Mwisho wa utawala wa Korea kaskazini umekaribia

Mwisho wa utawala wa Korea kaskazini umekaribia

hahahaaa kati ya hao uliowataja hakuna aliewahi kusema ana mpango wa kuwarushia makombora ya nuclear,kama yupo basi anaongea chinichini hajajitokeza hadharan km mwanaume mwenzao kim jong un
iwe iwavyo mimi nakakubali mnooo.
 
Naona sasa propaganda na conspiracy theories zimetawala baina ya Marekani na eneo zima la Peninsula ya Korea. Tangu ile vita ya Korea 1953, baada ya Babu yake Kim Jong Un, aliyekuwa muanzilishi wa taifa la Korea kaskazini ( Kim il Sun), na baadaye mwanae (Kim Jong il) Kuwekuwa na Mvutano wa moja kwa moja baina ya kusin na kaskazini, huku mgogoro huu ukipaliliwa na marekani kupitia propaganda zake kama democracy, human rights, the interview nk....

Baada ya Vita ya pili ya dunia (WWII) Korea iligawanywa na kuwa matafa huru mawilii , huku Marekani wakileta ustaarabu wa kimagharibi eneo la Kusini (USA na washirika wake walikuwa wanawakilisha komandi ya UN) na USSR wakieneza utaarabu wa kijamaa eneo la kaskazini. Baada ya muda mfupi tuu mwaka 1951 Korea mbili zikaingia vitani huku, kusini ikisaidiwa na Marekani na washirika wake zaidi ya nchi 60 na Kaskazini ikisaidiwa na USSR, China na baadhi ya nchi za kijamaa kama Hungary, Mongolia , Czech na Bulgaria..

Matokeo ya vita ikawa Kaskazini wakashinda na kuongeza eneo lao kuvuka 38 parallel. Huu ulikuwa ni moja ya ushindi mkubwa wa USSR dhidi ya USA kipindi cha vita baridi. Na ni moja kati ya vita ambayo USA walishindwa vibaya (vita nyingine ni ile ya Vietnam na wachambuzi wengine pia wanasema mgogoro wa Syria baada ya urusi kuingia) . Rais wa USA wa kipindi hicho (Harry S Truman) akaamua kusema sio vita bali ni "police in action" ili kuficha ukweli wa mambo ingawa walituma vikosi vya kijeshi wala siyo masheriff (police wa majimbo).

Baada ya mwaka 1953 vita iliisha huku USA akipata kuistaarabisha Korea kusini na kufanya mission impossible kwa kuistaarabisha Korea kaskazini. Hakukuwa na mkataba wa amani zaidi ya demilitary demarcation zone (DMZ)kati ya Korea kusini na kaskazini, hii imepelekea mataifa haya mawili kuishi kwa uhasama wa hali ya juu.

Sasa kwa suala la kufanya mazoezi eneo la peninsula ya Korea upande wa kusini ya hiyo DMZ ndiyo inatishia usalama wa upande wa kaskazini (Korea) hivyo Kim Jong Un anaitishia marekani kuwa anajibu kwa kutumia makobora ya nyuklia kuishambulia USA na Korea kusini. Anasema atatumia intercontinental ballistic missiles(ICBM) na cruise missiles ili kulibda utaifa wao dhidi ya uvamizi wa USA na Korea kusini, maana anaamini mazoezi hayo ni uvamizi wa taifa lake na ikumbukwe kuwa USA tayari ameweka mfumo wa kinga ya makombora eneo kusini ya DMZ ili kuilinda korea kusini.

ingawa naweza sema hii hali ya sasa kweli ni mbaya sana na inaweza leta vita kubwa ila tujue kuwa tangu mwaka 1953 hadi sasa hawajawahi pigana zaidi ya vita ya mdomo na viingozi wote wawili wa Korea naweza waita Warmongers. kwanini nawaita hivi? kila siku Korea kusini wanaweka vipaza sauti karibu na mpaka wa Korea kaskazini na kutoa propaganda zao kuwa wanauwezo mkubwa kijeshi na watawavamia Korea kaskazini. tukija upande wa kaskazini nao ni hivyo hi yo kilasiku Kim anatoa propaganda zake Mara wanauwezo mkubwa kijeshi wana A-bomb wana H-Bomb nk..... ila hawapigani. Mara kwa Mara USA anafanya mazoezi ya kijeshi na Korea kusini, na Korea kaskazini anatoa vitisho ila mwisho wasiku wote kimnya.

