Mwingira atangaza mwisho wa CCM 2015

Tatizo moja la hawa watu wa kiroho wanaparurana wenyewe kwa wenyewe, Yule mzee wa upako ktk mahubiri yake amekuwa akimtusi live huyo mwingira, huku na wengine wakihubiri vile watakavyo wao na si itakavyo biblia

Ninachoamnini ni kuwa ccm ilishajitabiria yenyewe kuwa ukomo ni 2015 wala watz hawahitaji msaada wa Nabii kujua hilo
 
Huyu Mwingira ameshaonesha kwa matendo yake kuwa ni NABII WA UONGO. Mtu mwenye kiburi, roho mbaya na tamaa ya mali hawezi kuwa Nabii wa kweli.

Enyi kizazi cha nyoka ni nani aliyewaambia kuwa mtaepuka laana na hasira ya Mungu? Sijui maneno haya yanatoka katika kitabu gani lakini yapo katika biblia...kwa hiyo wanaofanya maovu kwa wenzao hawataepuka mkono wa Mungu wasipojirekebisha kwa kutubu na kuacha njia zao mbaya. Lakini juu ya nani kuwa nabii wa uongo na nabii wa ukweli mimi naona hakuna tena manabii maana duniani tuna dini kuu mbili ukristo na uislam na kila moja inasema nabii wao ndo alikuwa wa Mwisho. Kwa wakristo wanasema Yohane Mbatizaji ndo nabii wa mwisho na waislam wanasema Mtume Mohamad s.h.w.t ndo nabii wa mwisho. Kama dini hizi zina asili moja kwa watoto wa Ibrahimu na wao wenyewe vitukuu wa Ibrahimu (wayahudi) hawatazamii nabii mwingine ila wanasubiri ujio wa masiha...sasa manabii wengine wanatoka wapii? Watakuwa ni wa uongo tu ila tunaweza labda tukasema wapo watabiri kama utabiri wa hali ya hewa, utabiri utokanao na ndoto n.k lakini si mababii...kipindi cha manabii kimeisha wamebaki watabiri tu maana nabii ni zaidi ya mtabiri...huyu huleta ujumbe wa Mungu kwa watu aliotumwa kwao na si kutabiri tu........!!!!
 
aah ccm mbona ni kama gari lilokatika brake huku linashuka mlima kitonga, bahati mbaya dereva misuri imebana amebakia kakanya mafuta.
sio lzm uwe nabii ujue kifuatacho
 
Kwi Kwi Kwi! Kuna manabii wengi Kama mungu alivyo sema nadhani sio mwisho wa ccm tu itakuwa miisho mingine tehe Tehe


Kipindi Live TRENET: Mtume na Nabii Josephat Mwingira katika mahubiri yake ameeleza kuwa yeye kama mtumishi wa Mungu anatangaza kuwa walioko madarakani mafisadi na wapiga mabomu mwisho wao ni 2015 kama alivyoitabiria KANU ya Kenya...!! ametoa mifano kadhaa ya Biblia kuhusu Shedrack, Meshack na Abednego waliotupiwa kwenye moto lakini hawakuungua. ameeleza kwa ujasiri sana kuwa watawala wa Tanzania wataharibikiwa mambo yao kutokana na maovu wanayowafanyia waTz..!

my take:
naona hz ni hasira za kupigwa mabomu pale kanisani kwake...!
 
Nashangaa kumtabiria marehemu kifo, sijui huu nao ni utabiri wa aina gani? Wao wenyewe ccm wanajua tayari wamekufa sasa sijui utabiri wa nini tena
 
Kipindi Live TRENET: Mtume na Nabii Josephat Mwingira katika mahubiri yake ameeleza kuwa yeye kama mtumishi wa Mungu anatangaza kuwa walioko madarakani mafisadi na wapiga mabomu mwisho wao ni 2015 kama alivyoitabiria KANU ya Kenya...!! ametoa mifano kadhaa ya Biblia kuhusu Shedrack, Meshack na Abednego waliotupiwa kwenye moto lakini hawakuungua. ameeleza kwa ujasiri sana kuwa watawala wa Tanzania wataharibikiwa mambo yao kutokana na maovu wanayowafanyia waTz..!

my take:
naona hz ni hasira za kupigwa mabomu pale kanisani kwake...!



unabii wa huyu bwana Mungu pekee ndio anaujua maana matendo yake mengine hayaendani na utumishi wake. Anyway God knows.
 
kitendo cha waislamu kugomea sensa ni rais wa tz ndiye wa kulaumiwa sababu sheikh ponda ni muumini mwenzake rais na anashindwa kuwachukulia hatua kama alivyofanya kwa mgomo wa madaktari na walimu huu ni uzembe na udhaifu wa kikkwete kama rais anaweka dini mbele kuliko taifa anaamini katika hilo ushahidi upo mwingi.na kama taifa hili litaingia kwenye vita ya kidini kiongozi atakayebeba mzogo huu ni jakaya kikwete.kama angelikuwa ni mchungaji mtikila kasema wakristo wasusie sensa basi manyang'au wa usalama wa taifa na polisi wangeshamuweka ndani mtikila sasa kikwete acha udini na ongoza taifa kwa misingi ya uongozi na si vinginevyo ubaguzi wa kidini utazikwa nao hata ukienda kaburini maan wewe ndie muanzilishi n​a unaendekeza.
 
Kuna nini siku zote hajasikika akikemea maovu yatokanayo na serikali ya CCM? Asijifanye nabii kwani dalili zote za mapungufu ya CCM si siri hata watu wa kawaida kabisa wanayaona. Kama kweli anaitakia Tanzania ustawi wa hakika, awapatie elimu ya uraia waumini wake ili wewe na ufahamu juu ya kupiga kura kuwachagua viongozi waadilifu. Kutabiri tu anguko la CCM hakusaidii. CCM ikianguaka then what next?
 
Wale wanaokunywa mnazi asubuhio badala ya chai?

Hawa watu mi nimeisha wachoka, 2005 walisema JK ni chaguo la Mungu, leo wanasema mwisho wake 2015 so Mungu ataicha CCM? sema kasoma alama za nyakati wala hakuna unabii hapo Picha la CCM karibu linasomeka THE END
 
Huyu Mwingira ameshaonesha kwa matendo yake kuwa ni NABII WA UONGO. Mtu mwenye kiburi, roho mbaya na tamaa ya mali hawezi kuwa Nabii wa kweli.

Mheshimiwa UNABII au UASKOFU siku hizi ni ULAJI. La muhimu uweze kuwachanganya akili watu wenye matatizo kimaisha ili wakufuate na kukulipa ZAKA na SADAKA
 
Time will tell,ila CCM kuanguka haihitaji mtabiri au nabii kutabiri...yote yanaonekana wazi kwa macho makavu.

Uko sahihi mkuu,
Kuanguka kwa ccm 2015 haihitaji kuwa mtumishi wa Mungu uliyebobea. Hata mimi natabiri kwamba 2015 ccm itakuanguka na mgombea wa Chadema atashinda.

 
Back
Top Bottom