Mwisho wa "Per Diem"? - Pinda aungwe mkono | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwisho wa "Per Diem"? - Pinda aungwe mkono

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 18, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 18, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  "Semina, warsha sasa kwa kibali cha ofisi ya Waziri Mkuu
  Na Habel Chidawali,Mpwapwa (Mwananchi)

  Maoni yangu:

  Mambo mengine yanashangaza sana lakini pia yanatuonesha kuwa jinsi "tulivyo". HIvi kabla ya agizo hili hii mikutano, warsha, na semina zilikuwa zinafanywa kwa taratibu gani hadi kusababisha watu kutumia mambo hayo kujitengenezea fedha? Angalau ni hatua muhimu.

  Hata hivyo swali ni jinsi gani serikali itapima mafanikio ya maagizo haya? Vipi kama kila warsha na semina wanayoomba ina lengo zuri, jina zuri na inayohitajika kwa watumishi?

  Ni vizuri kuweka vigezo wazi kabisa vya makongamano, semina na warsha; lakini wakati huo huo kutorudisha maamuzi muhimu kwenye idara na ofisi za sserikali mikononi mwa Waziri Mkuu kwani ni kurudisha ukiritimba usio wa lazima.
   
 2. M

  Mama JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Ilikuwa ikifika mwezi March, April au May seminar, makongamano, retreats and the sorts zinashamiri kila wizara kuhakikisha kuwa fungu la pesa kwenye bajeti linaloelekea kubaki linatumika.

  Miezi hii huwa ni shida sana kupata hotel, mahoteli ya Dar, Bagamoyo, Moro na Kibaha huwa yanajaa kwa ajili ya seminar hizi. Nyingi zilikuwa za Ukimwi na vitu insensitive. Perdiem ya mfanyakazi wa serikali ilikuwa hadi Tshs 65,000 per day. Wengine inakuwa pamoja na full board accomodation. Kongamano linaweza kuwa hata la wiki nzima, kule paradise bagamoyo, au hata pale belinda resort tu. Wafanyakazi wa serikali walizifaidi. Kuna watu walifikia sehemu kuwa mshahara hautumiki kabisaaaa, yaani hizo perdiems ndio zinaendesha maisha ya kila siku.

  Hapa wachumi na wahasibu ndipo walipokuwa wanakula madeal. Ukiomba pesa ya kununua karatasi unaambiwa pesa hakuna, subiri. Lakini pesa ya kongamano haikosekani.

  Hebu na ziondoke.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Nov 18, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  sasa wale mafisadi "wadebewadebe" watakasirika sana..
   
 4. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hizi hela za ukimwi jamani kama ni kufaidisha wachache basi wamefaidi!
   
 5. Kisura

  Kisura JF-Expert Member

  #5
  Nov 18, 2008
  Joined: Jun 21, 2007
  Messages: 363
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hii scrutiny itapunguza unnecessary seminars.

  Nimekuwa nikiongea na wafanyakazi wengi tu wa serikali na resume zao zimejaa listi ya trainings, warsha, semina nyingi na wengine hawajui wafanye nini nazo. Wenyewe wanasema ndio zinazowaweka mjini!

  Nimekuwa nikijaribu kuangalia nature ya semina, often times I have trouble aligning their objectives na kazi ya mhusika. Namna hii, hata wakirudi kazini, nyingi hazileti maendeleo wala hata matokeo yanayoyoweza kuwa measured!

  Time is up!
   
 6. M

  Masatu JF-Expert Member

  #6
  Nov 18, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hii huenda ikamtoa Pinda akaonekana nae yupo
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Nov 18, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nimepata news brief ya Ubalozi wa Marekani wakitangaza kufunguliwa kwa Kliniki huko Mpwapwa kesho. Katika kujipa ujiko taarifa hiyo inasema hivi:

  Kwa maana ya kwamba miaka mitano iliyopita kwa wastani Marekani ilitoa bilioni za kibongo 163. Je unafikiri wanaweza kunotice kutoweka kwa bilioni 133 toka EPA?

