Mwisho wa "Per Diem"? - Pinda aungwe mkono

WomenofSubstanc; [COLOR="Red" said:
Serikali ingeangalia ni kwa vipi taasisi nyingine esp. mashirika ya kimataifa wameweza kufanya watumishi wake wahudhurie mikutano, seminar etc bila kulipwa posho yoyote kwa maana ni sehemu ya kazi na ukipokea malipo utachukuliwa hatua za nidhamu ikiwa ni pamoja na kukatwa mshahara.Huu ni utamaduni ambao umeshajengeka serikalini na hata kwenye local NGOs wa kutegemea kulipwa hata kama mafunzo ni kwa manufaa ya mhudhuriaji.Inabidi kubomoa utamaduni huu na hii itawezekana kwa kulipa watu living wages[/COLOR].

Hapa nakubaliana na wewe kabisa, mashirika mengi tu ya kimataifa yana semina na makongamano lakini hawana per diem... kama serikali itaboresha wages kama ulivyosema, hili la kuondoa per diem litawezekana kabisa kwa sababu sasa hivi makongamano yanatumika kama source of income na sio kwa sababu zilizokusudiwa!
 
Hivi watu hawafanyi semina za ndani? Mahali ninapofanya kibarua changu kila wiki (jumatatu) tuna mkutano wa kuwakena sawa na kutathmini mambo yaliyopita n.k halafu kila mwezi tuna "communication meetings" halafu kuna mikutano ambayo watu wa HQ wanakuja kuendesha. Yote hii inafanywa hapa hapa kwenye jengo letu na hakuna cha per-diem wala posho yoyote. Kwa sababu ni sehemu ya kazi zetu.

Sasa sijui ni kwa kiasi gani au tofauti gani ya semina ipo ambayo inafanya semina za ndani zilipiwe per-diems au kutowezekana kwa semina ndani. Ungeniuliza mimi ningesema:

a. Kila ofisi lazima iwe na ukumbi wa kutosha wa mikutano ya ndani.
b. Semina na mikutano ipangwe kufanyika ndani ya wiki na muda wa kazi kwenye eneo husika (hata kwa makundi makundi)
c. Semina hizo hazina malipo yoyote yale.
d. Semina za nje ziwe zimepangwa kwenye kalenda mwaka mmoja kabla na anayeenda ajulikane na kwanini yeye aende (leo hii kwa mfano ATCL imepeleka watu kusoma SA, wakati haina ndege za kurusha!)
e. Lazima kuwe na kipaumbele na kujali matokeo ya semina hizo. Kama mtu ameenda kwenye semina ya kujifunza ziaid jinsi General Accounting Principles zinafanya kazi katika utawala wa kidemokrasia ni matarajio yetu kuwa akirudi tuone mabadiliko; kama hakuna mabadiliko semina ilikuwa ya nini? NI lazima tujifunze kupima matokeo (measuring results). Kama watu wameenda kujifunza kilimo cha kisasa halafu wakarudi na kulima kwa mtindo wa zamani, ile semina imewasaidia nini?

Hizo semina hufanyika nje ya ofisi makusudi ili kuhalalisha ulipaji DSA/Per diem/posho na allowances nyingine.Zikifanyika hapo ofisini hakuna malipo hayo na kusudi la hizo semina siyo kweli kuongeza uelewa au ujuzi bali ni kuongeza kipato (mara nyingi).
 
Hata hizo seminaries zitakazokuwa approved matumizi yake yawekwe bayana kama mtu amepata fedha ambayo matumizi yake hayakuwa direct to the seminaries yalipiwe KODI stahili. Hapa ndo tutaanza vizuri bin haki.
EE bwana unataka tukale wapi? au kwa sababu huna access na vijisenti hivyo?
 
Tatizo ni iyo mishahara yao ya TGS ndo wanaamua kukazia na semina,warsha,tafrija,kongamano.
Big up Pinda ila isije ikawa maneno matupu.
Atleast waanze kuwa wanakaa maofisini
 
Next level eeeeeh...hao ndio wale wale wanapishana huko mawizarani na taasisi za serikali wanaulizana.."jamani hakuna kasemina mahali? Mifuko mitupu!" Sasa muulize ni ya nini anaulizia au ipi hiyo atasema "yoyote tu" tumekaa sana humu ndani! Niliwahi kusikia huwa wanakwenda kwa zamu kuna wakati hata wapika chai waliokaa muda mrefu wanachukuliwa kwenda kuhudumia huko (Morogoro, bagamoyo) ili nao wapate chochote!
 
