Mwita Waitara: Tarime Kuna watu wanapigwa risasi hadharani

Mwita Waitara: Tarime Kuna watu wanapigwa risasi hadharani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,248
Reaction score
15,684
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12 Mkutano wa 11, Kikao cha 26 leo Mei 16, 2023.



WAITARA ADAI KUNA WATU WANAPIGWA RISASI HADHARANI TARIME
Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Mwikwabe Waitara ameuliza hatua za Serikali kuhusu tuhuma za mauaji akidai kati ya Aprili na Mei 2023 kuna mauaji yametokea Mji wa Sirari (Wilaya ya Tarime Mkoani Mara) pamoja na katika kata nyingie 8 ambazo watu wanapigwa risasi hadharani na hakuna hatua zinazochukuliwa hali inayosababisha amani kupotea na hali ya biashara kuyumba

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema “Hali ya usalama Nchini ni imara, matukio yote ya uhalifu yanadhibitiwa, kuhusu suala la Jimbo lake siwezi kumjibu hapa kuwa tukio hili lipo katika hatua gani lakini nimuhakikishie kuwa hakuna sehemu ambayo uhalifu unatokea na Polisi wasichukue hatua."

 
Waitara kwa Sasa ajikite kwenye kutunza akiba ya fedha zake maana siasa zinamshinda kwasasa.
 
Kwa hiyo kosa lake kusema ukweli? Au angepigwa risasi ndugu yako,ungekuja kukebehi?
 
Back
Top Bottom