Mwita Waitara aangua kilio bungeni na kutoka nje

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,666
Mbunge wa Mwita waitara ameangua kilio bungeni na kutoka nje huku akisema majibu ya waziri hayakuwa na maana yoyote, hayakidhi mahitaji.


My take :Tabia ni kama ngozi huyu aliozea akiwa barvicha walikuwa wakikwama wanakimbia nje ya bunge wanakaa kwenye Cafe za bunge wanakula kisha hao bar za mitaa

-----------------------------------------------
WAITARA AONDOKA BUNGENI KWA HASIRA - ALIA TENA.
Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara ametoka nje ya ukumbi wa Bunge huku akivua koti na tai yake baada ya kuonesha kutoridhidhishwa na majibu ya Serikali Bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu Jijini Dodoma leo May 9, 2023.

Mbunge Waitara alitaka kujua lini Wananchi wanaodai fidia katika maeneo ya Mgodi wa Barrick North Mara Komarera, Nyamichele na Murwambe watalipwa na majibu ya Serikali yalisema “Mgodi wa Barrick North Mara ulionesha nia ya kutaka kuchukua baadhi ya maeneo ya Vijiji vya Komarera, Nyamichele na Murwambie ambavyo ni sehemu ya Vijiji vinavyozunguka mgodi huo”

“Baada ya Wananchi wa Vijiji hivyo kupata taarifa ya maeneo yao kuhitajiwa na mgodi wa Barrick North Mara, walianza kuongeza majengo harakaharaka (maarufu kama Tegesha), hali hiyo ilipelekea mgodi huo kuachana na maeneo hayo kwani hayaathiri uendeshaji wa shughuli zao za kila siku”

Baada ya majibu hayo Mbunge Waitara hakuridhishwa hivyo badala ya kuuliza swali la nyongeza kama ulivyo utaratibu alisimama na kuanza kulalamika kutoridhishwa na majibu na kutoka nje ya Bunge.
#ngasatvdodoma
#ngasatv

Mwita arudi chadema ndiko anakoweza
Screenshot_20230509-131054.jpg
 
Mh. Waitara, tunaomba utulivu kidogo, Heche bado yuko katika manunuzi ya viungo vya chakula, hajaingia jikoni kukukaangiza.

Mpaka 2025 Waitara atakuwa anahitaji ulinzi, anaweza akaona kivuli chake akaanza kukitukana anajua kinamfatafata bila sababu.

Atafute dereva wa kumuendesha, vinginevyo anaweza kulivaa scania uso kwa uso akiwa "anaongeleshana" na kichwa chake.

Anaota majitu ya miraba minne yanamkimbiza kimyakimya

#Towards2025.
#Drama
#TheEndofMbelekoZaJPM
 
Mbunge wa Mwita waitara ameangua kilio bungeni na kutoka nje huku akisema majibu ya waziri hayakuwa na maana yoyote, hayakidhi mahitaji.


My take :Tabia ni kama ngozi huyu aliozea akiwa barvicha walikuwa wakikwama wanakimbia nje ya bunge wanakaa kwenye Cafe za bunge wanakula kisha hao bar za mitaa

Mwita arudi chadema ndiko anakoweza View attachment 2615478
Acha upuuzi wewe. Usiseme arudi Chadema Bali awarudishie Chadema Jimbo lao.
 
Back
Top Bottom