Mwigulu Nchemba na kitambaa cha bendera ya Taifa.

KISAKA MORIS

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
372
33
Naomba kuwauliza wadau wa Jf, kwa anayemfahamu vizuri mbunge wa Iramba Magharibi na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM na aliyekuwa Meneja wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Arumerumeru mashariki (Ndg Sioi Sumari) kupitia CCM Mh: Mwigulu Nchemba,.

Kuanzia nimemfahamu mbunge huyu kila nimuonapo huwa anapenda kujifunga kitambaa chenye nembo ya taifa shingoni mwake, huwa hakitoi kile kitambaa chenye nembo ya taifa shingoni mwake,'.

Swali ni je' huo ni uzalendo na nchi yake?? au anapenda tu kutoka kihivyo?? au ndivyo alivyoagizwa afanye na wataalamu wake ili asiterereke kisiasa?? au kuna kitu anaficha kwenye shingo yake???


Naomba majibu kwenu maana nimetafakari nikakosa jibu sahihi.
 
Kwa kuwa ni mwenzetu humu jamvini, naamini atatinga kutoa maelezo kwa kina.
 
Nchemba kama walivyo wana-CCM wengi wanajiona wakuu juu ya sheria. Matumizi ya alama/nembo za taifa including bendera ya Taifa yameelezwa. Na hata bungeni lilishaulizwa swali kuhusu tabia ya Nchemba kuvaa kitambaa chenye rangi za bendera ya Taifa, na Mh Lissu alisimama na kueleza kufungu cha sheria na hivyo Naibu Spika alimtaka Nchemba kuvua.

Lakini kwa sababu anazojua yeye mwenyewe Nchema ameona he is above the law, pengine hii tabia ya kulamba miguu akifikiri kuwa kuvaa bendera kunamfanya yeye aonekane mzalendo zaidi! Amekuwa BOT kipindi taasisi hiyo inabiwa mchana kweupe, uzalendo wake ulikuwa wapi? Bungeni ametoa hoja gani ya maana inayoonesha kuwa kweli ni mzalendo beyond mavazi?


Nikiwa bado kwenye bendera, ningependa kujua ni kwanini bunge/wabunge (wote) wameona ni sahihi kutumia rangi za bendera ya Taifa kwenye zulia (carpet)? Wabunge wanakanyaga bendera ya taifa kila siku na miguu yao iliyojaa rushwa! Wabunge wapo juu ya sheria? Sijamsikia mbunge yoyote akilisemea hili bungeni na naona kama tumepoteza mwelekeo maana sasa bendera inageuzwa kuwa zulia!
 
Mganga wake ndio alivyo mwagiza,naamini pale shingoni kuna kitu.
 
Anafanya hivyo kutisha wenye wake zao, si anajulikana alivyo mkware sketi na magauni?
 
Anafanya hivyo kutisha wenye wake zao, si anajulikana alivyo mkware sketi na magauni?

Jamani mimi simwelewi kabisa, kipindi chote cha kampeni huku Arumeru hata waliofatilia kwenye vyombo vya habari nadhani mlimuona akiwa amejifunga kitambaa kile kuanzia kampeni zinaanza hadi zilipoisha na jana bungeni nimemwona kavaa sijui ni suti au kaunda suti na kitambaa kile shingoni' kulikoni Nchemba!!!
 
Magwanda ya khaki yanapokosa hoja, yanakurupuka na chochote kile. Kwi kwi kwi teh teh teh.
 
Magwanda ya khaki yanapokosa hoja, yanakurupuka na chochote kile. Kwi kwi kwi teh teh teh.

Unaona ulivyo, kama unajua sababu ya yeye kufanya hivyo jibu, kama hujui haitakua vibaya kama utapita tu bila kuchangia ili watakaokuwa wana majibu wajibu.

Zomba badilika nlishakwambia jaribu kuwa na busara usije ukawa mtu wa ajabu uzee utakapoingia ndani yako badala ya kuwa na hekima kwa.
 
Unaona ulivyo, kama unajua sababu ya yeye kufanya hivyo jibu, kama hujui haitakua vibaya kama utapita tu bila kuchangia ili watakaokuwa wana majibu wajibu.

Zomba badilika nlishakwambia jaribu kuwa na busara usije ukawa mtu wa ajabu uzee utakapoingia ndani yako badala ya kuwa na hekima kwa.
f-mbowepress.jpg

 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom