Mwigulu Nchemba: CHADEMA itakufa 2015

Nionavyo mimi kufa kwa chama nikukosa wanachama na chama kukataliwa na wananchi, jee ichara hizi nani mwenye nazo kati ya chadema na ccm?.

Realty nikuwa ccm ndio iko coma na sio leo hupata unafuu kwa kuokolewa na Zec na Vyombo vya Dola bila ya kutumia kilinge hicho tungrkuwa tayari tumesha ifanyia feneral.
 
Tunashauri serikali na chama tawala, shughulikieni matatizo ya wananchi badala ya kutumia muda mwingi na rasilimali nyingi kudhoofisha/kuua upinzani. Mnaacha rasilimali zetu na pesa zetu zinatoroshwa huku mkiwapa kinga MAFISADI wanaoifilisi nchi na kutuongezea ugumu wa maisha. Tunaomba mtubadilishie wimbo sasa, tumechoka kuwasikia kutwa kucha mnapambana na CHADEMA badala ya kupambana na UMASKINI, MARADHI na KUFUTA UJINGA.
 
namuunga mkono mh.mwigulu maana kwa ukabila,na ukaskazini wa chadema hawawezi fika 2015 wakiwa salama.ubaguzi,chuki na choyo ndo unaokiua chama na si mwigulu wala ccm.watanzania wanajua mission na vision ya ya chadema si kuwasaidia watanzania zaidi ya kulinda maslahi ya wakaskazini na familia zao.
 
Malumbano ya vyama hayatusaidii watanzania tumepigika kipindi kirefu tunahitaji mabadiliko
 
Malumbano ya vyama hayatusaidii watanzania tumepigika kipindi kirefu tunahitaji mabadiliko
 

Huko mbali sana chadema chali 2014
 
Mbona mnanichanganya, huyu ni Mwigulu Nchemba au Lameck Madelu Mkumbo?. Mbona Mwigulu Nchemba ni msukuma yupo igunga anachunga mifugo yake?,
 
Atakufa yeye na domo lake refu. Hana adabu kwa wazee huyo.
 
Mwigulu, kulikoni! Mbona unapingana na ule utabiri wa awali wa mnajimu mwenza aitwaye S.M. Wassira?

Hii inathihirisha wazi kuwa ni ukweli usiopingika kuwa PM-7/Msalia na akina Shibuda ulikuwa ni mpango-mkakati wa kutegemewa wa CCM kuivuruga CHADEMA. Maana kwanini sio tena ndani ya mwaka mmoja kama alivyodai kwa majigambo Waasira Mei 2012?

Tanzania sio mali yenu, na ratiba yake haiko mikononi mwenu tena!
 
aka mkosa chama tatizo la Watz tunashabikia tusilolijua kwani hamjua vita iliyopo cdm? kama hamjui hicho chama cha wachaga mtadanganyika mpaka lini fuatilieni mtaona au ni chama cha mzee Mtei

Na wewe tukuite Great Thinker? Kama CDM ni chama cha wachagga na CCM ni cha watu wa kabila gani? Naona wewe ni mchumia tumbo uliye kwenye 'paylist' ya kina Nnauye na Mchemba usiye na uchungu kabisa na nchi yako! Toa data za kusapoti allegations zako la sivyo watu watatilia shaka uwezo wako wa kufikiri.
Ufisadi, rushwa na tamaa ya kutawala milele imewapumbaza CCM na kuwafanya waweweseke mithili ya mtu aliyepata ile dawa ya usingizi inayoitwa Ketalar ambayo aliyepewa huweweseka na kusema maneno kibao yasiyokuwa na maana yoyote! Statements kama hizi zinakivunjia hadhi chama kikongwe na mashuhuri hiki chenye historia ya kuzalisha watu mashuhuri walioitikisa Afrika na dunia!
Hivi kweli CCM imeshindwa kabisa kujifunza chochote toka kwa waasisi wake ambao busara zao zinakumbukwa hadi leo au ni upofu uliosababishwa na kufakamia ufisadi? Mwasisi wa chama chao Hayati Nyerere (RIP) alifanya juhudi za kuwafunda dhidi ya ubepari ndiyo kwanza sasa wameukumbatia na kamwe hawataki kuuachia hata kama utawagharimu roho zao na za waatanzania wengi! Aliwaonya juu ya udini na ukabila na sasa ndiyo waumini wazuri kabisa wa siasa hizo! Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa.
Watanzania tuamke sasa mchawi wa chuki zinazojitokeza sasa katika jumuiya ya watanzania ya kuhujumiana kiimani na pengine kubaguana kwa misingi ya ukabila, udini na matabaka ya walio nacho na wasio nacho ni dude hili linaloitwa CCM na kamwe hatutapumua mpaka ling'olewe litupwe linakostahili - motoni.

 
kiwewe cha 2015,anajua jimboni kwake ni pachungu sasa hivi!!!Tundu Lissu amesha mwanga sumu!!!
 
