Tuhuma za Askofu Josephat Mwingira zimehanikiza umuhimu wa kuundwa haraka kwa Tume ya Ukweli na Maridhiano ya Taifa...

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Kiongozi wa makanisa ya Efatha Ministries Tanzania Nabii, Mtume na Askofu Josephat Mwingira amezua taharuki na mjadala mkubwa ktk vyombo vya habari TV, redio na social media kwa sababu ya mahubiri yake ya Jana Jumapili kanisani kwake.

Baadhi ya watu na wengine viongozi wa serikali kabisa wamedai alichokiongea Askofu Mwingira ni UCHOCHEZI kwa wananchi ili watu waichukie serikali yao!

Wengine wamefika mbali na kuiomba serikali ichukue hatua za kisheria dhidi ya vyombo vya habari i.e redio, TV, magazeti, YouTube channels zilizosaidia kurusha matangazo hayo ikibidi vinyang'anywe leseni, vifungiwe au vionywe.

Haieleweki specific ni kwa kigezo kipi hasa vyombo hivi vifungiwe kwa sababu Askofu Mwingira yupo na kasema hayo kwa uwazi na mchana kweupe mbele ya camera za TV huku dunia nzima ikisikia na kuona.

Hii maana yake ni kuwa, kama kuna mtu ikiwemo serikali yenyewe inahisi madai au tuhuma za Askofu huyu dhidi ya serikali ni za uongo, ni obviously kuwa wanapaswa kutumia njia sahihi za kisheria kumtaka mtu huyu athibitishe.

Na maana yake ni kuwa, kama huyu alisimama hadharani kusema haya, pia anaweza kusimama na kijitetea mwenyewe hadharani.

Maswali ni haya: Kwanza kama ni kweli serikali itafanya mini? Pili, ni kwanini mnataka waadhibiwe wasiohusika?

Kwa maoni yangu, nadhani hoja iwe ni KWELI au SIYO KWELI yaliyosemwa na huyu askofu?

Kwa ufupi sana ni kuwa, ameituhumu serikali ya awamu ya 5 chini ya aliyekuwa Rais Hayati John P. Magufuli kuwa;

1. Kwa kutumia ile "Task Force" chini ya vijana wake maarufu kama "wasiojulikana" ilifanya majaribio ya kumuua mara 3 lakini ikashindwa.

2. Ilifanikiwa kuua baadhi ya watu wake askofu wa karibu sana.

3. Ilikuwa inataka kumfungulia mashitaka mabaya yasiyo na dhamana kwa kuwatumia watu wake wa karibu sana.

4. Ilipora na kuharibu mali zake zenye thamani ya TZS 10bn.

5. Ilifunga biashara zake ikiwemo benki kwa sababu ambazo hazijulikani mpaka leo.

Kwa vipimo vyote, hizi ni tuhuma mbaya kwa serikali inayopaswa kuwa kinara wa kufuata na kusimamia sheria na katiba ili kulinda haki za raia wake. Hii ndiyo sababu kubwa ya taharuki hii.

Hii sasa inanileta kwenye hoja kuu ya mada yangu. Yaani umuhimu wa kuundwa kwa Tume ya Haki na Maridhiano ya Kitaifa (The National Rights & Reconcilition Commission) ili kila mwenye malalamiko ya kutendewa vibaya kwa namna yoyote na serikali ya Rais Mgufuli (marehemu) apeleke malalamiko yake huko na kisha hatua zichukuliwe kwa njia sahihi na za amani ikiwemo kusameheana na kusonga mbele wote kwa pamoja kama taifa.

Labda tutakuwa tumesahau tu. Lakini ukweli ni kwamba, wapo wengi wenye malalamiko na tuhuma kama za Askofu Mwingira.

Walianza kina Freeman Mbowe, Manji, Mo Dewji, Anthony Diallo, Tundu Lissu, Godbless Lema, Joseph Mbilinyi (Sugu), wafanyakazi wa umma, wafanyabiashara nk.

Ya akina Askofu Mwingira yana - hit kwa sbb ni mtu maarufu na ametumia chombo chake cha habari (Trenet TV kama sijakosea)

Na ofcoz baadhi ya viongozi wametaharuki kwa sababu ya namna alivyosema, njia aliyotumia na namna lilivyosambaa, kupokelewa na kupata reaction ya kasi na kubwa kwa jamii.

Sasa Askofu Mwingira anataka kuumiza hata wasiohusika kwa kisingizio cha "UCHOCHEZI" kiasi cha serikali kuanza kufikiri kuvichukulia hatua vyombo vya habari vilivyoichukua habari hiyo, kuiandika, kuitangaza au kuandika kwenye magazeti.

Hii siyo sawa wala haki kwa sababu haitaondoa tatizo bali itaendelea kulifanya kuwa kubwa na complicated zaidi. Iko njia nzuri na salama kushughulika na malalamiko ya watu kama Askofu Mwingira ambao kiukweli wapo wengi maelfu.

Njia hiyo ni kukubali kuwa LIPO TATIZO LA CHUKI NA MGAWANYIKO KATIKA JAMII yetu lililosababishwa na serikali iliyoongozwa na Hayati John P. Magufuli.

Tukishakubali (kutubu na kukiri) kuwa tulikosea na tuna tatizo, kisha tukae chini na kufikiria njia njema ya kurekebisha ili twende mbele wote kwa pamoja kama nchi.

So far, by now, hatuwezi kuzuia watu kusema na kutoa madukuduku yao ya mayoni kuhusu serikali yao kwa namna yoyote na kwa njia zozote wanazoona wao zinafaa bila kuvunja sheria. Bishop Mwingira hajavunja sheria yoyote kusema makosa ya serikali ya Magufuli.

Jambo la muhimu ni kuwa, watu hao wahakikishe kuwa madai au malalamiko yao au tuhuma zao lazima ingalau ziwe na uthibitisho na siyo propaganda tu au chuki binafsi tu.

Haya yanaweza kufanyika vyema iwapo tu, sisi wote kama taifa tutakuwa na UTASHI na NIA safi ktk mioyo na nafsi zetu ya kutengeneza mahusiano yetu.

Kama UTASHI na NIA hii IPO, hakutakuwa na ugumu wa kuundwa kwa TUME YA HAKI NA MARIDHINO YA KITAIFA.

Mungu katika Kristo Yesu awabariki wote mtakaosoma haya. Amina.
 
Hii tabia itaendelea kujitokeza ,watu kutoa shutuma dhidi ya serikali iliyopita .
Kwa ajili ya kujipatia umaarufu .
Ni siasa zisizokuwa na mantiki Kwa taifa..
Tunatakiwa tuwe na siasa za kusema kwel.
Na sio umalaya wa kisiasa
 
Back
Top Bottom