Vipi safari hii imekuaje hakuja na huu Mtaji huku Sombetini?
![]()
Wanajamii kwanza niambatanishe Ushahidi wa kauli ya Mh. Nchemba HAPA.
Nasikitika namna Mh. Mwigulu anavyoidanganya jamii, kuna mambo mawili anayoyabainisha.
La kwanza: Kwamba yeye ni mchumi wa daraja la kwanza kwa maana alipata G.P.A. ya kiwango cha first class (4.4-5).
La pili: Kwamba yeye ni alikua mchumi mwandamizi (Senior Economist) wa Benki kuu.
UKWELI NI UPI??
La kwanza.
Kwenye digrii ya kwanza Hakuwahi kupata first class. Mwigulu Nchemba alianza degree ya Uchumi UDSM mwaka 2001 na kumaliza mwaka 2004. Katika darasa lao kulikua na FIRST CLASS MOJA TU! Aliipata Mkenya anayeitwa George Omondi, na alipata 4.4. Mwigulu alipata Upper Second Class na Darasani alikuwa wa kawaida sana, wapo waliokuwa wakimzidi (Mmoja wao alibakizwa kufundisha UDSM).
Kwenye digrii ya pili napo hakuwahi kupata first class.
La pili.
Hakuwahi kuwa mwandamizi wa Benki kuu. Mwigulu alikuwa mwajiriwa wa Benki kuu tawi la Arusha hadi anaondoka. Akiwa Benki kuu HAKUWAHI KUWA MCHUMI MWANDAMIZI. Aliondoka akiwa mchumi wa daraja la kwanza (Ikumbukwe wengi huajiriwa kama wachumi daraja la pili na kupanda hutegemea umri kazini).
Nawasilisha.
Umenisemea..! Na ya SUGU iwekwe hapa tuone kama walimaliza form four!

maelezo kuhusu degree ya pili kuwa hakuPata 1st class hayajajitosheleza, rudi katafute evidence uje upya. Pia ilete CV iliyopo kwenye tofuti ya bunge uweke hapa tuone wapi unaposema kadanganya.. Ulete pia CV ya mbowe na lema
hivi amemficha wapi huyu?Vipi safari hii imekuaje hakuja na huu Mtaji huku Sombetini?
![]()
200M ni ndogo? zinaweza kuhudumia ofisi ngapi za chama nchi nzima?Kumbe gharama za chopa ni 200m sasa hawa lumumba watasema nini tena.mchumi wao na naibu wa fedha kadhibitisha,
Kazi kwao mizigo,
M4C Daima
Naibu Katibu mkuu wa CCM na Naibu waziri wa fedha Mwigulu Nchemba Amesema Chama cha mapinduzi (CCM)kinashangazwa na kitendo cha chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)kutumia Helikpota kwenye chaguzi zake huku kikidai kuwa ni mkombozi wa wananchi jambo ambalo ni kujitafutia sifa na umaarufu pekee kwa wananchi.
Posted: 29 Jan 2014 07:44 AM PST
![]()
Naibu Katibu mkuu wa CCM na Naibu waziri wa fedha Mwigulu Nchemba
---
Na Mwandishi wetu, Arusha Chama cha mapinduzi (CCM)kimesema kuwa kinashangazwa na kitendo cha chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema)kutumia Helikpota kwenye chaguzi zake huku kikidai kuwa ni mkombozi wa wananchi jambo ambalo ni kujitafutia sifa na umaarufu pekee kwa wananchi.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu mkuu wa CCM ambaye pia ni Naibu waziri wa fedha Mwigulu Nchemba wakati akifungua rasmi kampeni za udiwani katika kata ya Sombetini . Mwigulu alisema kuwa CCM inashangaa sana Chadema kutumia Helikpota kwenye chaguzi nyingi hapa nchini jambo ambalo wanaonesha wazi kuwa wanatumia gharama kubwa kwa ajili ya kuongeza sifa kwani gharama ambazo zinatumika hadi kumalizika kwa kampeni ni zaidi ya Milioni 200.
Alisema kuwa Gharama ambayo inatumika kwenye uendeshaji wa Helkopta ni gharama ambayo ingeweza kuwasaidia wanachama wao lakini hata matumizi mbalimbali ya chama hicho ambacho bado kinaonekana kukabiliwa na changamoto nyingi sana "wananchi wa kata ya Sombetini napendwa kuwaambia kuwa hata sisi wenyewe huwa tunashangaa sana ujio wa hii Helikopta na ninapenda kusema wazi helikopta hiyo inakuja ili iweze kuwazubaisha ninyi sasa msikubali kudanganywa na helikopta baliangalieni sera za mgombea "aliongeza Mwigulu
Pia aliwataka wananchi kuhakikisha kuwa kamwe hawatumiki kwenye siasa za sifa na ushahbiki kwani siasa hizo wakati mwingine zinasababisha hata vifo vya watu ambao hawana hatia ya kufa ovyo "wananchi mnapswa kujua na kutambua kuwa siasa za sasa zimebadilika sana msikubali kuwa mashabiki wa siasa bali mnatakiwa kuangalia zaidi sera za vyama na mahitaji yenu msije mkachagua kiongozi kwa ushabiki itawagharimu sana kwenye utendaji"aliongeza Mwigulu
Awali Mgombea Udiwani katika kata hiyo ya Sombetini kwa tiketi ya CCM alisema Bw David Mollel alisema kuwa ana mikakati mingi sana ya kuhakikisha kuwa anasaidia kata hiyo endapo kama atapata ridhaa ya kuongoza rasmi kama diwani David alisema kuwa changamoto ambazo atahakikisha kuwa ameweza kuzitatua ni pamoja na urekebishaji wa barabara, uboreshaji wa masoko,kna uimarishaji wa vikundi vya wanawake na jamii kwa ujumla
[HUYU NDIYE NAIBU WAZIRI WA FEDHA ZETU NA NAIBU KATUBU MKUU BARA WA CCM]
TUSAIDIANE KUCHAMBUA HOJA YA MWIGULU MCHEMBA SIJUI ALILENGA KUWAMBIA NINI WANA ARUSHA