  Kumbuka hiki ni kiasi tofauti ya kile kilichotolewa na Rais Bush cha milioni 698USD mapema mwaka huu kupitia Millenium Account Challenge.

  Mimi nadhani hii misaada inaficha wezi wetu! Kwa sababu ukiingia sebuleni ukakuta meza na viti vipo huwezi kujua vilivyokuwepo vimeibiwa na hivyo vilivyoletwa ni awamu ya pili. Kwa vile hatuvimiss viti vilivyokuwepo basi hatujui kuwa tumeshaibiwa! Sitoshangaa kuna sebule ambazo viti vinaibwa kila mwezi na vipya vinaletwa na watu hawaoni tofauti!
   
 8. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #8
  Nov 19, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hata hizo seminaries zitakazokuwa approved matumizi yake yawekwe bayana kama mtu amepata fedha ambayo matumizi yake hayakuwa direct to the seminaries yalipiwe KODI stahili. Hapa ndo tutaanza vizuri bin haki.
   
 9. E

  Endaku's JF-Expert Member

  #9
  Nov 19, 2008
  Joined: May 25, 2007
  Messages: 322
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Semina, warsha sasa kwa kibali cha ofisi ya Waziri Mkuu
  Na Habel Chidawali,Mpwapwa

  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameingia kwenye orodha ya viongozi waliojaribu kupiga vita semina na warsha kwa taasisi za serikali baada ya kuzipiga marufuku kwa kile alichoeleza kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za serikali.


  Tamko kama hilo limeshawahi kutolewa na viongozi kadhaa wa juu wa serikali zilizopita bila ya kuwa na mafanikio, lakini Pinda amekwenda mbali zaidi kwa kuzitaka wizara zitakazotaka kuandaa semina, warsha au kongamano kuomba kibali kutoka ofisi yake.


  Pinda alitoa tamko hilo juzi kwenye viwanja vya Mteteja wilayani Mpwapwa alipokuwa katika ziara ya siku ya tano mkoani Dodoma na akaweka msisitizo zaidi kwa kusema atalisimamia agizo hilo kwa guvu zake zote.


  Alisema kuwa kuanzia sasa hakuna wizara itakayofanya semina au warsha na makongamano bila ya kibali cha ofisi yake. Alisema ofisi yake itatoa kibali baada ya kupata maelezo sahihi kuwa semina au warsha inalenga nini na kwa faida ya nani.


  Pinda alisema kuwa fedha zinazoteketezwa kwenye makongamano, semina na warsha hizo ni nyingi sana kiasi cha kuweza kusaidia katika miradi mingine yenye tija kwa wananchi wa Tanzania.


  Alisema ameshaagiza wizara zote kumpa bajeti zao katika ofisi yake ili

  aweze kuzipitia kabla ya kuruhusu makongamano hayo kufanyika popote na kama ataruhusu basi hiyo itaonekana kuwa ina faida kubwa wa wananchi.


  Waziri Pinda aliendelea kueleza kuwa wizara nyingi hazijampa bajeti zao lakini akabainisha kuwa moja ya wizara iliyompa bajeti yake ilimstua sana kiasi cha kuwaagiza wasaidizi ake waagize bajeti za wizara zoe zinazolenga katika makongamano ili azipitie.


  Alisema bajeti hiyo ya wizara hiyo ambayo hakuitaja ni Sh4 bilioni ambazo alisema hazitoshi kwa shughuli za wilaya kama zingetumika pia kwenye semina, warsha na kongamano zisingetosha na akaamua

  kusimamisha mambo hayo hadi atakapotoa ushauri wake.


  “Unajua serikali yetu ni masikini sana lakini watu wanapanga kujinufaisha kwa kutumia makongamano na semina wao wenyewe. Sijui wakulima wa huku vijijini wanaufaikaje kama si kumuongezea mwenye nacho," alisema Waziri Mkuu na kuongeza:


  "Walipoleta tu mimi niliangalia nikagundua kuwa wanataka kumaliza fedha bure hawa... nikasema NO, haiwezekani kabisa fedha nyingi kiasi hiki kutumika kwa ajli ya vitu vya namna hii wakati walipa kodi hawafaidi na kitu chochote."


