Mwigulu Nchemba, umelidanganya taifa?

Mwigulu Nchemba, umelidanganya taifa?

kwa udhamini wa BoT, unaajiriwa punde baada ya kumaliza. au unabaki idarani kwa ajili ya kufundisha! soma uelewe nilichoandika.

Kumaliza masomo na ili utambulike umehitimu elimu fulani kwa ngazi ya chuo lazima ufanye graduation mpewe transcript ambazo zinatumika kama cheti inakuchukua miezi 4 mpaka 5 tokea umalize mtihani wako wa mwisho sasa miezi hiyo utakuwa una kula nini na una familia.
 
Sio ukimaliza masomo unaajiriwa papo hapo utakaa kidogo mtaani aidha kusubiri matokeo au taratibu zingine na wakati huo mfadhili hatakuwa anakupa chochote maana tayari umemaliza masomo mfano vyuo vingi humaliza mihula mwezi wa 6 matokeo hutoka mwezi 9 na graduation hufanyika mwezi wa 11 ili angalau mtu apate cheti aweze kuajiriwa hivyo tangu kumaliza mitihani mpaka graduation ni miezi 4 mpaka 5 kwa mtu mwenye familia lazima uchakarike ili mambo yaende sawa.
Udhamini wa BoT; ukimaliza masters haina haja ya kusubiri matokeo ya mwisho, wapo wengi wameajiriwa kwa jinsi hiyo hata kabla hawajamaliza masters. Na pili, kama BoT hawatakuajiri, basi chuo kitaendelea na wewe.
 
Wewe ndo unatakiwa ueleze kama alifanya nini baada ya kumaliza 'Masters'...

Yeye kaeleza anachokiona ni ukweli sasa wewe kama unaona ni uongo ueleze ukweli ukoje....

Sina uhakika kama wewe(kama unafanya kazi) mara tu baada ya kumaliza masomo yako moja kwa moja ulianza kazi pasipo kusubiri mtaani...
Mkuu, karibu sana jukwaani.

Vitu vingine ni common sense tu.............mtu mweledi, mtu aliyetoka kwenyefamilia masikini, anaejua mzigo wa umasikini wake na umasikini wa wzazi na ndugu zake; ilikuaje akaoa akiwa shule? alitoa wapi fedha za kuanza kuwa na mwenza?

Au
Eti mkeo akawa mama lishe na wewe ukawa mbeba zege!
hakuwa mke bali mchumba au kuoa ilikuwa kipaumbele chake?
 
Ukimaliza masomo unaajiriwa papo hapo?
Ukimaliza masters haina haja ya kusubiri matokeo ya mwisho, wapo wengi wameajiriwa kwa jinsi hiyo hata kabla hawajamaliza masters. na pili kama BoT hawatakuajiri basi chuo kitaendelea na wewe.
 
Wacha hizo, Mwigulu alikuwa anazungumza na watu wa kawaida sana, wenye uwelewa wa kawaida na hata pengine wenye uwelewa wa chini. Hawa ndiyo walio wengi na ndiyo wapiga kura.

Swala kujidai umeelwa tofauti na hali ya kawaida ni kupotosha mada. Yeye kasema anajizungumzia yeye hali halisi ilivyokuwa, wewe unaleta fasihi za kuigiza ati kavaa taswira ya uhusika ambayo tunaikuta kwenye tamthiliya.

Kwa akili yako unadhani unamsaidia kumbe unamharibia zaidi. Watu wakijua kuwa hajaishi maisha anayoyasema wataona kumbe ni msanii. Ni afadhali madhara ya kukosea kauli kuliko kuvaa vazi la usanii. Msanii kwa maana nyingine ni mwongo kama vile maisha bora kwa kila mtanzania, nguvu mpya, ari mpya, kasi mpya.

Watanzania wakadhani ni nguvu mpya ,ari mpya na kasi mpya kwenda mbele, kumbe ilikuwa ni nguvu mpya, ari mpya na kasi mpya kurudi nyuma.Tumerudi nyuma maili 20 toka tulipokuwa kabla ya yeye kuingia madarakani. Maisha bora kwa kila mtazania sio maisha bora kwa watanzania wote kumbe ni maisha bora kwa kila mtanzania mteule tu.

Hii ndiyo kazi ya wasanii, kucheza na maneno.
Of course nyinyi mliokulia ktk familia za kifisadi hamuwezi kumwelewa Mwigulu uzoefu aliouzungumzia,ila wale waliokulia ktk familia za kikabwela ndiyo waliomwelewa zaidi.Mwigulu was talking to ordinary Tanzanians, his world view about Tanzanian economic development resonates well with ordinary/middle class tanzanians views.
 
Unataka kujua kabeba zege kwa muda gani au kibeba zege tu? Inawezekana ametumia neno zege kama tafsida akimaanisha alisota kupata ajira. Hata hivyo, tunataka utoe challenge kwa vitu tangible ili tuone una uwezo wa kuishawishi hadhira kama great thinker.
 