Siwezi sema kuwa ni propaganda tuu, na kwamba vita haiwezi tokea, bali tutambue kuwa vita haiwezi tokea bila propaganda, maana propaganda inapokomaa basi watu wanaingia vitani. Na ikitokea vita katika eneo la Korea peninsula basi itakuwa vita kubwa maana kuna uhasama wa muda mrefu sana yani tangu WWII na kunauwezekano wa kutumia silaha hatari za kinyuklia na kuhusisha mataifa makubwa ie. Urusi na china upande wa Kaskazini na USA na NATO yake upande wa kusini.

Urusi na china watatoa support kwa Korea kaskazini kwa kuwa eneo la peninsula ya Korea ni muhimu kwa usalama wa hay a mataifa mawili , ni eneo muhimu katika Geopolitics za mataifa haya.

My take: naona hapa kuna conspiracy theories tuu na wanafanya mambo yao kwakujua kile wanachokitaka ili kuandaa mpango mpya wa ulimwengu. Hivi inakuwaje K. kusini na K. kaskazini kuwa na uhasama wakati wana viwanda vya uzalishaji vya pamoja mpakani? sasa vinaendeshwaje? mbali na hayo kuna wakati wanandugu wanavuka mpaka kusalimiana? zaidi sana wanamkakati wa kuungana, na hii inashangaza sana maana wote wanaridhia kuungana.

Mwisho: Naona matatizo na migogoro mingi inatengenezwa na mataifa yenye nguvu. Kipindi cha vita baridi kilibadili geopolitics za wakati ule na pia bado kinaendelea kubadili wakati huu, ingawa USA ndiye anayeshape global geopolitics kwa sasa na anapelekea kuleta machafuko mengi na huku akiendeleza sera za kipindi cha vita baridi ndo maana hata baada ya kusambaratika kwa Warsaw pact ya soviet union yeye hajavunja NATO, na ikiwa NATO ilianzishwa kwa lengo la kulinda mataifa ya magharibi dhidi ya vitisho vya soviet union.
 
watu wakiwa wanapia mabiti kama ya north korea watu ooh marekan anaogopa wewee...ikitokea mtu kashushiwa chapo ooh marekani anajifanya mbabe...maana watu walimsifia ooh saddam hussein ni mtu hatari sana marekan hawez kugusa pale..ila jamaa walivyogawa chapo yakabaki malalamiko oooh hawa marekani wanaonea sana.....sasa msifieni huyo dogo mpen kichwa awarushie hio nuclear yake kwa hao jamaa kama hawajamfanyia carpet bombing
Well said mkuu

Huyu dogo atakuja kuchezea kichapo hatokaa aamini..mi namshangaa sana na mikwara yake..hajaanza leo wala jana kila siku mikwara..watu tunataka kaz tu
 
"i see an "arrow" from there(north korea) and it will affect the whole world"(namnukuu tb joshua
Kwa hayo maneno ya unabii aliyotoa mkesha wa mwaka mpya mwaka huu huoni kuna kitu?
Since northkorea ni taifa la kibabe na lina silaha ambazo mataifa mengi yanaziogopa na pia rais wake dictator Anaamua anavyotaka yeyey hata mabaraza ya usalama yakijitoa kumshauri hashauriki..So akisema ndio ujue shambulizi linafuata tu.Na unadhani marekani ikishambuliwa itatulia tu!!?? ni vita! na itasambaa kwa most of d countries pande za asia na amerika kutokana na assistance watakazopata kila
Mmoja na ubaya wa silaha za nyuklia pia utaongeza athari and possibly it will b the 3world war!! na hiyo itaaffect dunia nzima kiuchumi,kiustawi etc..
kama ni kweli ni unabii kutoka kwenye bible kwamba ni nyakati za mwisho basi yatimie!
Na ukweli tb joshua anaonyeshwa na mungu,hadanganyi.Alishatoa nabii nyingi sana ikiwemo syria,aliwashauri wasijiingize kwenye vita kwani uamuzi utaleta matokeo mabaya,wengi wasio na hatia watakimbilia nchi za ulaya,pia utaathir nchi jirani zinazoizunguka syria...But syria wakaamua walichoona kinafaa na matokeo yameonekana.
So kama tb joshua angeonyeshwa pia wafanye nini ili huyu kim jong asiingie kwenye vita angesema but ukweli hii vita kuna kila dalili haina budi kuja mengineyo yatimie!
Hiv unajua ameanza kusema tangu lin hii mikwara yake? Na mpaka leo hata bom la mkono hajawahi rusha
 
