Mwigulu Nchemba, umelidanganya taifa?

Mwigulu Nchemba, umelidanganya taifa?

Wacha abebe hilo zege ila swala la urais asahau. maana hatumchaguai rais et kwa sababu aliishi maisha ya kubeba zege.
 
Hukumuelewa kwasababu ww ulikuwa bize kutafuta kasoro. Na inaelekea hoja zake zilikukuna na hiyo ndio kasoro pekee uliyoiona kutokana na utashi wako. Hebu rudi uisikilize hotuba yake. Kipindi alichobeba zege ni baada ya kumaliza degree, yaani kabla hajaanza masters na kuwa sponsored na BoT.
hapana, hapana, hapana. alisema baada ya kumaliza degree ya pili!

msikilize kuanzia dakika ya 7:25 anasema wazi kabisa, alipomaliza degree ya pili!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu. Kumbuka mtu muongo huwa hana kumbukumbu ya kile alichodanganya hata kama ingekuwa ndani ya dakika 10 lazima asahau alichokisema maana ni uongo. Hiyo ni sifa mojawapo ya mtu muongo.

Mwigulu ni tapeli la kisiasa. Amesahau kuwa tunajua alifeli darasa la saba na badala yake akanunua jina la mtu aliyekuwa amefaulu aitwaye Mwigulu.

Kuna watanzania wengi sana walikosa fursa za kusoma kwa kigezo hicho ulichokitaja "...alifeli darasa la Saba.."

Kuna vipaji na vipawa vingi sana vilipotelea mitaani na vijijini kwa kigezo hicho cha kufeli darasa la Saba!!!

Kuna watu tumesoma nao enzi hizo walikuwa na uwezo mkubwa sana darasani na nje ya darasa lkn "...walifeli darasa la Saba.."

Nnasikitika unajiona wewe uko salama huku kaka, dada, wajomba, shangazi, marafiki nk wakihangaika mitaani huku wewe ukiwa umeridhika kwavile "... Walifeli darasa la Saba.."

Unatamani na Mwigulu na watu wote waliorudia shule ili walau watoke kimaisha wangezama hukohuko topeni!!

#Rohombaya inaliangamiza taifa
 
Mkuu. Kumbuka mtu muongo huwa hana kumbukumbu ya kile alichodanganya hata kama ingekuwa ndani ya dakika 10 lazima asahau alichokisema maana ni uongo. Hiyo ni sifa mojawapo ya mtu muongo.

Mwigulu ni tapeli la kisiasa. Amesahau kuwa tunajua alifeli darasa la saba na badala yake akanunua jina la mtu aliyekuwa amefaulu aitwaye Mwigulu.
Hakuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari mkuu, those days wale tuliochaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari kwenye shule za serikali tuliaminishwa kwamba tumefaulu kumbe kuna vichwa vingi vilikuwa vimeachwa kutokana na uchache wa shule na hasa wa vijijin ili uchaguliwe ulihitaji maksi za juu sana kwa kuwa suruhisho pekee lilikuwa ni shule za boarding lakini wazee wa day ilikuwa kiaina tu unafaulu unachaguliwa.

Kama alivyosema Mr. Django ni ukosefu wa fursa
 
Last edited by a moderator:
wacha abebe hilo zege ila swala la urais asahau. maana hatumchaguai rais et kwa sababu aliishi maisha ya kubeba zege.

Hoja kuu siyo kubeba zege,hoja yenyewe hasa ni maisha ya kawaida aliyoyaishi kabla ya kupata ajira BOT,CCM na sasa uwaziri.Siyo siri kwa hali tuliyofikia tunahitaji kiongozi mwenye historia ya maisha kama Mwigulu.

Huyu ndiye anayeelewa namna maisha yalivyo magumu mitaani kiasi kwamba mkimwambia mzee tusaidie jambo hili atawasikiliza.Mmeona athari ya kuongozwa na viongozi waliokulia ktk maisha mazuri kama akina Makamba,

ametuongezea msalaba wa kodi za Sim card na vocha licha ya kelele za raia lkn yeye wala hakujali,hii yote ni kwasababu hakuwahi kupitia maisha ya mitaani na kuona jinsi yalivyo magumu
 
duh! neno jipya, "tapeli la siasa!"

inawezekana kununua jina na hadi kupata first class na heshima aliyonayo-huyo alifaulu kwa akili zake mbona hatuoni alichofanya, chuki za kijinga zinazuia uwezo wa kufikir
 
alichoniacha hoi kuipnda system iliyopo wakati ye mwenyewe yupo kwenye system
 
Usihame kwenye agenda, elewa hoja kabla ya kuchangia. Hoja iliyokuwa inajadiliwa ni: lini alibeba zege wakati CV yake inaonesha alitoka chuo kikuu na kuajiriwa BOT.
Hoja ya kusema alivaa uhusika tu na wala siyo maisha yake halisi aliyoishi ndiyo inayopingwa hapa, kuwa siyo kweli ama ni maisha yake halisi ama ni usanii tu kunogesha mjadala, tujue hilo.

