Mwigulu Nchemba ndani ya Dakika 45 leo saa 3 usiku

Mwigulu Nchemba ndani ya Dakika 45 leo saa 3 usiku

nitampa kura yangu kama atataja wale wa stanbic
 
Nashukuru sana kwa taarifa maana imenisaidia kubadili channel ... Nilitegemea Lisu atusaidie kuchambua madhaifu ya muungano na suluhisho la muungano kwa maslahi mapana ya nchi ... Huyu Nchemba msakatonge alieshindwa kuwalipa wastaafu mafao yao, ameshindwa kukusanya kodi kwenye madini, ameshindwa kukusanya kodi kwenye mazao ya baharini, ameshindwa kushusha PAYEE, ameshindwa kupunguza gharama kubwa za maisha.... Hana Jipya Zaidi ya kuja kutuhadaa na mabango aliyojiandikia yeye mwenyewe kwa kujiita JesusChalie ...
 
Mwigulu Nchemba si alikuwa na vipindi kama viwili miezi michache iliyopita,sasa hii sifa tangia atimize miaka 40,amekuwa mtamu.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu wana JF,
Kwa muda sasa nimekuwa nikifatilia kauli za Mh. Mwigulu, kwa kweli napata utata mkubwa. Yani anapoongea inakuwa kana kwamba yeye ndiye waziri Wa fedha. Mara nyingi anatumia kauli kama "nimeagiza..., nimefuta... Nime...." Ila kwa wizara zingine naibu waziri huwa hawaongei kwa mamlaka kama ya Mwigulu.
Kwa mtazamo wangu ni kwamba inawezekana waziri wa fedha ni boya, au Mwigulu anaamua kwa makusudi kumfunika boss wake Na kujitafutia umashuhuri wa kisiasa.

Ni mtizamo tuu!!
 
Anakomaa pesa ya ESCROW kwa kua mgao wake ulikua mdogo.. Jinga kabisa alafu tunapita mitaa yake tunaona anachafua kuta!!!!
 
Heri umeliona hilo. Buhorera ni tikisa kichwa tu liende. Anasahau mtangazaji huwakilisha na kuvaa viatu vya wasikilizaji wake. huuliza maswali ambayo tungeuliza sisi.....

Kama hawezi awaachie wengine....
 
Anasema mtu akichota pesa ya umma, akaachishwa kazi pasipo kushtakiwa ni sawa na kwamba ume m -send off akatumie vizuri ile pesa.
 
Anasema watu wa ESCROW wamepewa send-off!!! hapa ni kukubali kuwa serikali ni dhiaifu!! hakuna ubishi!! pia ni kukubali kuwa rasimu yenu ya KATIBA haiwabani mafisadi!!huu ni udhaifu wa sheria.. serikali lazima ione udhaifu huo!!
 
Nchi hii itafikia uchumi wa kati endapo tu,mh.Mwigulu Nchemba ama mh lowassa atagombea urais 2015
 
Du kazikweli umenikumbusha alichangia maazimio ya pac nikadhani kesho yake mh rais kikwete atamteua awe waziri mkuu lakini baada ya hotuba ya rais nikajiona mimi kumbe nilikuwa nafanya ushabiki maandazi tu
 
Kuliko kupoteza muda kumuangalia nchemba angalia HBO wana Movie nzuri yazamani kidogo : " Body of Lies"
 
Back
Top Bottom