Duh...!! Wapi baraza la usalama UN maana huyu mtu sina imani nae kabsaaa hakawii kufanya kweli
 
Well said mkuu

Huyu dogo atakuja kuchezea kichapo hatokaa aamini..mi namshangaa sana na mikwara yake..hajaanza leo wala jana kila siku mikwara..watu tunataka kaz tu
dogo bhana hivi anafika hata miaka 35?
 
Kim hangekuwa na matatizo kama wangekuwa hawamchokozi,kila siku wanamfanyia mazoezi makubwa ya kijeshi mpakani.
watu wanafanya mazoez kwenye ardhi yao na yeye anaruhusiwa kufanya mazoez na china russia au rafiki yake yeyote,nchi nying sana dunian znafny joint millitary exercise
 
Hiv unajua ameanza kusema tangu lin hii mikwara yake? Na mpaka leo hata bom la mkono hajawahi rusha

Marekani na Korea Kusini wanataka kufana mazoezi ya kijeshi.

Na kila mara wafanyapo hivyo jamaa huwa anachimba biti.

Ndo maana nimesema hakuna jipya katika alilolisema sasa.
 
kwa anaye fatilia history ya hawa rafiki zetu wa zamani si Mara ya kwanza...... awamu ya mwisho walionesha mpaka pentagon na white house zikitunguliwa.... pia alisogeza mpaka makombora baharini wengi mnakumbuka hili.......
Nipishane na wale wanao amini ama wanaohisi kuwa hii familia tawala haipendwi! wanawapenda mno! Babu aliweza kuweka misingi mizuri ya kuwafanya waaminike. Naomba niseme na MSEZA MKULU shahidi hawa jamaa wanaaminiwa na wanapendwa kuliko kitu chochote! Ni Kama dini. Ile itikadi ya kijamaa ya JUCHE inafuata kwa kupendwa zaidi.
Mwusho nipishane na wale wanao hisi hawa jamaa watapigwa kirahisi na marekani. Kwanza Tawala zote zilizopita ziliipa sekta ya kijeshi uzito wa hali ya juu Kama sekta ya kilimo. Jeshi Lao ni Kali Kama siafu! Idadi ya wanajeshi ni kubwa kuliko RAIA na wanambinu na vifaaa. Ujio wa huyu Kijana umeiimarisha nchi kiteknolojia wapo vizuri! mifumo yao ni siri mno! wanaubarozi wa RUSIA tu! Hata tunavyosikia ameua ama amefanya nini ni tetesi tuu ama uzushi wa Korea kusini japo machache yaweza kuwa kweli. Kwakifupi tusubiri kwasababu huyu dogo anajua kuwa tumechoshwa na vitisho tunataka vitendo
 
watu wakiwa wanapia mabiti kama ya north korea watu ooh marekan anaogopa wewee...ikitokea mtu kashushiwa chapo ooh marekani anajifanya mbabe...maana watu walimsifia ooh saddam hussein ni mtu hatari sana marekan hawez kugusa pale..ila jamaa walivyogawa chapo yakabaki malalamiko oooh hawa marekani wanaonea sana.....sasa msifieni huyo dogo mpen kichwa awarushie hio nuclear yake kwa hao jamaa kama hawajamfanyia carpet bombing
Na mmarekan alivyo mshenz kesho utasikia katuma B2 bomber yeye hatakag maneno meng
 
