Mwigulu Nchemba na kiingereza cha Kayumba mahakamani...

Alfred Daud Pigangoma

JF-Expert Member
Mar 30, 2009
1,826
966
Katika hali isiyo ya kawaida katika kesi ya kupinga matokeo katika jimbo la Igunga ambapo Mbunge P. Kafumu alipita kwa njia za panya huku mpiga debe wake akiwa ni Mwigulu Nchemba amepelekea wanachama wa CHADEMA kufungua kesi ya kupinga ushindi huo wakiongozwa na Mwl. J. Kasindye ambaye alikuwa mgombea kwa tiketi ya CHADEMA.

Katika mahakama ya mjini Nzega ambapo kesi hiyo inasikilizwa, jana kuliibuka kizaa zaa baada ya Sugar-Dady kuitwa kutoa ushahidi wake na kuanza kujibizana na wakili wa mlalamikaji ambaye ni Prof. Safari na hatimae Mwigulu akaanza kuongea chake ndipo Prof. Safari akamwambia "Kama huwezi kuongea kiingereza chagua moja kati ya kukaa kimya au kuongea kiswahili kwani mimi nikiongea kiingereza hapa huwezi kuendelea kwani wewe si mwanasheria hivyo kiingereza cha kisheria hukijui"

Kesi hii inaendelea kwa mfululizo katika mahakama ya mjini Nzega....
 
Ungetupa hayo maneno ya kiingereza ingekuwa safi zaidi tujue aliongea nini.
 
Anachokiweza sana Mwigulu, ni kutumia posho za kampeni kuchukulia wake wa makada wenzake, na kuongea kiingireza cha I LOVE YOU SO MUCH DEAR, MKE WA MTU. Atanywea maji kwenye karai.
 
Ungetupa hayo maneno ya kiingereza ingekuwa safi zaidi tujue aliongea nini.

Naweza kuotea alivyokuwa akiongea broken English huyu Bwana Mwigulu Mchembe kama hivi:

Mwigulu Mchembe says "Excellency,oh no,Honorauble Judge,you the,the...the,the CHADEMA,the pepoz power,the Igunga District and the CCM the kushinda. The CCM,the CDM they kick each other in the box,the CCM the kushinda Uchaguzi,the Mbunge wetu Kafumu the kushinda in the box,the kick,the bingwa,sasa the CHADEMA start the complain to the Mahakama.Why??The CCM the box is full the kula is top. Kwa hiyo the win the Uchaguzi. The CDM is finished!'"
 
Hao ndio wachumi wetu, wakienda hata cross border tu wanabaki kutikisa vichwa na kusubiri saa za chai wapige na sambusa kuvuta siku... matokeo yake tumebaki na mibwabwajo tu
 
Kinafanana na hiki?

Wewe Kifulambute!!! Umenisababishi kesi hapa ofisini.. Kwani nilipomaliza kupakua (to download) hiki kiambatanisho cha sauti ulichokiweka si ndiyo nikaanza kukisikiliza!..... Kumbe ofisini kwangu kuna mwanachama wa CUF, alipomsikia mwanachama mwenzake anamwaga lugha akanitusi kwa kuniambia "Unapenda sana kututania sisi wana-CUF mbona CCM wapo wengi %*ˆxx*:hatari:x$x# sana wewe" (kwenye mafyampufyampu nimeficha tusi naogopa BAN).
 
Wewe Kifulambute!!! Umenisababishi kesi hapa ofisini.. Kwani nilipomaliza kupakua (to download) hiki kiambatanisho cha sauti ulichokiweka si ndiyo nikaanza kukisikiliza!..... Kumbe ofisini kwangu kuna mwanachama wa CUF, alipomsikia mwanachama mwenzake anamwaga lugha akanitusi kwa kuniambia "Unapenda sana kututania sisi wana-CUF mbona CCM wapo wengi %*ˆxx*:hatari:x$x# sana wewe" (kwenye mafyampufyampu nimeficha tusi naogopa BAN).


hahahahaha I have 3 Crids sijui ndio nini? my daily blead
 
Katika hali isiyo ya kawaida katika kesi ya kupinga matokeo katika jimbo la Igunga ambapo Mbunge P. Kafumu alipita kwa njia za panya huku mpiga debe wake akiwa ni ########## - Mwigulu Nchemba amepelekea wanachama wa CHADEMA kufungua kesi ya kupinga ushindi huo wakiongozwa na Mwl. J. Kasindye ambaye alikuwa mgombea kwa tiketi ya CHADEMA.

Katika mahakama ya mjini Nzega ambapo kesi hiyo inasikilizwa, jana kuliibuka kizaa zaa baada ya ######## kuitwa kutoa ushahidi wake na kuanza kujibizana na wakili wa mlalamikaji ambaye ni Prof. Safari na hatimae Mwigulu akaanza kuongea chake ndipo Prof. Safari akamwambia "Kama huwezi kuongea kiingereza chagua moja kati ya kukaa kimya au kuongea kiswahili kwani mimi nikiongea kiingereza hapa huwezi kuendelea kwani wewe si mwanasheria hivyo kiingereza cha kisheria hukijui"

Kesi hii inaendelea kwa mfululizo katika mahakama ya mjini Nzega....

Mkuu A. D. Pigangoma unaweza kabisa kuwasilisha ujumbe wako kiustaarabu na kwa heshima yako na jukwaa hili
Vinginevyo JF itakuwa sasa kama kijiwe cha wahuni na kupunguza nguvu ya hoja zetu
 
Last edited by a moderator:
kweli wakati akiwa ilboru matangazo ya asubuhi kwa kiingereza mimi nilikuwa simuelewi mwigulu nchemba.alikuwa hajui kupanga maneno mimi nilikuwa nasikia mtu akinunguna na lugha ya kikwao hahahaha
 
Mimi siwezi kuwa mwanasiasa wala kiongozi wa dini. Vitu hivi viwili vinaharibu akili za watu. Siwezi kusimama kila siku kuwadanganya watu! Kijana Mchemba alikuwa Benki Kuu akiwa mtu na heshima na akili zake, ameingia siasa amekuwa garasa kama zezeta hivi na tarumbeta la mafisadi. Kazi zoooote duniani nitafanya lakini si kuwa mwanasiasa. Huyo kiongozi wa dini naye atasimama na kudai, jana nimekutana na Yesu, na Mungu, kaniambia hivi, leteni zaka ghalani, kumbe mfukoni mwake. Nikagundua kumbe ndo sababu ya matapeli hawa hawataki mmoja aingilie kazi ya mwingine. Kwa nini? Sababu wote soko lao moja. Wananchi, na wote wanasema uongo. Wote wanatafuta pesa kwa kudanganya wafuasi wao!
 
Back
Top Bottom