Mambo ya maisha yake binafsi baada ya kuajiriwa hakuna aliyegusia. Hata kama yapo hiyo siyo hoja inayojadiliwa sasa. Kama uliweke utetezi wako kwenye eneo hilo subiri au anzisha uzi, tutachangia kulingana na hoja itakayokuwa mbele yetu TEKNOLOJIA
 
Last edited by a moderator:
ferre.g
Mimi naamini alibeba zege, maana mtu mzima hawaze kudanganya kwa kazi kama hii.

Mm mwenyewe nilishafyatua tofari nikiwa O-Level, Nikauza nyama bucha na Kufundisha tuition. Leo hii nasoma Phd na kazi nzuri nafanya.

Msipende kuendekeza ubishi bila ushahizi nyie watoto wa mafisadi
 
Last edited by a moderator:
maswali ni je alibeba zege?.... Na mkewe akawa Mama ntilie.. Na ni Mtaa upi huo huyu binti alikuwa ntilie?
Eti amekulia mazingira ambayo Dozi Moja ya Dawa wanapewa watoto zaidi ya mmoja!! Hivi ingekuwa ni kweli huyu Bwana angeishi mpaka leo? Malaria Nusu dozi?? Tapeli mkubwa
 
Amebeba hoja nzuri, mtu unapohitimu elimu ya juu (chuo) hupati kazi moja kwa moja, inawezekana ndiyo shughuli aliyoifanya kabla ya kupata nafasi ya kazi BOT
 
Eti amekulia mazingira ambayo Dozi Moja ya Dawa wanapewa watoto zaidi ya mmoja!! Hivi ingekuwa ni kweli huyu Bwana angeishi mpaka leo? Malaria Nusu dozi?? Tapeli mkubwa

Wewe umekulia wapi mbona hayo yapo mimi nimekuwa nikidhani asprin inatibu malaria maana nilikuwa nikiugua nanunuliwa asprin 3 kwa shilingi 10 maisha hayo yapo sema tu Mungu anatulinda.
 
Mkuu wangu Bukyanagandi.

Inaonekana jamaa ana bifu naye maana kusema alibeba zege ndiyo iwe kosa.

Mkuu, ni rahisi sana kuwasoma jamaa hawa - unajua tatizo ni nini? Lameck kawashtua baada ya kuonekana kube aliwahi kutipia suruba za kimasikini za kila sampuri mfano: Mwambie Mwingulu kwamba uliwahi kutembea peku peku mpaka ulipo ingia form one - Lameck atakuelewa, unakula mara moja kwa siku, ulikosa karo, kuishi nyumba za TEMBE, beba zege na matofali, mama ntilie nk yote hayo kapitia - hata ukiangalia wazazi wake ndugu zake mke wake watoto -wote wanaonekana ni watu wa kawaida kabisa - kuna baadhi ya members waliojipanga kumzulia vitu visivyo na kichwa wala miguu.

Mkuu nikwambie kitu, Mwenyezi Mungu alituhumba na instinct za aina fulani za kuweza kutambua mtu ambaye ni mkweli au mwigizaji - mtu mkweli ambaye anajali binadamu wenzake anapozungumza unahisi msisimuko wa aina fulani down your spine - ni binadamu wachache Duniani wenye uwezo wa kuwafanya binadamu wenzake wajione wapo karibu nao kiroho- mfano:

Nyimbo za Michael Jackson, Kambarage, John Fitzgerald Kennedy, Martin Luther King Jr, Chinese leader Ti Xing Ping, JK nk. Jana nimejaribu kuzungumza na wenzangu kuhusu hotuba ya Lameck - wengi wamehisi feelings kama za kwangu - why? Ana kitu cha ziada yule si bure, si rahisi mtu kuteuliwa kwenye uongozi tangu hupo shule ya msingi mpaka Chuo Kikuu na baadae ndani ya Chama na Serikalini - hata hasipo teuliwa katika hawamu ijayo basi kama tuko serious na mstakabali wa Taifa letu basi apewe uwaziri Mkuu na mamlaka kamili ya kuwasimamia MAWAZIRI.
 
Bukyanagandi
Mkuu wangu umeongea kwa hisia sana mawazo yako na yangu hayatofautiani sana.

Ni kweli Mwigulu Nchemba ni tofauti na viongozi wengi hata malezi na makuzi Mwigulu akulelewa maisha ya kufungua hotpots au fridge akisikia nja wala kupelekwa kindergarten na BMW au Benz katoka kwenye thug life Singida.

