Mwigulu Nchemba wadanganye wasiokujua

Mwigulu Nchemba wadanganye wasiokujua

maelezo kuhusu degree ya pili kuwa hakuPata 1st class hayajajitosheleza, rudi katafute evidence uje upya. Pia ilete CV iliyopo kwenye tofuti ya bunge uweke hapa tuone wapi unaposema kadanganya.. Ulete pia CV ya mbowe na lema
uko kwa Zitto au kwa Mwigulu?
 
Mkuu, nimeshamweleza ktk mchango wangu kuhusu masuala aliyoonyesha kupinga.

mbona unakuwa mbishi kama mbuzi? wewe ni msemaji wa mwigulu? mtoa mada kasema mwigulu hakupata first class kama anavyojitapa wewe unasema alipata basi tuthibitishie siyo unawaya waya kama mlevi wa matapu tapu!
 
Nchi hii tuu ambapo Raisi anachagua watu wasio na moral authority Mwigulu ni muongo toka alivyotoka tumboni kwa mamaye embu aseme jina la mwigulu , na lameck Mkumbo lipi alipewa na wazazi wake ,
 
Neno 1 la kiswahili linalomfaa Mwigulu ni 'LIMBUKENI'.
 
Elimu inaendana na matendo yake, siyo unakuwa na elimu ya vyeti, ukienda field empty, hao akina Mbowe mnaowasema, matendo yao yanatosha kuonesha kuwa ni watu waliosoma wakaelimika, haijalishi ni kwa kiwango gani, ukimchukua Mh Sugu na huyo mnayesema ni mchumi first class Mwigulu, is quite different, ngalia hata michango yao bungeni, heri umpate form 6 pure, kuliko kumpata mwanachuo, Dr au profesor feki.
 
Eti kuishi TANZANIA ni kuona mengi......."DHAIFU + MIZIGO + MWIGULU =??????" WONDERS WILL NEVER END
 
Graduate wa UDSM miaka ya 2000's wengi wadesaji yaani ni degree za kuingia na nyenzo ktk test na kuangaliziana, wapo best student kweli lakini kwa argument za Mheshimiwa kama ni 1st class basi ni zile za kudesa.
 
Kwani aliye mteua naye si anasingiziwa hiyo PHD yake (Ole wale usimwite DR). Kwanini mwigulu naye asiji pachikie ka first class kakusingiziwa..

Nafikiri tatizo lipo kwa mwajiri wake.. Nyerere asinge dhubutu kumweka mwigulu jikoni..


Ila nafikiri kuna agenda ya siri pale wizara ya fedha.. nduru kaaa vizuri, hii team ya vilaza iliyo ingia itakupeleka pabaya...
 
Jk amemfuta kazi naibu waziri wa elimu kwa kufoji, wakati huo huo amempa unaib waziri Mwigulu aliye foji, hii ndo serikali yet dhaifu ilivyo, hapo unategemea nini?
Hivi ilikuaje kwa kihiyo?natamani kwenda mahakamani kumshitaki Huyu mwigulu kama walivyomfanyia kihiyo
 
Wanajamii kwanza niambatanishe Ushahidi wa kauli ya Mh. Nchemba HAPA.
Nasikitika namna Mh. Mwigulu anavyoidanganya jamii, kuna mambo mawili anayoyabainisha.

La kwanza: Kwamba yeye ni mchumi wa daraja la kwanza kwa maana alipata G.P.A. ya kiwango cha first class (4.4-5).
La pili: Kwamba yeye ni alikua mchumi mwandamizi (Senior Economist) wa Benki kuu.

UKWELI NI UPI??

La kwanza.
Kwenye digrii ya kwanza Hakuwahi kupata first class. Mwigulu Nchemba alianza degree ya Uchumi UDSM mwaka 2001 na kumaliza mwaka 2004. Katika darasa lao kulikua na FIRST CLASS MOJA TU! Aliipata Mkenya anayeitwa George Omondi, na alipata 4.4. Mwigulu alipata Upper Second Class na Darasani alikuwa wa kawaida sana, wapo waliokuwa wakimzidi (Mmoja wao alibakizwa kufundisha UDSM).

Kwenye digrii ya pili napo hakuwahi kupata first class.

La pili.
Hakuwahi kuwa mwandamizi wa Benki kuu. Mwigulu alikuwa mwajiriwa wa Benki kuu tawi la Arusha hadi anaondoka. Akiwa Benki kuu HAKUWAHI KUWA MCHUMI MWANDAMIZI. Aliondoka akiwa mchumi wa daraja la kwanza (Ikumbukwe wengi huajiriwa kama wachumi daraja la pili na kupanda hutegemea umri kazini).

Nawasilisha.

Eeeh! Tuambie wewe ulipata daraja gani?
 
Mh! Tanzania kazi bado ngumu sana. Ngoja tuendelee kuwajadili watu.
 
"Dyu-silu", Du! Umenikumbusha mbali sana, niliwatega sana hao ndege kule kwetu. Wana kawaida ya kutengeneza viota kwa kuchimba chini, wanaweka vinyasi na kutaga mayai.
Avanti, kwa comments zako tu inaonesha kuwa, pamoja na kuwatega sana hao dyu-silu hukuwahi kuwahi kwenye mtego hata mara moja, na bahati mbaya inavyoonesha mdogo wako alikuwa akiona umeona kiota cha dyu-silu anaongelea kwenye moto (jikoni) ili kesho usikute mayai/watoto. Nadhan hili nalo litakukumbusha mbali.
 
ImageUploadedByJamiiForums1391088950.015825.jpg
 
Mtatumia mbinu zote za kilaghai kama wanazotumia viongozi wenu kufukuzana ndani ya CHADEMA lakini Mwigulu hachafuki.

Toka lini chura akamzuia tembo kunywa maji?.

68469_210861869116049_1231644896_n.jpg

Mwigulu Nchemba akionyesha kadi ya CHADEMA kwenye mkutano kata ya Sombetini, Arusha baada ya waliokuwa wanachama wa CHADEMA kuhama na kujiunga CCM.

Gonga na usome hapa chini,

https://www.jamiiforums.com/chaguzi...mba-aitikisha-kata-ya-sombetini-arusha-2.html

Vipi safari hii imekuaje hakuja na huu Mtaji huku Sombetini?
DSC06896.JPG
 
Back
Top Bottom