Nimepata taarifa ya kusambaa kwa barua ambayo amepewa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndg Mwigulu Nchemba, yenye maudhui ya katazo la kufanya ziara.
Kimsingi ni sahihi kuwa Mhe Mwigulu, Mbunge wa Iramba, Naibu waziri wa fedha na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara amepewa barua ya kumtaka kusitisha ziara zake kwa minajali kuwa;
Ziara zake hazifuati utaratibu wa chama, ambao unataka ziara hizo kupangwa na kuratibiwa katika mfumo wa vikao rasmi ndani ya Chama.
Mwigulu ni miongoni mwa wanaotajwa kuwania Urais kwa tiketi ya CCM, na imehisiwa kuwa ziara hizo ni maandalizi na kampeni ya kujiandaa kwa jambo hilo kubwa.
Msimamizi wa Kanuni na Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ni Katibu Mkuu na ndiye mwenye mamlaka ya kusimami shughuli za kila siku za chama hicho. Hii ni pamoja na ku-oversight utendaji wa subordinates wake (Mwigulu akiwemo)
Suala hili limeshaibua mijadala katika forum mbalimbali, mijadala yenye hoja na hisia mbalimbali, baadhi wakiiunga mkono hatua hiyo na wengine wakiipinga.
Wanaoipinga wanastress on the point kuwa ziara hizo zinajenga chama, zinarudish imani ya watu kwa Chama na watendaji wake. Ni ukweli kuwa kukubalika kwa Mwigulu ndio kukubalika kwa CCM and vice versa is true.
Katika kipindi ambacho wananchi wamevurugwa na mitazamo inayosimamiwa na ukawa inayokipaka chama cha mapinduzi matope, ziara hizo zilikuwa ni dozi ya nyongeza baada ya ile ya Katibu Mkuu.
Hoja nyingine inahoji busara iliyotumika, ikiwa kutangaza nia ya urais kunamuondolea kiongozi muandamizi wa Chama haki ya kufanya kazi yake ndani ya Chama, basi kanuni zetu hazituongozi sehemu salama, ikiwa waziri mkuu kutangaza kwake nia kungemfanya apate katazo la kufanya kazi zake kiserikali, ama waziri ama naibu waziri basi tungekuwa na taifa la ajabu. Ikiwa watu wanaofanya kazi za taasisi zetu kwa umakini na ari wanapoteza sifa siku tu wanapoonekana kuwa wanahamu ama kuna hisia tu kuwa wanataka nafasi za juu zaidi za utumishi kwa Chama na Serikali...wanahoji busara hii.
Lakini hoja nyingine ni ya ulinganishi (comparison analysis) inayodai kuwa zipo taarifa mbalimbali za makada wa CCM na baadhi viongozi ambao wanakihujumu chama waziwazi, kwa maneno na matendo na hatua za makatazo na karipio hazijaelekezwa kwao. Lakini hoja hii pia inatanuka na kutathmin athari zinazopatikana kwa Ziara za Mwigulu ndani ya Chama na Nje ya Chama ndani ya jamii, na madhara yatakayopatikana kwa kusitishwa kwake na watetezi wa hoja hii wanasema madhara yake ni makubwa kuliko athari zake.
Wanaounga mkono hatua hiyo ya Katibu Mkuu wanatoa hoja zifuatazo;
katika kipindi ambacho baadhi ya watarajiwa wakiwa wanaendelea kutumikia adhabu, si busara wala haki kuwaacha wengine wanaofanya mfano wa yale waliyoyafanya wao waachwe wakiendelea kwa mwamvuli wa nafasi zao ndani ya Chama. Chama hiki kimejengwa katika misingi ya Haki, Usawa na Uadilifu, si vyema kwa katibu mkuu kuendesha chama nje ya misingi hiyo.
chama ni taratibu, siku CCM kikiacha kanuni zake, misingi yake na mila yake hakitabaki chama salama na itakuwa ndio mwisho wake. Na kimsingi utaratibu unaeleweka wazi kuwa muda wa kampeni bado, hivyo ni sahihi bila kujali nafasi, hadhi ama cheo kila mmoja akafuata utaratibu huo na atakayeenda kinyume achukuliwe hatua za kinidhamu kama ilivyokwishafanyika kwa wengine.
Ziara hizo hazijengi chama, bali zinalenga kumjenga mtu binafsi, kwa maana zinalenga kumjenga Mwigulu kama yeye na wala si kwa manufaa ya Chama, na zipo kimkakati maalum unaolenga Urais 2015.
Kimsingi mjadala huu utaendelea kujengwa kwa hoja zenye tafsir mbalimbali na zinategemewa hoja hizo kuijenga ama kuibomoa taswira ya MWIGULU lakini pia kwa kiwango hicho hicho na hoja hizo hizo zinaweza kujenga chama kwa maana kitachukuliwa ni chenye kusimamia taratibu zake na chenye kufanya maamuzi lakini pia zinaweza kuharibu murua wa chama na kutoa taswira kuwa ktk chama hicho kuna vita kali ya wenye uchu wa madaraka ambao hawafikirii chochote kwa maslahi ya chama hicho isipokuwa kukalia kiti cha Urais.
Hii ni tathimini tu..
By:
ALLEX KOWE.

Last edited by a moderator: