Mwigulu Nchemba ndani ya Dakika 45 leo saa 3 usiku

Mwigulu Nchemba ndani ya Dakika 45 leo saa 3 usiku

Panapojitokeza na maswali lazima ajbu yeye. Na kutoa ufafanuz.

Kwa kukumbusha tu, hivi unajua Wizara ya Fedha ina Manaibu Waziri wawili?; yaani Mh. Adam Kighoma Malima & Mh. Mwigulu Nchema. Sasa iweje yeye tu ndio mtoa matamko?
 
Umofia kwenu wana JF,
Mwanasiasa Madelu amekuwa mtu wa kutafuta kiki sana kwenye vyombo vya habari,haipiti lisaa kama hayupo hewani clouds basi radio one,kama sio radio1 basi yupo ch10,juzi juzi alikuwa na vipindi vya dkk 45 itv,leo wamemuweka tena kabla hata hakijaisha tena yupo kwenye mkasi na salama(promo), jamaa ndoto ya kumpiku lowassa anayo kichwani mwake,sasa hii sifa kila siku kwenye vyombo vya habari.
 
anahitajika sana kutoa ufafanuzi wa kina wa mambo yahusuyo maendeleo ya inch kwa ujumla. kumbuka yuko wizara ya fedha.
 
Kipindi chochote cha siasa lazima kirushwe live...hivi dunia ya sasa unarecord kipindi kama cha siasa je bongofleva wafanyeje?
 
Mwigulu amechachamaa na kujifagilia kwa ajili ya kampeni za urais.Anasema wakati akiwa chuo kikuu watu kutoka nje ya nchi hawakumfahamu kwa jina la Mwigulu isipokuwa la Nyerere kwa sababu ya kuwatetea waliokuwa wanaonewa.
Halafu tena kagipeleka kwenye kipindi cha Mkasi kwa ajili ya Jumatatu ijayo.Huyu jamaa anajitafutia laana kujifananisha na Yesu, Sokoine,au Nyerere.Kwa kweli ni shida!
 
hana kosa kuagiza jambo gulani lifanyike ktk wizara yake. mwiguru siyo passive na hana masiahala kwenye masuala ya kitaifa na hapendi watu lege lege. kinacho kushangaza hapo hata mimi sikioni maana ni mara nyingi sana manaibu mawaziri wetu kutokea kuwa active kuliko mawaziri.
 
Mwigulu Nchemba...nilipokuwa sekondari watu wengi walikuwa wananiita Sokoine na Chuo Kikuu hasa Masta walikuwa wananiita Nyerere. Na marafiki zangu wa nje walikuwa wananiita Nyerere. Ana haki ya kujifananisha na Sokoine na Nyerere maana hamna mwenye hati miliki ya majina haya mawili. Pili, Mwigulu Nchemba anasema..nilipoenda ziara Geita kuna mtu alibeba bango kibwa lililosomeka.....Mwigulu Nchemba ndiyo huyu au timtegemee mwingine...hapa Mwigulu akajifananisha na Yesu...pia ana haki maana hamna mwenye haki miliki ya jina la Yesu. Kwa hiyo matendo yake ni kama ya;
a) Sokoine
b) Nyerere au
c) Yesu.

Mtangazaji ni kutikisa kichwa tu juu na chini.
 
kipindi hiki cha 45 kinachoendeshwa na kituo cha itv kilipoanza mara ya kwanza kusema kweli nilijua ni kipindi ambacho hata wanasiasa watakuwa wanakiogopa kwa maswali magumu na ya kufikirisha. Lakini mimi niseme wazi kinanikera kwa mambo yafuatayo;
1. Wanaoitwa tangu kianze ni hao hao tu; kwa mfano lukuvi,wasira,mwigulu,sumayi au kwa kifupi wengi mawaziri;
2. Mtangazaji huwa sijui hajiandai maana hana maswali ya kufikirisha,na hii inasababisha aliyeitwa aanze kuongea tuuu mpaka dakika zinaisha
3. Mtangazaji huwa anaonekana yupo yupo tu,waziri atakavyoongea na yeye hana cha kumuuliza zaidi ya kuitikia

rai yangu kwa mtangazaji (buhohela)

ebu mtangazaji amwangalie dotto bulembu wa star tv-tuongee asubuhi atajifunza kitu. Au aangalie kipindi cha hard talk kiko nadhani bbc au cnn kama cjakosea.simaanishi atangaze kama wao,namaanisha ule udadisi wa mwendesha kipindi na kile mwalikwa anachokiongelea.

Pili,iwe moja kwa moja na si kurekodi nako, inawafanya watazamaji wajisikie vizuri,mambo ya dijitali ni kurusha kipindi live na kusema kweli itapendeza sana.

Kwa kifupi mimi kibaniboa sana na itv napenda kuiangalia maana hakina ubunifu wa maswali.

naunga mkono inaonekana hiki kipindi kimegeuka ganga njaaa ......inawezekana ukitoa hata laki unaalikwa ....sijui muongozaji wa kipindi anafanya nini ....kama recycling ya wanaokaribishwa ni hiyo hiyo ...
 