Huyu chalii sijui kwanini bado ulimwengu una muangalia tu kichwa chake kilivyojaa tope siku atashambulia kwa nuclear atafutiwe njama tu angoke ata kwa assassination
Kosa lake ni nini? Mkorea wa Kasikazini anaelalamika ni nani? Kwangu mimi mharifu namba moja duniani ni George Bush baba na mtoto wake
 
watu wanafanya mazoez kwenye ardhi yao na yeye anaruhusiwa kufanya mazoez na china russia au rafiki yake yeyote,nchi nying sana dunian znafny joint millitary exercise
uko nyumbani kwako halafu jirani yako anakuja na marafiki zake nje ya geti lako na kuanza kufanya mazoezi ya kulenga shabaha,utakaa kimya ?
Halafu jirani unamsikia anakusema vibaya kwa watu,"ooh,wanalala na njaa,hawana chakula cha kutosha"etc etc
utabaki mpole ama nawe utajitutumua
 
Na mmarekan alivyo mshenz kesho utasikia katuma B2 bomber yeye hatakag maneno meng
af anaanzaga kama masihara vile,hashtukizagi huwa anatangaza kwanza kwamba tunakupa 48hrs tunakuja kukuvamia so kama nawe unabomba za kutosha ujipangage kabisa,y
kwa anaye fatilia history ya hawa rafiki zetu wa zamani si Mara ya kwanza...... awamu ya mwisho walionesha mpaka pentagon na white house zikitunguliwa.... pia alisogeza mpaka makombora baharini wengi mnakumbuka hili.......
Nipishane na wale wanao amini ama wanaohisi kuwa hii familia tawala haipendwi! wanawapenda mno! Babu aliweza kuweka misingi mizuri ya kuwafanya waaminike. Naomba niseme na MSEZA MKULU shahidi hawa jamaa wanaaminiwa na wanapendwa kuliko kitu chochote! Ni Kama dini. Ile itikadi ya kijamaa ya JUCHE inafuata kwa kupendwa zaidi.
Mwusho nipishane na wale wanao hisi hawa jamaa watapigwa kirahisi na marekani. Kwanza Tawala zote zilizopita ziliipa sekta ya kijeshi uzito wa hali ya juu Kama sekta ya kilimo. Jeshi Lao ni Kali Kama siafu! Idadi ya wanajeshi ni kubwa kuliko RAIA na wanambinu na vifaaa. Ujio wa huyu Kijana umeiimarisha nchi kiteknolojia wapo vizuri! mifumo yao ni siri mno! wanaubarozi wa RUSIA tu! Hata tunavyosikia ameua ama amefanya nini ni tetesi tuu ama uzushi wa Korea kusini japo machache yaweza kuwa kweli. Kwakifupi tusubiri kwasababu huyu dogo anajua kuwa tumechoshwa na vitisho tunataka vitendo
hawez kupigwa kirahisi ila lazima achapike,sema nchi kama china lazima wamtulize dogo maana wanajua akizingua akachapwa basi lazima nchi imezwe na south korea af sasa hii itakua ina negative impact kwa china so china atafnya awezavyo ili pensula iendelee kuwa tulivu tu mikwala iendelee ila wasianzishe vita
 
uko nyumbani kwako halafu jirani yako anakuja na marafiki zake nje ya geti lako na kuanza kufanya mazoezi ya kulenga shabaha,utakaa kimya ?
Halafu jirani unamsikia anakusema vibaya kwa watu,"ooh,wanalala na njaa,hawana chakula cha kutosha"etc etc
utabaki mpole ama nawe utajitutumua
naye afanye kwake,mbon china anfanyaga mazoez kwe pwan ya japan ila japan hajawah lalamika?marekan anafanya mazoez kule black sea lakin russia anawamonitor tu coz hawavunji international laws,sasa yeye aawapige watu nuclear kisa wanafanya mazoez nchini kwao kweli??kweli lazima mtu ajihami ila yule kijana anaongea sana,huwez kuwa rais af unakosa staha vile,alishwah mwambia presida wa south korea ni mpumbavu na kichaa.....wale jamaa wanamatatizo mkuu
 
Back
Top Bottom