Mwigulu Nchemba wadanganye wasiokujua

Mwigulu Nchemba wadanganye wasiokujua

Hivi huyu Mwigulu anajifanya kujisahaulisha eh! Amesahau kwamba atika uchaguzi uliopita mwenyekiti wake wa ccm taifa naye alitumia helikopta mbili? Hizi ndizo siasa za majitaka!
 
Hiyo kichwa mbovu, ndio maana kila mtu alishangaa kusikia ni naibu ya waziri ya fedha! Hiyo mtu ni majanga ingine ya taifa. Aliiba EPA katumwa kukwepua pesa ingine kwaajili ya uchaguzi ijayo! Kwiba tu kijana
 
HAKUNA ADUI anayekupenda wakati anapaMbana na wewe,
Huwezi kuacha kupeleka ujumbe wa ukombozi vijijini halafu unagawa fedha
kwenye matawi utashIndwa

























x
 
ushauri wake huo angeanza kwa kumpa bosi anayesafiri mpaka marekani naujumbe wa watu 30 kukutana na fifty cent.
 
Ila jamaa ana kiburi,yani pamoja na zile 4 sifuri bado karudi tena arusha.......
 
Hivi Garama zinapimwa vipi? kutokea Dar Mpaka Kigoma ni kiasi gani na miji yeto ya karibu! Kwa helikopta ni siku moja Kampeni ya Kighoma nzima. Gharama za Magari, hoteli, Chakula na hii sio kampeni ya siku moja!. Ni sawa na kusema sisi tulio diaspora tutumie Meli kuja Tanzania!!
 
Ndugu wanajf huyu jamaa ni namjua kwahiyo sisemi sana...,ila ana ugonjwa wa kutoa hoja nafikiri.
 
Hivi, hii ya huyu jamaa kuwa naibu waziri halafu kuendelea kuwa naibu katibu mkuu wa CCM imekaaje?

Presidential (political) appointees wanaofanya kazi kwenye executive branch wanaruhusiwa kuendelea kupiga siasa kweli?
 

naibu katibu mkuu wa ccm na naibu waziri wa fedha mwigulu nchemba amesema chama cha mapinduzi (ccm)kinashangazwa na kitendo cha chama cha demokrasia na maendeleo (chadema)kutumia helikpota kwenye chaguzi zake huku kikidai kuwa ni mkombozi wa wananchi jambo ambalo ni kujitafutia sifa na umaarufu pekee kwa wananchi.
posted: 29 jan 2014 07:44 am pst
mwigulu-nchemba11.jpg

naibu katibu mkuu wa ccm na naibu waziri wa fedha mwigulu nchemba
---
na mwandishi wetu, arusha chama cha mapinduzi (ccm)kimesema kuwa kinashangazwa na kitendo cha chama cha demokrasia na maendeleo (chadema)kutumia helikpota kwenye chaguzi zake huku kikidai kuwa ni mkombozi wa wananchi jambo ambalo ni kujitafutia sifa na umaarufu pekee kwa wananchi.

hayo yameelezwa na naibu katibu mkuu wa ccm ambaye pia ni naibu waziri wa fedha mwigulu nchemba wakati akifungua rasmi kampeni za udiwani katika kata ya sombetini . Mwigulu alisema kuwa ccm inashangaa sana chadema kutumia helikpota kwenye chaguzi nyingi hapa nchini jambo ambalo wanaonesha wazi kuwa wanatumia gharama kubwa kwa ajili ya kuongeza sifa kwani gharama ambazo zinatumika hadi kumalizika kwa kampeni ni zaidi ya milioni 200.

alisema kuwa gharama ambayo inatumika kwenye uendeshaji wa helkopta ni gharama ambayo ingeweza kuwasaidia wanachama wao lakini hata matumizi mbalimbali ya chama hicho ambacho bado kinaonekana kukabiliwa na changamoto nyingi sana “wananchi wa kata ya sombetini napendwa kuwaambia kuwa hata sisi wenyewe huwa tunashangaa sana ujio wa hii helikopta na ninapenda kusema wazi helikopta hiyo inakuja ili iweze kuwazubaisha ninyi sasa msikubali kudanganywa na helikopta baliangalieni sera za mgombea “aliongeza mwigulu

pia aliwataka wananchi kuhakikisha kuwa kamwe hawatumiki kwenye siasa za sifa na ushahbiki kwani siasa hizo wakati mwingine zinasababisha hata vifo vya watu ambao hawana hatia ya kufa ovyo “wananchi mnapswa kujua na kutambua kuwa siasa za sasa zimebadilika sana msikubali kuwa mashabiki wa siasa bali mnatakiwa kuangalia zaidi sera za vyama na mahitaji yenu msije mkachagua kiongozi kwa ushabiki itawagharimu sana kwenye utendaji”aliongeza mwigulu

awali mgombea udiwani katika kata hiyo ya sombetini kwa tiketi ya ccm alisema bw david mollel alisema kuwa ana mikakati mingi sana ya kuhakikisha kuwa anasaidia kata hiyo endapo kama atapata ridhaa ya kuongoza rasmi kama diwani david alisema kuwa changamoto ambazo atahakikisha kuwa ameweza kuzitatua ni pamoja na urekebishaji wa barabara, uboreshaji wa masoko,kna uimarishaji wa vikundi vya wanawake na jamii kwa ujumla

[huyu ndiye naibu waziri wa fedha zetu na naibu katubu mkuu bara wa ccm]

tusaidiane kuchambua hoja ya mwigulu mchemba sijui alilenga kuwambia nini wana arusha



sasa ambacho hakijaeleweka ni nin? Nani asiejua ufsadi wa chadema wa ruzuku na vyeo vya kugawana ni nani...chopa ni ufsadi
 
Hivi kwanini huyu jamaa (Nchemba) huwa anapenda kuongelea habari za vifo? Na maranyingi akiyasema haya then vifo hutokea kweli. Wiki ya kwanza OPD imemalizika bila fujo, ngoja tuone yatakayotokea baada ya hii kauli.
 
Tahila mkubwa huyo, hiyo ndo agenda aliyoona ya msingi? hivi pesa alizogawa kule Igunga anaweza kusema kuwa zilikuwa kiasigani,anakumbuka yule rafikiyake aliyempa milion 30 keshi za bule huku akimwaga zingine kwa watu kama makalatasi, sasa mtima nyongo wanini kwa chama kutumia Helkopta kutoa elimu kwa watu kama si kutaka kuwapumbaza watu ili waone kuwa utumiaji wa Helkopta ni ufisadi kama EPA,Richmond,na sasa Ujangili wa kumaliza Wanyama wetu hasa Tembo unaoongozwa na bosi wake abdulahman Kinana.
 
It is cheaper kutumia helicopter kuliko magari

Hata ccm walitumia helicopter in 2010
 
Ni bora kutumia Tsh 200M katika kuwaelimisha watanzania kujua haki zao kuliko kutumia Tsh 600M kwa safari za Kikwete kwenda Jamaica kubembea.

CCM wanatumia sh ngapi kupelekana India kwenye matibabu ili hali Hospitali zetu hapa nyumbani ni mbovu na hazina dawa?.
 
kuna kimama kina kiherehere kelele mingi mwongozooooo...aaaggggr! huyu jamaa kapinda ..hajali!! ila ndo inavyofaa kuishi na wabongo wa jk
 
Back
Top Bottom