Mwigulu Nchemba ndani ya Dakika 45 leo saa 3 usiku

Mwigulu Nchemba ndani ya Dakika 45 leo saa 3 usiku

Robert PR

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2014
Posts
591
Reaction score
57
wanajamvi leo nimeona Tangazo la Mwigulu Nchemba ITV kwamba atakuwepo kipindi cha dakika 45 saa 3 usiku mwenye update aweke hapa wakuu.
 
Mwenye update muda ukifika atuwekee hapa wakuu jamvini.
 
fisadi namba 1, tangu lini pesa za wizi zikatozwa kodi, anatumiwa ili kutakatisha pesa chafu
 
Kipindi hiki cha 45 kinachoendeshwa na kituo cha ITV kilipoanza mara ya kwanza kusema kweli nilijua ni kipindi ambacho hata wanasiasa watakuwa wanakiogopa kwa maswali magumu na ya kufikirisha. Lakini Mimi niseme wazi kinanikera kwa mambo yafuatayo;
1. Wanaoitwa tangu kianze ni hao hao tu; kwa mfano Lukuvi,Wasira,Mwigulu,Sumayi au kwa kifupi wengi mawaziri;
2. Mtangazaji huwa sijui hajiandai maana hana maswali ya kufikirisha,na hii inasababisha aliyeitwa aanze kuongea tuuu mpaka dakika zinaisha
3. Mtangazaji huwa anaonekana yupo yupo tu,waziri atakavyoongea na yeye hana cha kumuuliza zaidi ya kuitikia

RAI YANGU KWA MTANGAZAJI (BUHOHELA)

Ebu mtangazaji amwangalie Dotto Bulembu wa Star Tv-Tuongee asubuhi atajifunza kitu. Au aangalie kipindi cha HARD TALK kiko nadhani BBC au CNN kama cjakosea.Simaanishi atangaze kama wao,namaanisha ule udadisi wa Mwendesha kipindi na kile mwalikwa anachokiongelea.

Pili,iwe moja kwa moja na si kurekodi nako, inawafanya watazamaji wajisikie vizuri,mambo ya dijitali ni kurusha kipindi live na kusema kweli itapendeza sana.

Kwa kifupi Mimi kibaniboa sana na ITV napenda kuiangalia maana hakina ubunifu wa maswali.
 
wajifunze chanel 10 kipindi cha baragumu live!mimi sikifuatilii kabisa siku hizi......sura zilezile..wasira..lukuvi...mwigulu.....sumaye....hoja nyepesi....kinaboa
 
Wabadilike......yaani unamuona mtangazaji hana swali hata la kuuliza. Anauliza basi kwa sababu kuna kuuliza. Nikikiona tu natoa maana kusema kweli nilitegemea sana kingekuwa kipindi cha kuigwa lakini mtangazaji hana ubunufu. Hata ambao hatujui utangazaji maana ndo walaji nikiwemo Mm kinaniboa sana. Nasema haya kwa sababu tu kumfanya mtangazaji huyu abadilike nahisi watampa taarifa wenzake au yeye maana wanaingia humu
 
Buhohela huwa hana maswali magumu! I wish angejifunza kwa Amanpur ama kile kipindi cha BBC Hard Talk ... Nahisi huyu Jamaa huwa anavutiwa mshiko kwanza ndo maana anakuwa legelege ...

Kipindi hiki cha 45 kinachoendeshwa na kituo cha ITV kilipoanza mara ya kwanza kusema kweli nilijua ni kipindi ambacho hata wanasiasa watakuwa wanakiogopa kwa maswali magumu na ya kufikirisha. Lakini Mimi niseme wazi kinanikera kwa mambo yafuatayo;
1. Wanaoitwa tangu kianze ni hao hao tu; kwa mfano Lukuvi,Wasira,Mwigulu,Sumayi au kwa kifupi wengi mawaziri;
2. Mtangazaji huwa sijui hajiandai maana hana maswali ya kufikirisha,na hii inasababisha aliyeitwa aanze kuongea tuuu mpaka dakika zinaisha
3. Mtangazaji huwa anaonekana yupo yupo tu,waziri atakavyoongea na yeye hana cha kumuuliza zaidi ya kuitikia

RAI YANGU KWA MTANGAZAJI (BUHOHERA)

Ebu mtangazaji amwangalie Dotto Bulembu wa Star Tv-Tuongee asubuhi atajifunza kitu. Au aangalie kipindi cha HARD TALK kiko nadhani BBC au CNN kama cjakosea.

Kwa kifupi Mimi kibaniboa sana na ITV napenda kuiangalia maana hakina ubunifu wa maswali.
 
Aisee huyu Doto Bulembu wa star tv ni namba nyingne, anajiamini na anajua kuchokoza zile angle muhimu. Big up to him.
 
Hivi kuna mtu anaweza kupoteza muda wake kumsikiliza mwigulu nchemba. Hana mvuto na maelezo yake.
 
Back
Top Bottom