Mwigulu Nchemba na kitambaa cha bendera ya Taifa.

Vaa uzalendo!

Uzalendo CCM mmekuja kuujua uzeeni?? Mmekuja na kauli hiyo ili mdanganye tena wananchi??' Naona hii kauli yenu ya sasa ndiyo itaandikwa kwenye mabango, kanga, kofia, mashati na tisheti zenu 2015''
 
Naomba kuwauliza wadau wa Jf, kwa anayemfahamu vizuri mbunge wa Iramba Magharibi na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM na aliyekuwa Meneja wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Arumerumeru mashariki (Ndg Sioi Sumari) kupitia CCM Mh: Mwigulu Nchemba,.

Kuanzia nimemfahamu mbunge huyu kila nimuonapo huwa anapenda kujifunga kitambaa chenye nembo ya taifa shingoni mwake, huwa hakitoi kile kitambaa chenye nembo ya taifa shingoni mwake,'.

Swali ni je' huo ni uzalendo na nchi yake?? au anapenda tu kutoka kihivyo?? au ndivyo alivyoagizwa afanye na wataalamu wake ili asiterereke kisiasa?? au kuna kitu anaficha kwenye shingo yake???

Naomba majibu kwenu maana nimetafakari nikakosa jibu sahihi.

Msikilize hapa anajibu hili swali mwenyewe
 
Last edited by a moderator:
Naomba kuwauliza wadau wa Jf, kwa anayemfahamu vizuri mbunge wa Iramba Magharibi na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM na aliyekuwa Meneja wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Arumerumeru mashariki (Ndg Sioi Sumari) kupitia CCM Mh: Mwigulu Nchemba,.

Kuanzia nimemfahamu mbunge huyu kila nimuonapo huwa anapenda kujifunga kitambaa chenye nembo ya taifa shingoni mwake, huwa hakitoi kile kitambaa chenye nembo ya taifa shingoni mwake,'.

Swali ni je' huo ni uzalendo na nchi yake?? au anapenda tu kutoka kihivyo?? au ndivyo alivyoagizwa afanye na wataalamu wake ili asiterereke kisiasa?? au kuna kitu anaficha kwenye shingo yake???

Naomba majibu kwenu maana nimetafakari nikakosa jibu sahihi.
Mkuu do you have a problem with that?...............au ndio wale watu wanachikia tu kila kitu kinachofanywa na mpinzani wako
 
f-mbowepress.jpg

hapo mwenyekiti wangu anasema, peoples!
 
bendera ni nyara ya serikali. Anakosea na adhabu yake ni kifungo kisichozidi miaka 20
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mkuu do you have a problem with that?...............au ndio wale watu wanachikia tu kila kitu kinachofanywa na mpinzani wako

Nimeuliza maana yake, naona urudie kusoma thread niliyoandika halafu unipe jibu maana hapo hujajibu!
 
Nchemba kama walivyo wana-CCM wengi wanajiona wakuu juu ya sheria. Matumizi ya alama/nembo za taifa including bendera ya Taifa yameelezwa. Na hata bungeni lilishaulizwa swali kuhusu tabia ya Nchemba kuvaa kitambaa chenye rangi za bendera ya Taifa, na Mh Lissu alisimama na kueleza kufungu cha sheria na hivyo Naibu Spika alimtaka Nchemba kuvua.

Lakini kwa sababu anazojua yeye mwenyewe Nchema ameona he is above the law, pengine hii tabia ya kulamba miguu akifikiri kuwa kuvaa bendera kunamfanya yeye aonekane mzalendo zaidi! Amekuwa BOT kipindi taasisi hiyo inabiwa mchana kweupe, uzalendo wake ulikuwa wapi? Bungeni ametoa hoja gani ya maana inayoonesha kuwa kweli ni mzalendo beyond mavazi?

Nikiwa bado kwenye bendera, ningependa kujua ni kwanini bunge/wabunge (wote) wameona ni sahihi kutumia rangi za bendera ya Taifa kwenye zulia (carpet)? Wabunge wanakanyaga bendera ya taifa kila siku na miguu yao iliyojaa rushwa! Wabunge wapo juu ya sheria? Sijamsikia mbunge yoyote akilisemea hili bungeni na naona kama tumepoteza mwelekeo maana sasa bendera inageuzwa kuwa zulia!

FJM,
suala la wabunge kukanyaga bendera ya taifa liliwahi semwa bungeni spika alikuwa anamjibu mwananchi aliyewaambia kwanini wanakanyaga bendera ya taifa, spika alitoa majibu mepesi, eti hizo ni rangi tu siyo bendera ya taifa.
 
Kwa kuwa ni mwenzetu humu jamvini, naamini atatinga kutoa maelezo kwa kina.

joji kwa taarifa tuu,Mwigulu na Mwenzetu ni watu wawili tofauti................,hivyo basi Mwigulu si Mwenzetu na Mwenzetu si Mwigulu,Mwenzetu anakitambaa anachoweka mfukoni almaarufu kwa jina la handkerchief,....tusubiri tusikie kitambaa cha Mwigulu.
 
Msubirini aje amwage pumba zake humu, Magamba wote wakiulizwa maswali wao wanayachukulia wepesi wepesi. Hakuna hata Magamba wenyewe majibu ya kuridhisha zaidi ya Dharau na ujinga walionao, likianzia na lile la Magogoni ndio punguwani kabisaa halijijiu wala halijitambui pumba na upumbavu kwenda mbele
 
Nchemba kama walivyo wana-CCM wengi wanajiona wakuu juu ya sheria. Matumizi ya alama/nembo za taifa including bendera ya Taifa yameelezwa. Na hata bungeni lilishaulizwa swali kuhusu tabia ya Nchemba kuvaa kitambaa chenye rangi za bendera ya Taifa, na Mh Lissu alisimama na kueleza kufungu cha sheria na hivyo Naibu Spika alimtaka Nchemba kuvua.
Nchi yenye sheria legelege utaijua tu!
Ukipita Kariakoo, mitaani, maduka ya watalii, utaona vifaa kadhaa vyenye bendera ya taifa vinauzwa: T-Shirts, track suits, vitambaa vya shingoni, kofia, kanga...tunajua vinaishia wapi vitu hivi? Kuna "utakatifu wowote katika bendera ya nchi? Kama ni hivyo, kwa nini mataifa mengi wanavaa bendera zao vichwani na kuna tafauti gani na bendera ya Tanzania?

Masikini mimi sijui hata hizo kanuni zinazoilinda bendera ya taifa letu, ninaona tu katika nchi nyengine wanaikashifu bendera ya nchi fulani kwa kuichoma moto.

Hapo juu kwenye red, mimi nisiyekuwa Nchemba, nikivaa kitambaa cha bendera ya taifa nitaadhibiwa kisheria? Na hapa hoja ya msingi ni nini, tunajadili maadili na matumizi ya bendera ya taifa au tunamjadili Nchemba tu?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom