Mwigulu Nchemba na tai, skafu na fulana zenye rangi ya bendera ya Taifa

Konda wa bodaboda

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
7,981
4,166
Huyu mheshimiwa Nchemba ni mzalendo wa kweli kwa taifa lake. Kila alipo anatanguliza alama ya taifa lake Tanzania.Hata sasa bungeni amevaa suti na tai yenye rangi ya bendera ya taifa. Wapo wanaoogopa kuonekana hawajapendeza, lakini mhe. Nchemba hajali, utanzania kwake ni kitu cha maana sana kuliko kupendeza.

Big up mzalendo Mwigulu hakika ni mfano mzuri kwa wazalendo wachanga.
 
Uzalendo wa Nchi hauonyeshwi kwa mavazi. Je ni matukio mangapi ameshiriki ya kuangalia uchumi , elimu, afya, na maendeleo ya Taifa hili?. Kile kitendo tu cha kuwa mwana ccm sio uzalendo bali muuaji wa Taifa.
 
Sio tu mzalendo lakini pia ni mchafuzi mzuri wa mazingira ya taifa lake kwa zile 'Mwigulu rais wetu 2015' Tanzania nzima.

Hivi atafuta lini?
 
Uzalendo haupimwi Hivyo Ndg yangu!! Kuvaa skafu,tai yenye bendera ya taifa siyo uzalendo.

Uzalendo hupimwa kwa Namna ambayo unajitoa kwa Nguvu zako zote kwa ajili ya Ujenzi wa taifa lako na Siyo kuvaa skafu,bendera ya nchi nk,
Muasisi wa Nchi hii baba wa taifa Mwl Jk Nyerere alikuwa mzalendo,Waziri mkuu ngudu Edward Sokoine alikuwa mzalendo na baadhi ya wengi ambao waliipigania nchi hii dhidi ya Umasikini,Maradhi na Ujinga walikuwa wazalendo.

Viongozi wetu wengi wa sasa wako kimaslahi sana,Uzalendo haupo ndani yao,Ndiyo maana wanaona Sahihi kupiga Dili za Mabilioni bila ya kuwa na huruma kwa wananchi!!

* Kiongozi anatamka mbele ya Bunge kuwa hiyo ni hela ya Mboga wakati wananchi wake hawana uhakika wa milo mitatu halafu unataka tumwite Mzalendo??

* Viongozi wanafanya biashara haramu halafu unataka tuwaite wazalendo?? Pembe za Ndovu kila siku zinakamatwa Nje,huu ni uzalendo kweli??

* Viongozi wanaishi kwenye Utajiri wa hali ya juu sana,Huo sio uzalendi ilhali waliokuzunguka ni Masikini wa kutupwa.

* Watoto wa Viongozi hawasomi Nchini,Hata hili unataka tujivunie kuwa tu wazalendo?? Nahitaji kupimwa akili kwa haya.

*****************************

* Hebu jaribu kutupilia jicho la tatu kwa Mifano ya Hawa wawili.

1,Mwl Julius Kambarage Nyerere.
2,Mh Edward Moringe Sokoibe.

Waliiaga dunia sote tukifahamu kuwa hakukuwa na Taasisi,Kampuni au Chochote cha wanawe Madaraka,Makongoro, Grace na Namelock pamoja na wake zao!

Waliiaga dunia wakiwa na Nyumba za kawaida na siyo haya Ma-hekalu yaliyojaa Nchini ya viongozi wetu wasio na huruma na kodi zetu.

Wachunguze viongozi wa sasa kwa umakini,Kama yeye siyo Mmiliki basi Mwanae,Mkewe ni Mmiliki wa jambo fulani.
Wana Mahekalu kila Mkoa,Hoteli,Apartment nk.

Viongozi wetu siyo wazalendo,Kama wapo Naomba unitajie japo kwa Majina!!

Asalaam.
 
Huyu mheshimiwa Nchemba ni mzalendo wa kweli kwa taifa lake. Kila alipo anatanguliza alama ya taifa lake Tanzania.Hata sasa bungeni amevaa suti na tai yenye rangi ya bendera ya taifa. Wapo wanaoogopa kuonekana hawajapendeza, lakini mhe. Nchemba hajali, utanzania kwake ni kitu cha maana sana kuliko kupendeza.

Big up mzalendo Mwigulu hakika ni mfano mzuri kwa wazalendo wachanga.

Hebu tuone picha yake!
 
Hakika Mwigulu ni mzalendo wa kweli.
upload_2016-1-29_0-55-54.jpeg

Moja ya shule iliyopo ktk jimbo la Iramba Magharibi,ikionyesha jinsi wanafunzi wote wamekaa kwenye madawati hongera kwake mbunge kwa uzalendo uliotukuka.
 
Kuchafua mazingira kwa kuwatuma vijana waandike jina lake kwenye madaraja na kura za nyumba na kwenye mawe nako ni uzalendo? Kuratibu ulipuaji mabomu Arusha nap ni uzalendo?
 
Mtu kuvaa skafu ni uzalendo? Kama mzalendo avae kama mpoto, na atembee peku, hizo suti,skafu soksi si asili yetu.
 
Back
Top Bottom