Mwigulu Nchemba ndani ya Dakika 45 leo saa 3 usiku

Mwigulu Nchemba ndani ya Dakika 45 leo saa 3 usiku

yule buhoera ni bonge la fara hajielewi lile likipindi kake nilakulipia ndio unaalikwa kwenda kupiga polojo sasa makamanda wa chadema wameshazoea kupata majukwa bure bila kuhonga shida ndio iko hapo
 
Ingekuwa uwaziri ndio unafanya uzunguke kwenye vyombo vya habari,basi pinda na mwandosya wasingekuwa wanapata hata mda wa kulaz,ufafanuzi wao unahitajika sana maana wanasimamia wizara zote.
Umenifungua macho mkuu! Kumbe huyu jamaa ni kama makamu waziri mkuu! I like that.
 
ati anawaambia waliokatiwa posho la escrow walipie kodi badala aseme zirudishwe zote!!
 
Huyu Mtangazaji Emmanuel Buhohela ni kijana lkn si mtu wa kujifunza kupitia vipindi kama hivi kwenye broadcasting houses kama BBC, VOA, CNN, Al Jazira au hapa karibu Citizen TV Kenya. Kwa mfano Citizen TV kuna kipindi cha cheche, ukiwaona watangazaji wake kwa maana ya umahiri wao na ukilinganisha na huyu Emmanuel Buholela wetu unaweza kumuomba Joyce Mhaville, Mkurugenzi wa ITV na RedioOne amfute kazi. Kibaya zaidi hana information za kutosha ya kile anachokihoji, very unfortunate.

Namshauri buhohela akajifunze kenya Kwa mtangazaji wa KTN Kama sikosei anaitwa Jeff Koinange ! Ila awe Na mkalimani maana jamaa anaongea kiingereza halisi !
 
Kipindi hiki cha 45 kinachoendeshwa na kituo cha ITV kilipoanza mara ya kwanza kusema kweli nilijua ni kipindi ambacho hata wanasiasa watakuwa wanakiogopa kwa maswali magumu na ya kufikirisha. Lakini Mimi niseme wazi kinanikera kwa mambo yafuatayo;
1. Wanaoitwa tangu kianze ni hao hao tu; kwa mfano Lukuvi,Wasira,Mwigulu,Sumayi au kwa kifupi wengi mawaziri;
2. Mtangazaji huwa sijui hajiandai maana hana maswali ya kufikirisha,na hii inasababisha aliyeitwa aanze kuongea tuuu mpaka dakika zinaisha
3. Mtangazaji huwa anaonekana yupo yupo tu,waziri atakavyoongea na yeye hana cha kumuuliza zaidi ya kuitikia

RAI YANGU KWA MTANGAZAJI (BUHOHELA)

Ebu mtangazaji amwangalie Dotto Bulembu wa Star Tv-Tuongee asubuhi atajifunza kitu. Au aangalie kipindi cha HARD TALK kiko nadhani BBC au CNN kama cjakosea.Simaanishi atangaze kama wao,namaanisha ule udadisi wa Mwendesha kipindi na kile mwalikwa anachokiongelea.

Pili,iwe moja kwa moja na si kurekodi nako, inawafanya watazamaji wajisikie vizuri,mambo ya dijitali ni kurusha kipindi live na kusema kweli itapendeza sana.

Kwa kifupi Mimi kibaniboa sana na ITV napenda kuiangalia maana hakina ubunifu wa maswali.
Sasa mkuu huyu buhohela awe na maswali yanayofikirisha kama ya kina steven sucker (hard talk wa bbc)?? Na yule mama wa cnn christina Aman pour??? Tatizo shule mkuu, hawa wetu hawawezi hapo ndipo uwezo wao umefikia, na ukiongeza na uonga, kutojiamini na kujipendekeza kwa kuuliza maswali ya kitoto ili ikiwezekana afikiriwe kwenye u dc!!! Kidogo General ulimwengu alikuwa anajitahidi kiasi chake.Hapa Tz hakuna waandishi wa habari ni wajanja wajanja tu.Siku moja Nyalandu alikuwa kwenye kipindi cha hard talk na steven sucker ilikuwa aibu kwani mtangazaji ana kuwa na data kuliko waziri!!!!! Hii ni fani kama u pilot sio ulikuwa Mc huko mtaani una sauti nzuri basi unajiita mtangazaji!!! Ona kina Richard Quest (means business) wanavyo wahoji ma CEO hadi mtu anachanganyikiwa!!!
 