Ukimsikiliza inajua kabisa jamaa ana kitu cha kuwafanyia Watanzania.

Kiukweli maisha yote anayajua na kilichomfikisha hapo ni kichwa chake siyo mbeleke za mjomba yupo serikalini kapenya mwenyewe Mungu atamsaidia huko mbeleni.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, ni rahisi sana kuwasoma jamaa hawa - unajua tatizo ni nini? Lameck kawashtua baada ya kuonekana kube aliwahi kutipia suruba za kimasikini za kila sampuri mfano: Mwambie Mwingulu kwamba uliwahi kutembea peku peku mpaka ulipo ingia form one - Lameck atakuelewa, unakula mara moja kwa siku, ulikosa karo, kuishi nyumba za TEMBE, beba zege na matofali, mama ntilie nk yote hayo kapitia - hata ukiangalia wazazi wake ndugu zake mke wake watoto -wote wanaonekana ni watu wa kawaida kabisa - kuna baadhi ya members waliojipanga kumzulia vitu visivyo na kichwa wala miguu.

Mkuu nikwambie kitu, Mwenyezi Mungu alituhumba na instinct za aina fulani za kuweza kutambua mtu ambaye ni mkweli au mwigizaji - mtu mkweli ambaye anajali binadamu wenzake anapozungumza unahisi msisimuko wa aina fulani down your spine - ni binadamu wachache Duniani wenye uwezo wa kuwafanya binadamu wenzake wajione wapo karibu nao kiroho- mfano:

Nyimbo za Michael Jackson, Kambarage, John Fitzgerald Kennedy, Martin Luther King Jr, Chinese leader Ti Xing Ping, JK nk. Jana nimejaribu kuzungumza na wenzangu kuhusu hotuba ya Lameck - wengi wamehisi feelings kama za kwangu - why? Ana kitu cha ziada yule si bure, si rahisi mtu kuteuliwa kwenye uongozi tangu hupo shule ya msingi mpaka Chuo Kikuu na baadae ndani ya Chama na Serikalini - hata hasipo teuliwa katika hawamu ijayo basi kama tuko serious na mstakabali wa Taifa letu basi apewe uwaziri Mkuu na mamlaka kamili ya kuwasimamia MAWAZILI.

Uko Sawa mkuu kwa waliopo ndani ya hicho chama ndo chaguo bora na ana nguvu bado na vision nzuri kama hatayumbishwa na wapambe.
 
maswali ni je alibeba zege?.... Na mkewe akawa Mama ntilie.. Na ni Mtaa upi huo huyu binti alikuwa ntilie?

sio lazima abebe yeye anaweza ikawa alipewa kazi kusimamia project kubwa zihusuzo zege...na mama ntilie sio kama wale unaokula ww wa mbagala ...inaweza kuwa mgahawa mkubwa wenye hadhi
 
Usihame kwenye agenda, elewa hoja kabla ya kuchangia. Hoja iliyokuwa inajadiliwa ni: lini alibeba zege wakati CV yake inaonesha alitoka chuo kikuu na kuajiriwa BOT.

Hoja ya kusema alivaa uhusika tu na wala siyo maisha yake halisi aliyoishi ndiyo inayopingwa hapa, kuwa siyo kweli ama ni maisha yake halisi ama ni usanii tu kunogesha mjadala, tujue hilo. Mambo ya maisha yake binafsi baada ya kuajiriwa hakuna aliyegusia.

Hata kama yapo hiyo siyo hoja inayojadiliwa sasa. Kama uliweke utetezi wako kwenye eneo hilo subiri au anzisha uzi, tutachangia kulingana na hoja itakayokuwa mbele yetu.

Duh hii Kali,hivi ulitarajia Mwigulu aweke pia kazi za kubeba zege ktk CV yake?are you serious?
 
Hata Maccm yaongee vipi yanajisumbua tu kwa sababu yako kwenye lichama lenye sera zisizozingatia wakati,lenye ufisadi na ulaghai!
 
Duh hii Kali,hivi ulitarajia Mwigulu aweke pia kazi za kubeba zege ktk CV yake?are you serious?
Suala sio kuweka 'kubeba zege' kwenye CV, suala ni kwamba mtu anapopata udhamini wa BoT anaajiriwa hata kabla haja-graduate. nenda pale BoT kuna watu wanafanya kazi huku wanaandika dissertation! na hata kama hatoajiriwa BoT moja-kwa-moja basi UDSM wanamuajiri katika idara husika! hakuna jinsi yoyote Mwigulu Nchemba akose ajira baada ya udhamini wa BoT kwenye 'masters'! labda aje aeleze sababu za msingi za yeye kubeba zege!
 
Back
Top Bottom