  Pinda alisema anafanya mpango wa kuwasiliana na rais ili kumweleza juu ya nia hiyo ya kuzuia mambo hayo na kwamba fedha zilizotengwa kwa ajili ya mambo hayo, zitumike kununulia pembejeo za wakulima ili kuwapunguzia makali ya maisha.


  Wakati huohuo, Waziri Pinda amemuagiza mkuu wa mkoa wa Dodoma kuwa mkali ili aweze kuwazuia madiwani wa mkoa huo wasiende kufanya ziara wanazosema kuwa ni za mafunzo na badala yake alisema wanatakiwa kujifunza wakiwa ndani ya halmashauri zao.


  Alimweleza kuwa ni lazima ufike wakati mkuu huyo wa mkoa akaacha huruma kabisa na kutenda kazi aliyomtuma ili fedha zilizokuwa zikitumika katika ziara za mafunzo hayo, zitumike katika miradi ya maendeleo ya wananchi katika halmashauri zao.

  Source: Mwananchi Tanzania News Paper

  Hivi hizi fedha zingiweza kuanzisha miradi ya maana kabisa Vijijini badala ya washawasha hizi ?
   
 10. L

  Lorah JF-Expert Member

  #10
  Nov 19, 2008
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hili nalo neno ndugu yangu
   
 11. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #11
  Nov 19, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  1.Agizo hili la kuzuia seminar, warsha etc liliwahi kutolewa huko nyuma na Rais Mkapa mwenyewe! je wamefanya tathmini kuona kama lilitekelezeka na kama hapana ni kwanini?

  2. Ukiangalia kwa undani ni kuwa seminar/warsha etc hizi kufanyika kwa kutumia fedha za wafadhili kulingana na maeneo ya support..je kama projects husika zilizoombea fedha zilionyesha fedha hiyo itatumika kwa warsha na siyo kununulia pembejeo itakuwaje?
  Chukulia kwa mfano wizara imepewa fedha na wafadhili kwa ajili ya awareness creation on corruption, au human rights au economic patnerships agreements etc yeye PM ataagiza vipi fedha hiyo ikawanunulie pembejeo wakulima?

  3.Nadhani tatizo la hizi semina ni kubwa na pana zaidi ya hiki tunachofikiria.As long as watumishi wa serikali watalipwa peanuts maagizo kama haya ni rahisi sana kuyajengea hoja na kuya bypass.Kipindi kile agizo la kuzuia semina na warsha lilipotoka, watu wakawa creative wakabadilisha majina na ndipo tukaanza kuona " midahalo" makongamano etc yakiibuka!

  Serikali ingeangalia ni kwa vipi taasisi nyingine esp. mashirika ya kimataifa wameweza kufanya watumishi wake wahudhurie mikutano, seminar etc bila kulipwa posho yoyote kwa maana ni sehemu ya kazi na ukipokea malipo utachukuliwa hatua za nidhamu ikiwa ni pamoja na kukatwa mshahara.Huu ni utamaduni ambao umeshajengeka serikalini na hata kwenye local NGOs wa kutegemea kulipwa hata kama mafunzo ni kwa manufaa ya mhudhuriaji.Inabidi kubomoa utamaduni huu na hii itawezekana kwa kulipa watu living wages.
   
 12. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #12
  Nov 19, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  wajanja husema kama hujui kusoma angalia picha!! Pinda anataka kupindisha akili zetu tu, huo ni ujanja wa kutafuta huruma za wananchi waonekane wanachapa kazi..kwa taarifa tu, SERIKALI HAINA PESA, ndio maana haiwezi kuendesha hivyo alivyokataza...fungueni macho wakuu..
   
 13. W

  WildCard JF-Expert Member

  #13
  Nov 19, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Uvujaji wa mapesa ya serikali una njia nyingi. Hii ya semina, kongamano, elekezi, ... ni ndogo ukilinganisha na safari za NJE na NDANI, maadhimisho ya sherehe za kitaifa, misafara mikubwa ya viongozi wa kitaifa mikoani, manunuzi hewa ya stationery, furniture,..., orodha ni ndefu.
   
 14. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #14
  Nov 19, 2008
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mkuu asante kwa mchango wako,

  Lakini, naona hupo kabisa na hujui kabisa ni nini kinaendelea hapa TZ! Sikubishii kwamba kauli ya Pinda inaweza kuwa ni geresha, kwa maana kwamba akawa hamaanishi anacho kisema, ninachopingana na wewe ni kuwa eti ''SERIKALI HAINA PESA na ndio maana haiwezi kuendesha hivyo alivyokataza'', hivi unaelewa sawasawa hizi kashfa za EPA, Migodi, Richmond,IPTL, RADAR etc, hizo si pesa za serikali zinazoachwa zipotea kwa maksudi? Angalia Rasilimali tulizo nazo na mapato yanayokusanywa na TRA, hivyo vyote havitoshi kuipa uwezo mkubwa wa kifedha serikali ?

  Na kwenye issue ya hayo makongamano etc, aliyekwambia serikali haiwezi kuendesha semina, warsha etc ni nani? Kwa taarifa yako nenda kila wizara au taasisi ya kiserikali, sehemu kubwa ya bajeti yao huelekezwa huko kwenye makongamano, semina, warsha etc. Huko mtu akiishiwa hela mfukoni mwake au akiwa na tatizo nyumbani linalohitaji fedha, kama ni bosi huanzisha safari au shughuli (activity) ili tu apate sababu ya kuchota mihela, mpaka mareceptionists huomba safari......huko watu wanakwambia maisha yao yanategemea, warsha,makongamano,semina, safari etc

  Swali pekee la kujiuliza hapa ni je, moto huo aliouanzisha Mh. Pinda, hautazimwa kiaina? Najua, walio wengi huko wizarani wataupinga mpango huo kwa nguvu zote, na kama watendaji wakuu kama makatibu wa wizara na wakurugenzi hawataunga mkono tamko hilo, litabakia kuwa historia kuwa Pinda naye aliwahi kukataza hili!
   
 15. F2S

  F2S JF-Expert Member

  #15
  Nov 19, 2008
  Joined: Feb 16, 2008
  Messages: 216
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Yap hili ni neno nadhani Pinda anaonekana kukerwa kama ambavyo mwananchi wa kawaida anavyokereka na mambo haya, keep it up boy. Wakati tukiwa chuoni tulikuwa tunasikia kwamba ni heri upate kazi ya mshahara wa laki tatu Serikalini kuliko laki tano katika kampuni binafsi kwa mfano wakuu. Kwa sababu.....

  1. Job security- Hata kama haugongi vitu( hauko competitive -mvivu) hakuna wa kukufukuza kazi no one is responsible.
  2. Career advancement-Serikalini ni easy kusomeshwa hata course ambayo haihusiani na kile unachofanya.
  3. Warsha na mikutano( mambo ya perdiem) - Hapa ndio mshahara wa serikali +perdiem UNAKUWA MKUBWA KULIKO mshahara wa kampuni binafsi
  4. Safari- mambo ya ulaya and the like

  Hivi vitu vyote vinatakiwa kufatiliwa kwa makini na sheria ziwekwe ili kusimamia haya ma warsha, mikutano,makongamano nk. Tunajua magari mazuri, nyumba nzuri , furniture nk wafanyakazi wanazipata kupitia hayo niliyotaja hapo juu na mengineyo mengi ambayo mwananchi wa kawaida hayajui.

  Hebu wana jf tusimkatishe tamaa Pinda tujaribu kumuunga mkono ktk hili na kutoa ushauri wetu hapa jf kuona nini kifanyike na haya mawarsha yaendeshwe vipi kwani nilazima watu waweupdated right. Huwezi jua labda Pinda huwa anapindia jf anawezaokota ushauri hapa.

  Mimi binafsi naunga mkono hoja ya pinda papapa pa papapa pa


  SORY GUYS KAMA KUNA MWENYE WARAKA WA SERIKALI UNAOHUSISHA HAYA MA PERDIEM HEBU AMWAGE HAPA TUONE NAMNA WATU WANAVYOMALIZIA MAJUMBA YAO KWA PERDIEM
   
 16. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #16
  Nov 19, 2008
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  LOL. Unafikiri wangefanya tathmini wakati wenyewe waliingia na gia ya Semina Elekezi. Na kule kwenye semina elekezi watu walikula mshiko wa nguvu tu
   
 17. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #17
  Nov 19, 2008
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hahah atachemsha mwenyewe... amegusa sehemu nyeti za wengi tusijashangaa kuona kazi haziendi kisa muda hautoshi na utulivu unaotakiwa kufanyakazi fulani (kama unaopatikana tukiwa tunafanya retreats) haupo..... zitarudi tu.

  Hili si suala dogo kama tunavyofikiria seminars, makongamano na warsha ni muhimu sema angejaribu kupunguza matumizi katika vitu hivyo kwa
  1. Kubana idadi ya watu
  2. Kuainisha sehemu za kufanyia ziwe local meaning sio expensive kiasi hicho e.g. badala ya kwenda Paradise basi wafanyie kwenye mojawapo majengo ya serikali au hata Msimbazi Center na vyakula wawe wanakula vya mama lishe na si mabufee kama walivyozoea
  Za Dar zifanyike Dar na si Moro wala Bagamoyo... tatizo litakuja kama wahusika watatakiwa kutoka sehemu mbalimbali za nchi yetu.

  Bado huu ni mchemsho na nafikiri ametumia jazba tu kuamua

  Ni mtazamo wangu tu.
   
 18. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #18
  Nov 19, 2008
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mwanakijiji! Jamani Mwanakijiji, naomba uache kufikiri na badala yake ufahamu kuwa aid thing is killing us silently. Ni kama saratani. Hii ni njia inayo corrupt viongozi na waserikali kuliko njia nyingine yoyote. Tunauza nchi kwa kupitia misaada! Hebu nipe mfano wa nchi moja...au hata jirani yako aliyewahi kuendelea na kubadilisha maisha yake kwa sababu alikuwa anajua kuomba sana misaada? Hakuna!

  Hakuna sustainability katika hili bakuli letu la kuomba omba na vile vile huwezi hata kuwahoji wanapotumia hii misaada kwa vile "wametusaidia kuomba"..kina JK!

  Hapo kumbuka kuna wale wanaotoa hii misaada hebu jiulize wanatutaka nini hasa! Wanafanya hivi ili kupata dhawabu???? Thubutu! Hivi kweli haya si ni yale yale yalifanyika Berlin walipojigawia Africa? Hii Aid Effectiveness si ni plan B kwa vile wapo walioanza kushtuka kuhusu matumizi ya Aid na maswali ya wadanganyika wa "nchi zinazoendelea"..by the way sijuii hata kuendelea hapa kuna maana gani!

  Nchi badala ya kuhakikisha ina wataalamu wanaoweza kuwa creative katika utatuaji changamoto tulizo nazo inatafuta wataalamu wa kuandika proposal za kuomba! Jamani! Pathetic!
   
 19. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #19
  Nov 19, 2008
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,503
  Trophy Points: 280
  Wakuu mambo ya kuishi bongo ndo kutumia bongo hivo

  lakini the bottom line ni kwamba serikalini mshahara wanaotoa wanajua ni mdogo kumwezesha mfanyakazi kutunza familia yake na yeye mwenyewe, kulipa ada, usafiri, kodi ya nyumba etc

  na serikali yenyewe ina kigeu geu. mfano ilipowauzia nyumba, kwa kuwakopesha, ilitegemea watalipa kwa hela gani kama zio mishe mishe hizi za makongamano na semina?

  So kabla PM hajasema hayo, ni bora kwanza waboreshe mishara.

  na ni kweli watu wa serkalini mshahara mdogo lakini maisha yao yapo juu sana kiubora kutokana na hizi nafasi nyingine....
   
 20. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #20
  Nov 19, 2008
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Yes, tufisadi tudogodogo "hawavumi lakini wamo'' ni issue na wataleta upinzani mkubwa sana kwenye tamko hilo!
   
Loading...