Wazanzibar wamesema wamechoshwa na tabia ya CCM bara kuwapereka Dodoma na kuwachagulia Rais sasa wanataka wao kama CCM zanzibar watakuwa wanachagua wao Rais wamtakaye siyo kuburuzwa na CCM bara! Mimi naona sasa CCM imeishikwa pabaya sasa ndo mwanzo wakufa hiki chama! Na hawana ubavu wa kuwazuia ngoja tuone hii ngoma ninani ataicheza!
 

Nasikia kwamba Mheshimiwa Mwigulu Mchemba ni mchumi mwenye shahada ya uzamili. Sitarajii mtu wa aina hiyo atoe kauli hii: "hakuna rasilimali ya wilaya fulani." Namshauri aliombe radhi taifa. Vinginevyo tutaiomba seneti ya chuo kikuu kumvua kofia ya uzamili. Rasilimali za nchi hii ni maslahi ya wote. Hivyo, kila rasilimali ni ya wilaya fulani, japo sio ya wilaya fulani pekee. Kwa mfano maji ya Victoria ni rasilimali ya wilaya fulani, japo sio rasilimali za wilaya fulani pekee. Ni vivyo hivyo kwa rasilimali zingine. Angeuelewa umantiki huu, nadhani hotuba yake ingekuwa yenye kujenga ukweli badala ya ghiliba. Nasubiri kusikia toka kwake.


 
Ndugu zanguni,

Kama mjuavyo ndani ya chadema kuna mgawanyiko wa kutosha na tayari tuna team tatu ambazo zimejigawa kikanda., Hii ni moja ya dalili kuwa Chadema itasambaratika mapema kuliko wengi tulivyofikiri

Sababu kuu ya kusema haya ni hili suala la mahesabu na uchaguzi ndani ya Chadema

Tayari tunajua kuwa Chadema wameingia kambini kuchakachua mahesabu ili wayawakilishe kwenye kamati ya bunge ya mahesabu huku yule aliyewaitisha mahesabu haya akiwa tayari ana data zote za haya mahesabu hivyo hata wakichakachua vipi wataishia kuumbuka tu.

Suala la uchaguzi litaibuka upya soon kwani vijana tayari wameishaanza kuwashitukia viongozi waliopo kuwa ni matapeli.

Nawashauri makamanda wasikubali kufanywa misukule na kudanganywa kitoto bali wasimame na kudai uchaguzi ili wachague viongozi wanaowataka.

TUSUBIRI MHESHIMIWA JEMBE ARUDI KUTOKA SAFARI ......

JITAMBUE




 
Same as CCM... wakisha toa Majina ya waliolimbikiza MALI USWIS; Utaona jinsi gani watakavyoanza kugombana...
Na Pesa nyingi ni zile walizopewa na Mchina...

Mbona CUF haina Uchaguzi na Bado Inapendwa huko ILIKO? Ukiangalia VYAMA VINGI VYA KISIASA havina VIONGOZI wa kuchaguliwa kila baada ya miaka kadhaa... Ni hapa tu TANZANIA bado tuanafuata ile tabia ya KI-CUMMUNIST kama CHINA kubadilishana VIONGOZI kama MASHATI... kwani Rais KIKWETE alipita kwa kupendwa au kwa Mizengwe? Mkapa alipita kwa kupendwa au MIZENGWE??? all those are COMMUNIST IDEOLOGIES...

Nipe Chama Chochote Duniani kinachochagua Viongozi wake kwa Mihula kama CCM na CCCP ??? HAKUNA>>>

Mnajua ya kuwa CHADEMA wakichagua VIONGOZI hawatakuwa wa kubebwa kama wa CCM na wanaweza wakawa sio wenye NGUVU kama wa sasa hivyo RAHISI kukipindua...
 
View attachment 117860
View attachment 117863

Wewe unazungumzia Kufa kwa CHADEMA wakati CCM imeishakufa kitambo kama picha zinacyoonyesha migogoro katika jumuia zake mbalimbali, je Unaweza kuufahamisha umma katika migogolo iliyotokea katika hizo picha kuna ufumbuzi wowote ulipatikana?
Kiuhalisia hizo picha zinaonyesha Misukule ya CCM ilivyo na uchu wa Madaraka.


View attachment 117864

Misukule ya CCM inataka kuuawana katika hizo picha hapo juu huku wenzao kicheko kwa kwenda mbele.
 
nani atatoa majina ya uswis?hakuna atayetoa majina ya uswiss ni sawa na kutoa majina ya wauza unga,Mheshimiwa hata juzi nilisikia anasema yatajeni majina ya wauza unga,wakati alishasema anayo,haki ya mungu hii nchi yetu sijui wananchi wake nao ni wendawazimu ama viongozi wanatuona wendawazimu,
 
Tatizo ni huyo mnayemuona mtakatifu Slaa wa karatu

Hivi wewe kweli na akili zako unakenda kuchangia mafuta ya chopa wakati hata baiskeli huna?

Hawa jamaa wanawachuna bila huruma lakini kwa sababu mko kwenye msukule mode inakuwa ni vigumu sana kushtuka, lakini naamini iko siku mtajitambua tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…