Mtanganyika
JF-Expert Member
- Jul 18, 2007
- 1,601
- 964
Mtanganyika,
Mkuu wangu kwa nini tuandikie mate wakati wino tunao...tazama figures za IMF kulingana na madai yako miaka ya Nyerere na Mwinyi.
Bofya HAPA
Mkuu Mkandara, kwanza asante kwa kuleta argument based on the facts na sio fiction. Angalia debt % per GDP wakati wa baba Mwinyi ukicompare na Mwalimu.
Mwinyi alipoingia madarakani alikabidhi serikali kwa IMF and World Bank, Washington consensus became Tanzania government main policy. Tukaanza kugawana viwanda vya serikali, tukawa cheerleader wa free market bila hata kuandaa Urafiki kushindana na mitumba. Tukazima subsidize kwenye kilimo usiku mmoja, wakati USA bado wananua mahindi kwa wakulima wao. Inshort Mzee wenu Mwinyi ndio alitupiga msumali wa kichwa.
Watu wanakumbuka phrase yake moja ya Ruksa, mnasahau aliruhusu mazuri na mabaya.
Gamba,Wapo wanaodai eti mzee Mwinyi siye aliyerudisha Vyama vingi nchini, this is ridiculous, Yeye ndiye aliyekuwa raisi wa nchi wakati ule, angesema hapana liwalo na liwe , wala hakuna mchakato wowote wa vyama vingi ambao ungeendelea nchini. huwezi kumnyang'anya mzee Mwinyi credit ya kurudisha vyama vingi nchini hata kidogo. inawezekana kweli Idea iitolewa na IMF au World Bank au hata Taifa lolote kubwa, lakini kitendo cha kukubali wazo zuri na kulifanyia kazi ni kitendo cha busara.
Mpaka mwaka 1985 Ujamaa ulikuwa umeshashindwa, sasa ingekuwa jambo la ajabu kuendelea na sera zile zile wakati dunia nzima ilikuwa inabadirika kufuata ubepari na sera za soko huria.
Halafu kingine cha kushangaza wengine wanadiriki hata yale mazuri ya Mwinyi credit kumpa Nyerere, eti kama Si Nyerere kupigia debe vyama vingi visingerudishwa, mbona yeye alivifuta at the first place?.
Mwinyi angesema NO!, na kuamua kufa na tai shingoni kingefanyika kitu?
So far, nadhani Mzee Mwinyi is one of the Great presidents our country has ever had, or will ever have
Mkuu hata sielewi argument hapa. Debt % per GDP ya Mwinyi ilikuwa juu, inflation na karibu kila kitu ukiangalia wakati wake ndio tulikuwa vibaya zaidi lakini huu ndio undani wa uchumi kulingana na data hali wananchi walifurahia zaidi ruksa ambayo iliwapa uwezo wa kuiba mali zao wenyewe.
Gamba,
Ni kweli Mwinyi alikuwa rais wakati wa mfumo wa vyama vingi kuanzishwa. Lakini yeye alitaka Tanzania iendelee na chama kimoja baada ya maoni ya raia kuonyesha kuwa 80% walitaka kuendelea na mfumo huo. Nyerere akawatahadharisha kuwa wakichagua kuendelea na chama kimoja wataganda nacho na madhara yake ni makubwa zaidi kuliko kuachia vyama vingi. In theory Mwinyi was opposed but yes, the multiparty was established under his rule. PS. Hotuba zote za Nyerere na Mwinyi on multiparty unaweza kuzipata pale TBC.
Mkuu wangu, nilisoma hapa hapa JF jinsi Mwinyi alivyomtumia watu wa Usalama Nyerere kule Butiama wakiulizia kwa nini Nyerere anawaunga mkono Mrema na Seif Sharrif kuanzisha Upinzani. Na Nyerere akatishia kurudisha kadi ya chama ikiwa limewagusa akisema CCM sio mama yake mzazi. Sasa la kujiuliza kwa nini Mwinyi hakuwa mwepesi kukubali upinzani hata akawa na balls za kutaka kumpinga mwalimu - Yasome ya Sikonge vizuri!Jasusi:
Wakati wa mwanzo wa vuguvugu la vyama vingi, Mwinyi hakuzungumza sana ni mfumo gani ufuatwe. Watu wengi walitaka chama kimoja lakini yeye alifuata ya Nyerere alivyofanya 1965. Alianzisha tume na kufuata maoni ya tume. Wala hakujiingiza sana kwenye mijadala ya vyama.