Mwigulu Nchemba...nilipokuwa sekondari watu wengi walikuwa wananiita Sokoine na Chuo Kikuu hasa Masta walikuwa wananiita Nyerere. Na marafiki zangu wa nje walikuwa wananiita Nyerere. Ana haki ya kujifananisha na Sokoine na Nyerere maana hamna mwenye hati miliki ya majina haya mawili. Pili, Mwigulu Nchemba anasema..nilipoenda ziara Geita kuna mtu alibeba bango kibwa lililosomeka.....Mwigulu Nchemba ndiyo huyu au timtegemee mwingine...hapa Mwigulu akajifananisha na Yesu...pia ana haki maana hamna mwenye haki miliki ya jina la Yesu. Kwa hiyo matendo yake ni kama ya;
a) Sokoine
b) Nyerere au
c) Yesu.

Mtangazaji ni kutikisa kichwa tu juu na chini.

this is insulting and nausea ..unaweza kutapika Kama Kweli mgombea urais anajitambulisha kwa hoja dhaifu hivi .......yaani yeye 7/7 days ..ni Kuuza sura tu ..kazi sijui anafanya saa ngapi
 
ndugu wana jf,
kwa muda sasa nimekuwa nikifatilia kauli za mh. Mwigulu, kwa kweli napata utata mkubwa. Yani anapoongea inakuwa kana kwamba yeye ndiye waziri wa fedha. Mara nyingi anatumia kauli kama "nimeagiza..., nimefuta... Nime...." ila kwa wizara zingine naibu waziri huwa hawaongei kwa mamlaka kama ya mwigulu.
Kwa mtazamo wangu ni kwamba inawezekana waziri wa fedha ni boya, au mwigulu anaamua kwa makusudi kumfunika boss wake na kujitafutia umashuhuri wa kisiasa.

Ni mtizamo tuu!!


only kwenye baraza hili la mawaziri ambapo maana ya waziri na naibu waziri inapotoshwa wazi wazi ...na wasimamizi wanakaa kimya ....
Maboya kama nyalandu na nchemba wanaweza hata kupanda vyeo kwa kufanyia kazi maelezoo au kucheza na media
 
Haina haja ya kutukana mbona wakija wapinzani kama mchungaji msigwa, tundu lisu, kafulila na wengine hua hamtukani. lazima mkubali hoja za wenzenu. nyie akija mpinzan kipindi kizuri akija wa ccm kipindi kibaya tuwaeleweje sasa.
 
Hivi hakunaga watu wengine wa dakika 45? mbona kila siku ni hao hao tu?
 
Kipindi hiki cha 45 kinachoendeshwa na kituo cha ITV kilipoanza mara ya kwanza kusema kweli nilijua ni kipindi ambacho hata wanasiasa watakuwa wanakiogopa kwa maswali magumu na ya kufikirisha. Lakini Mimi niseme wazi kinanikera kwa mambo yafuatayo;
1. Wanaoitwa tangu kianze ni hao hao tu; kwa mfano Lukuvi,Wasira,Mwigulu,Sumayi au kwa kifupi wengi mawaziri;
2. Mtangazaji huwa sijui hajiandai maana hana maswali ya kufikirisha,na hii inasababisha aliyeitwa aanze kuongea tuuu mpaka dakika zinaisha
3. Mtangazaji huwa anaonekana yupo yupo tu,waziri atakavyoongea na yeye hana cha kumuuliza zaidi ya kuitikia

RAI YANGU KWA MTANGAZAJI (BUHOHELA)

Ebu mtangazaji amwangalie Dotto Bulembu wa Star Tv-Tuongee asubuhi atajifunza kitu. Au aangalie kipindi cha HARD TALK kiko nadhani BBC au CNN kama cjakosea.Simaanishi atangaze kama wao,namaanisha ule udadisi wa Mwendesha kipindi na kile mwalikwa anachokiongelea.

Pili,iwe moja kwa moja na si kurekodi nako, inawafanya watazamaji wajisikie vizuri,mambo ya dijitali ni kurusha kipindi live na kusema kweli itapendeza sana.

Kwa kifupi Mimi kibaniboa sana na ITV napenda kuiangalia maana hakina ubunifu wa maswali.

Huyu Mtangazaji Emmanuel Buhohela ni kijana lkn si mtu wa kujifunza kupitia vipindi kama hivi kwenye broadcasting houses kama BBC, VOA, CNN, Al Jazira au hapa karibu Citizen TV Kenya. Kwa mfano Citizen TV kuna kipindi cha cheche, ukiwaona watangazaji wake kwa maana ya umahiri wao na ukilinganisha na huyu Emmanuel Buholela wetu unaweza kumuomba Joyce Mhaville, Mkurugenzi wa ITV na RedioOne amfute kazi. Kibaya zaidi hana information za kutosha ya kile anachokihoji, very unfortunate.
 
anahitajika sana kutoa ufafanuzi wa kina wa mambo yahusuyo maendeleo ya inch kwa ujumla. kumbuka yuko wizara ya fedha.

Ingekuwa uwaziri ndio unafanya uzunguke kwenye vyombo vya habari,basi pinda na mwandosya wasingekuwa wanapata hata mda wa kulaz,ufafanuzi wao unahitajika sana maana wanasimamia wizara zote.
 
tangu aondoke Suleimani Semunyu Kipindi hiki kimepoteza ubora wake.hivi Semunyu yupo wapi?

Suleiman Semunyu alikuwa almost vile vile anavyokiendesha huyu Emmanuel Buhohela. Hawana taarifa za kutosha kwa mada inayoongelewa, seems, not prepared to interview such big fishes.
 
Ana weweseka zile damu za wasio na hatia pale Arusha.Rais si lelemama.Inahitaji mtu asiye na mawaa hata kidogo.Mtu asiye na hata chembe ya kashfa ya aina yeyote,kama lakutumia jina la mtu
 
Back
Top Bottom