Umofia kwenu wana JF,
Mwanasiasa Madelu amekuwa mtu wa kutafuta kiki sana kwenye vyombo vya habari,haipiti lisaa kama hayupo hewani clouds basi radio one,kama sio radio1 basi yupo ch10,juzi juzi alikuwa na vipindi vya dkk 45 itv,leo wamemuweka tena kabla hata hakijaisha tena yupo kwenye mkasi na salama(promo), jamaa ndoto ya kumpiku lowassa anayo kichwani mwake,sasa hii sifa kila siku kwenye vyombo vya habari.

Afanye Yoooooooote ILA Atueleze Tu Alikowazikia Wapendwa Wa Watu Kwa Kuwadedisha.
 
Mimi huwa simuelewi huyu Mhe. Mwigulu, pamoja na kufanya vizuri ktk maeneo fulani lkn namuona kama ni kiongozi anayependa sifa binafsi kuliko kuwajibika kwa pamoja. Eti kipindi fulani wakati anafanya Masters programme wanafunzi wenzie wa kutoka mataifa ya nje walikuwa wanamuita Nyerere, huyu Mwigulu ana masihala sana, Baba wa Taifa na Mwigulu kwa lipi hasa! Huyu mtu hajielewi kabisa, mara watu wanasema eti mimi ni the next Edward Moringe Sokoine. This man is not serious. Hawa wazee, Nyerere na Sokoine waachwe wapumzike, hakuna hata eliyefikia hata robo ya sifa zao ndani ya CCM ya sasa.
Hivyo ni vionjo tu vya kisiasa.kwani hata sokoine alifanya nini cha maana zaidi ya kutia watu umasikini?.
mwigulu hata ivo anajitahidi atleast
 
Namshauri buhohela akajifunze kenya Kwa mtangazaji wa KTN Kama sikosei anaitwa Jeff Koinange ! Ila awe Na mkalimani maana jamaa anaongea kiingereza halisi !

Mbali Sana Akamwone Ndugu Dotto Bulendu Wa StarTV. Jamaa Yko Vizuri Sana Yule.
 
Ni ndoto kuwa rais Mnyapaa kwa sababu ya kwenda kuhiji katika sinagogi la Babu wa Lagos !
 
Mwigulu amechachamaa na kujifagilia kwa ajili ya kampeni za urais.Anasema wakati akiwa chuo kikuu watu kutoka nje ya nchi hawakumfahamu kwa jina la Mwigulu isipokuwa la Nyerere kwa sababu ya kuwatetea waliokuwa wanaonewa.
Halafu tena kagipeleka kwenye kipindi cha Mkasi kwa ajili ya Jumatatu ijayo.Huyu jamaa anajitafutia laana kujifananisha na Yesu, Sokoine,au Nyerere.Kwa kweli ni shida!
niliwaambia mapema pamoja na kuwa Wanyiramba tunapenda sifa za kishamba lakini huyu kazidi sana
 
Buholela ni bure kabisa anapwaya sana kny kile kipindi,hana maswali magumu na ndio maana kina lukuvi,wassira na Membe wanarudi kila siku,maana wamepata ma mahali pa kujisafishia.
 
Kipindi hiki cha 45 kinachoendeshwa na kituo cha ITV kilipoanza mara ya kwanza kusema kweli nilijua ni kipindi ambacho hata wanasiasa watakuwa wanakiogopa kwa maswali magumu na ya kufikirisha. Lakini Mimi niseme wazi kinanikera kwa mambo yafuatayo;
1. Wanaoitwa tangu kianze ni hao hao tu; kwa mfano Lukuvi,Wasira,Mwigulu,Sumayi au kwa kifupi wengi mawaziri;
2. Mtangazaji huwa sijui hajiandai maana hana maswali ya kufikirisha,na hii inasababisha aliyeitwa aanze kuongea tuuu mpaka dakika zinaisha
3. Mtangazaji huwa anaonekana yupo yupo tu,waziri atakavyoongea na yeye hana cha kumuuliza zaidi ya kuitikia

RAI YANGU KWA MTANGAZAJI (BUHOHELA)

Ebu mtangazaji amwangalie Dotto Bulembu wa Star Tv-Tuongee asubuhi atajifunza kitu. Au aangalie kipindi cha HARD TALK kiko nadhani BBC au CNN kama cjakosea.Simaanishi atangaze kama wao,namaanisha ule udadisi wa Mwendesha kipindi na kile mwalikwa anachokiongelea.

Pili,iwe moja kwa moja na si kurekodi nako, inawafanya watazamaji wajisikie vizuri,mambo ya dijitali ni kurusha kipindi live na kusema kweli itapendeza sana.

Kwa kifupi Mimi kibaniboa sana na ITV napenda kuiangalia maana hakina ubunifu wa maswali.
HARD TALK kipo BBC na Steve Sucker ndiye host mwenyewe.Wanaokwenda kwa Steve Sucker siyo watu wasi wasi,Ni watu walioshiba knowledge hasa na wako well-versed in international affairs lakini bado wanashikwa na kigugumizi cha ghafla kutokana na maswali mazito mno ya yule host.Mwulize Bill Clinton na Tony Blair mbona walichanganyikiwa kwa Steve Sucker kutokana hard questions na follow-up questions zake!Huwezi kumlinganisha Sucker na hawa wa kwetu,Kawaacha mbali sana.
 
Nashukuru sana kwa taarifa maana imenisaidia kubadili channel ... Nilitegemea Lisu atusaidie kuchambua madhaifu ya muungano na suluhisho la muungano kwa maslahi mapana ya nchi ... Huyu Nchemba msakatonge alieshindwa kuwalipa wastaafu mafao yao, ameshindwa kukusanya kodi kwenye madini, ameshindwa kukusanya kodi kwenye mazao ya baharini, ameshindwa kushusha PAYEE, ameshindwa kupunguza gharama kubwa za maisha.... Hana Jipya Zaidi ya kuja kutuhadaa na mabango aliyojiandikia yeye mwenyewe kwa kujiita Jesuschalie ...

Ni Je suis Charlie, si Jesuschalie maana yake Mimi ni Charlie ni kifaransa hicho.
 
Heri umeliona hilo. Buhorera ni tikisa kichwa tu liende. Anasahau mtangazaji huwakilisha na kuvaa viatu vya wasikilizaji wake. huuliza maswali ambayo tungeuliza sisi.....

Kama hawezi awaachie wengine....
Wangekuwa Wazungu hapo wangesema....'Buholela have treated Mwigulu with kid' gloves'.Hata CNN inao baadhi ya watangazaji wa aina ya Buholela wanaoonyesha mapenzi dhahiri kwa Wanasiasa flani kule Marekani.Namkumbuka sana mtangazaji Chris Mathew aliyekuwa mshabiki mkubwa wa Barack Obama wakati anapigania kuingia madarakani 2007/8
 
ana ndoto za kuja kuwa raisi wa magaidi
 
Uwezo wa Buhohela umeishia pale,hawez kuuliza maswali yenye mashiko yanayoweza kumfikirisha mwalikwa ndio maana akina Mwigulu wanarudi ITV mara mbilimbili kwa sababu hawakumbani na hard time ktk kujibu maswali.Ushauri akaongeze ELIMU zaidi au ITV wabadilishe mtu mwingine.
 
Back
Top Bottom