampeni kabla ya wakati, na mwezi March aliitwa na kuhojiwa.
Sasa katika kundi la WhatsApp la CCM Tarime, Kuna mwanachama alitupia picha ikionyesha taasisi ya Tulia inayomilikiwa na Naibu Spika, Dr. Tulia Ackson ikionyesha matangazo ya mikopo ya Bajaj.
Ndipo Naibu Waziri, Mh. Waitara akahoji ni kwanini Dr. Tulia hajaitwa kamati ya Maadili ili kujibu tuhuma za kuanza kampeni kabla ya wakati? Na akaendelea kuuliza je na Dr. Tulia ataitwa kama na yeye alivyoitwa??
Nimeweka screen shot ya comment ya Naibu Waziri hapa.