Kumaliza masomo na ili utambulike umehitimu elimu fulani kwa ngazi ya chuo lazima ufanye graduation mpewe transcript ambazo zinatumika kama cheti inakuchukua miezi 4 mpaka 5 tokea umalize mtihani wako wa mwisho sasa miezi hiyo utakuwa una kula nini na una familia.
Wacha kubisha usilolijua. watu wanaosomeshwa na BoT wapo pale 'twin towers' hata kabla hawajamaliza dissertation/thesis, graduation. ninaongea kutokana na uzoefu! hawawezi kukuacha ukabebe zege
 
Unataka kujua kabeba zege kwa muda gani au kibeba zege tu? Inawezekana ametumia neno zege kama tafsida akimaanisha alisota kupata ajira. Hata hivyo, tunataka utoe challenge kwa vitu tangible ili tuone una uwezo wa kuishawishi hadhira kama great thinker.
Hakutumia kama tafsida, alisema wazi-wazi! kwa kifupi hajui uchungu wa kutafuta ajira!
 
Hukumuelewa kwasababu wewe ulikuwa bize kutafuta kasoro. Na inaelekea hoja zake zilikukuna na hiyo ndio kasoro pekee uliyoiona kutokana na utashi wako. Hebu rudi uisikilize hotuba yake. Kipindi alichobeba zege ni baada ya kumaliza degree, yaani kabla hajaanza masters na kuwa sponsored na BoT.
 
Mkuu, karibu sana jukwaani.

Vitu vingine ni common sense tu.............mtu mweledi, mtu aliyetoka kwenyefamilia masikini, anaejua mzigo wa umasikini wake na umasikini wa wzazi na ndugu zake; ilikuaje akaoa akiwa shule? alitoa wapi fedha za kuanza kuwa na mwenza?

Au hakuwa mke bali mchumba au kuoa ilikuwa kipaumbele chake?

Jadili vitu vya msingi ukitoka familia maskini ndo usioe suala la ndoa ni la mapenzi baina ya wawili.
 
Ili Kumaliza huu mzozo tunamuomba Ndugu Mwigulu arudi tena akabebe zege hata kwa siku moja tu,ili tuyaamini anayosema.Huu siyo muda wa kutafuta huruma ya watanzania hasa masikini, bali ni muda wa kuwa na huruma sana juu ya umasikini wao.
 
Mkuu, karibu sana jukwaani.

Vitu vingine ni common sense tu.............mtu mweledi, mtu aliyetoka kwenyefamilia masikini, anaejua mzigo wa umasikini wake na umasikini wa wzazi na ndugu zake; ilikuaje akaoa akiwa shule? alitoa wapi fedha za kuanza kuwa na mwenza?

Au hakuwa mke bali mchumba au kuoa ilikuwa kipaumbele chake?

Asante Bigi...

Hilo la kuoa kabla ya kazi ni jambo la kawaida sana kwa watu wenye background ya vijijini/mijini...

Wengi wameoana wakiwa hohehahe..

So mimi simshangai Mwigulu kuoa kabla ya kupata kazi...Ni jambo la kawaida sana kwa 'watoto wa wafugaji' na wale wa wakulima
 
bantulile
Hivi ushawahi kusikia Mwigulu akifanya matanuzi au kufanya mambo makubwa au kufanya jambo lolote lile linaloambatana na matumizi makubwa ya fedha tangu aukwae Uwaziri?

Jambo pekee ambalo alilifanya Mwigulu labda ni ile ziara aliyoifanya mikoani akaishia kupigwa stop na Kinana kufuatia fitina za Nape.Mwigulu na Nape hewaivi kisiasa hata kidogo.

Sasa kama unafuatilia maisha yake ya kisiasa yalivyo sasa mara baada ya kuukwaa unaibu waziri na kuona jinsi yalivyo ya kawaida tu, yaani hatusikii Mwigulu sijui kaonekana hotel gani au ukumbi gani wa starehe au kajenga mjengo wa maana sehemu flani tofauti na walivyo wenzie then kwanini hutaki kukubali kuwa jamaa hayo maisha aliyoyasimulia kuyaishi ndiyo anayoyaishi?
 
Last edited by a moderator:
Naona vijana wanaonekana wana mapenzi na Mwingulu.

Hapiti term hii, maana yake hadi 2025. Na term hyo hataweza pita tena hdi 2035.

Ok, tumuombee afya na uzima. Koz kama ana miaka 40+ 20= 60. Bado atakua na nguvu.
 
Hata mimi jana nilishangaa pia wakati anasema kua alibeba zege na mke wake alupika mama ntilie nilijaribu angalia body language yake nikagundua alikua akidanganya
 
No,jana hata mimi nilimsikiliza kijana huyu.Ni kama nilimsikia akiseme mkewe alikuwa mama ntilie kwenye site moja ya ujenzi Dar.Sikumbuki kama yeye mwenyewe alisema alibeba zege.Lakini naomba niseme ukweli kwamba hata mazingira ya mkewe kuwa mama ntilie niliyatilia shaka.

Hata hivyo nikiyakumbuka matusi ya Mwigulu sometimes huko nyuma alipokuwa anawatukana upinzani, napata picha kwamba kijana huyu ni opportunist, ingawa hotuba yake ililenga matatizo ya Watanzania kwa sasa.An opportunist changes with circumstances, he cannot make a good president.

Nilimwamini Kikwete akaniangusha,siwezi kumwamini mtu yeyote tena,hasa akiwa anatoka CCM.
Abebe zege asibebe hayatuhusu tujadili vitu vya msingi sio kumjadili mtu eti kasema alibeba zege.
 
Back
Top Bottom