Gamba la Nyoka,
Wewe naona umezaliwa miaka ya 80 na haya ya Mwinyi umeyasikia tu au kuyaona ukiwa mdogo. Kuwa na vyama vingi ni NYERERE alilazimisha. Ni Mwinyi huyu alitaka hadi kujiongezea muda kwenye Urais kwa kuvunja katiba na hapo kazee ka Butiama kakaja na kummaliza. Kakasema "nchi haiwezi kuongozwa kwa maamuzi ya Kitandani....." Miaka hiyo Mama Sitti Mwinyi akisema " Gamba la Nyoka uwe au usiwe PM" basi itakuwa hivyo.
Jasusi:
Kipindi Mwinyi anaondoka, Tanzania ilikuwa na hali mbaya sana. Nakumbuka kuna mashine moja muhimu sana male Muhimbili iliyokuwa itumike kumtibu Dada yangu Mpenzi na Mumewe iliharibika. Yes, mwaka mmoja wote walikufa kwa ugonjwa ambao ungeliweza kutibiwa au hata kuwasaidia kuishi miaka kadhaa zaidi. Hili limenifanya NIMCHUKIE Mwinyi hadi kesho na sidhani kuna jambo lolote atafanya ili nimpende. Nilichukia kile KIBAO alinaswa hakikuwa cha Nguvu. Angelirushiwa VIATU kama Iraq na vikampata.........
Ningelikuwa na uwezo wa Kisiasa.................... Mungu asipe uwezo huo.
Na wakati Mwinyi anaachia madaraka nchi ilikuwa imefilisika. Serikali ilikuwa haina uwezo wa kuwalipa wafanyikazi wake mishahara hata wafanyikazi wa Ikulu walikuwa hawajalipwa kwa miezi zaidi ya mitatu. Ndio Mkapa akaanzisha zoezi la ukusanyaji kodi kitu ambacho Mwinyi alikuwa ameacha kabisa kwa kuwapa maswahiba wake wafanyibiashara ruksa ya kutolipa kodi.
Mkuu wangu, nilisoma hapa hapa JF jinsi Mwinyi alivyomtumia watu wa Usalama Nyerere kule Butiama wakiulizia kwa nini Nyerere anawaunga mkono Mrema na Seif Sharrif kuanzisha Upinzani. Na Nyerere akatishia kurudisha kadi ya chama ikiwa limewagusa akisema CCM sio mama yake mzazi. Sasa la kujiuliza kwa nini Mwinyi hakuwa mwepesi kukubali upinzani hata akawa na balls za kutaka kumpinga mwalimu - Yasome ya Sikonge vizuri!
Zakumi,Hapa JF kila mtu ana-source zake. Na sioni mantiki yoyote ya Mwinyi kutuma watu wa Usalama kule Butiama wakati vyama vyenyewe vya upinzani vilikuwa vina watu wa Usalama wa kutosha.
JF kila mtu ana source za kuaminika na kila mtu ana ndugu usalama wa taifa. Tell me hao Usalama walimpeleleza vipi Nyerere?
Mwinyi aliikuta nchi katika hali mbaya sana. Kumbuka wakati Mwinyi anaacha madaraka Watanzania wengi walikuwa katika hali nzuri ya kimaisha. Mwinyi hakukusanya kodi kwa sababu Watanzania wengi walikuwa hawana kipato.
Mwinyi aliweza kuwanufaisha Watanzania wengi kimaisha, kitu kilichomsaidia Mkapa kuweza kukusanya kodi. Foundation aliotuachia Mzee Mwinyi ni muhimu sana kwa taifa letu.
Zakumi,
Walioenda kumwona Mwalimu wakati wa Mwinyi walikuwa mawaziri wawili. Mmoja wa ulinzi na mwingine nadhani wa mambo ya ndani. Katika mazungumzo yao wakamwambia Mwalimu wametumwa na rais kumwuliza kwa nini anaunga mkono kuwepo upinzani. Mwalimu akasema kama huo ndio msimamo wa CCM basi nawarudishia kadi yenu. Waziri wa ulinzi akaruka akasema alikuwa amekuja kuona maendeleo ya nyumba anayojengewa na jeshi. Yakaisha. Hizi habari si ngeni.
Zakumi,Jasusi:
Unaona usemi wako ulivyo tofauti na posti zingine hapo juu. Mwinyi kumuuliza Nyerere kwa kutumia proxy kwanini anaunga mkono upinzani ni tofauti kubwa sana na kusema kuwa Mwinyi alipinga vyama vingi.
Nakumbuka 1987, Nyerere akiwa Zambia alisema mfumo wa chama kimoja haufai. Alipokuja Tanzania alinyamaza. Baadaye walipobanwa akafafanua kwa kusema kuwa mfumo wa chama kimoja hauchangamshi mawazo na hauna check and balance.
Hivyo Nyerere alikuwa convert wa vyama vingi zamani. Na conversion yake ilikuwa ya kuwa vyama viwili vikubwa vyenye ideas za mvutano kama Republican na Democratic. Hakuwa na mpango wa vyama utitiri.
Sikonge:
Sasa unamchukia Mwinyi kwa sababu ya hospitali ya Muhimbili. Tena hospitali yenyewe ni ya serikali. Je huoni kuwa serikali kuendesha hospitali ni kitu kilichodumaza sekta ya afya?
Wakina Doc. Kariuki wangeruhusiwa kufungua hospitali binafsi miaka ya 60, 70 na 80, uwezekano mkubwa ni kuwa mashine unazozitaja zingekuwepo na zingekuwa zinafanya kazi.
Kuiuliza serikali huduma ya afya, ujenzi wa barabara, kutoa elimu wakati hakuna resources za ku-sustain hizo huduma ni kujitakia matatizo.
Zakumi,
' Hii ya Mwinyi kupinga Tanzania kuwa na multiparty mbona imo kwenye hotuba yake ya February 1992 wakati CCM ilipoanza mjadala huo? It was Mwalimu who put the nail in the coffin of one party system and you should have listened to the debate that followed the whole day on Radio Tanzania. You are right that Mwalimu had become a convert of multipartism much earlier after being disappointed by CCM's performance.
Mkandara kakuambia USOME UJUMBE WANGU VIZURI.
Hasira zangu kwa Mwinyi ziko mbili yaani kama alivyo Kikwete, tulimtegemea sana abadili mambo baada ya JKN. Ila yeye akaja akaleta madudu mazito zaidi. Akataka na kubadili Katiba ili atawale zaidi. Kama si yeye, Kikwete asingeliweza kuwa mgombea wa CCM. Kwa sasa ndiye kiongozi pekee mkubwa anayeweza kusema Kikwete STOP, ila ndiyo hivyo JANGALA.
Kuanza kusema hospital za akina Kairuki nk naona kweli wewe au ni dogo (samahani kama una umri wako zaidi ya 25) au umekulia kwenye familia ya wenyenazo. Kipindi kile bado zilikuwepo hospital private ila hawakuwa na mashine kubwa namna hiyo. Yeye kwa cheo chake alikuwa akitibiwa Agha Khan na mumewe akiwa ni Dr Wa Muhimbili Hospital, sasa sijui na yeye angelienda kwa akina Kairuki siyo? Ndiyo maana kwenye kila nchi, baadhi ya huduma inabidi zilipiwe na nchi. Hata Ulaya kwenyewe, huduma kama za Moyo ni Serikali inalipia maana kama ni mtu binafsi basi watashindwa wengi, sasa iweje kwa Tanzania miaka ya 90?
Maisha na pesa walizokuwa nazo, kwa wafanyakazi wa Serikali wakati ule ni wachache sana wangeliweza kulingana nao. Ila hata wao walipiga mahesabu gharama za kwenda nje na bila uhakika wa matokeo, wakaamua tu YAISHE na pesa wawaachie watoto. Private Hospital zilishakuwepo tayari na hao Agha Khan wenyewe ndiyo walim-direct aende Muhimbili maana wao hawana mtambo. Sasa unakuja kusema angelienda kwa akina Kairuki? Mkuu, usiache na wewe nikakuchukia bure kama Jangala wako unayemtetea.