Hivi watu hawafanyi semina za ndani? Mahali ninapofanya kibarua changu kila wiki (jumatatu) tuna mkutano wa kuwakena sawa na kutathmini mambo yaliyopita n.k halafu kila mwezi tuna "communication meetings" halafu kuna mikutano ambayo watu wa HQ wanakuja kuendesha. Yote hii inafanywa hapa hapa kwenye jengo letu na hakuna cha per-diem wala posho yoyote. Kwa sababu ni sehemu ya kazi zetu.

Sasa sijui ni kwa kiasi gani au tofauti gani ya semina ipo ambayo inafanya semina za ndani zilipiwe per-diems au kutowezekana kwa semina ndani. Ungeniuliza mimi ningesema:

a. Kila ofisi lazima iwe na ukumbi wa kutosha wa mikutano ya ndani.
b. Semina na mikutano ipangwe kufanyika ndani ya wiki na muda wa kazi kwenye eneo husika (hata kwa makundi makundi)
c. Semina hizo hazina malipo yoyote yale.
d. Semina za nje ziwe zimepangwa kwenye kalenda mwaka mmoja kabla na anayeenda ajulikane na kwanini yeye aende (leo hii kwa mfano ATCL imepeleka watu kusoma SA, wakati haina ndege za kurusha!)
e. Lazima kuwe na kipaumbele na kujali matokeo ya semina hizo. Kama mtu ameenda kwenye semina ya kujifunza ziaid jinsi General Accounting Principles zinafanya kazi katika utawala wa kidemokrasia ni matarajio yetu kuwa akirudi tuone mabadiliko; kama hakuna mabadiliko semina ilikuwa ya nini? NI lazima tujifunze kupima matokeo (measuring results). Kama watu wameenda kujifunza kilimo cha kisasa halafu wakarudi na kulima kwa mtindo wa zamani, ile semina imewasaidia nini?

Nilipata kazi serikalini,nikakomplain mbona mshahara ni kidogo? Bosi mkubwa tu akanijibu "bwana mzee ukijumlisha na semina kama tau au nne hivi basi utakuwa mzito zaidi ya unavyotegemea", nikamuuliza mbona kazi yangu haitoi nafasi ya kusafirisafiri kwani nitakuwa peke yangu kituoni? akajibu hiyo haimo serikalini, Basi mie nikawa nimeshindwa na nilipoenda waambia rafiki zangu walio serikalini waliniona mjinga sana kwani wote wanaishi hivyo, Ukweli hapo Pinda kapinduka pwaaaa!!!
 
Next level eeeeeh...hao ndio wale wale wanapishana huko mawizarani na taasisi za serikali wanaulizana.."jamani hakuna kasemina mahali? Mifuko mitupu!" Sasa muulize ni ya nini anaulizia au ipi hiyo atasema "yoyote tu" tumekaa sana humu ndani! Niliwahi kusikia huwa wanakwenda kwa zamu kuna wakati hata wapika chai waliokaa muda mrefu wanachukuliwa kwenda kuhudumia huko (Morogoro, bagamoyo) ili nao wapate chochote!

Hiyo mbona kawaida kabisa....
 
Kwa mtindo huo ripoti hii inamake sense:

DASSU STEPHEN
Daily News; Wednesday,November 19, 2008 @21:15

Iincome poverty at the household level has significantly decreased among Tanzanians over the past six years, Deputy Minister for Finance and Economic Affairs Jeremiah Sumari has said. Sumari quoted recent studies in Dar es Salaam yesterday indicating a significant segment of the local population who could not afford basic needs had gone down to 33.2 per cent - from 35.7 per cent between 2001 and 2007.

The deputy minister was speaking during an official opening of a three-day consultative meeting on a National Strategy for Growth and Reduction of Poverty (NSGRP) and Public Expenditure Review (PER). Mr Sumari also said the studies had also shown that food availability was also rising: some 19 out of 100 people in 2007 were able to cater for their food needs as compared to 16 out of 100 people in 2001.

Local experts also say the Gross Domestic Product (GDP) in the country is reported to have increased from 6.7 to 7.1 per cent within the same period of time. The other sectors which have in recent past witnessed a significant improvement included education, health, tourism, infrastructure and communication, said Mr Sumari.

He reiterated that the government through the 2025 development vision will continue to improve living standards among its people in all aspects of life. Speaking in the same occasion, a representative of development partners, Ambassador Tim Clarke, stressed a need for people's participation and good governance as a requisite in fighting poverty among the grassroots. “It very important to make effective and efficient use of public resources….. Dialogue that includes all key stakeholders is also very important in promoting people’s development and public ownership,” he noted.
 
Back
Top Bottom