Mwigulu: Mimi ni Nyerere

Mwigulu: Mimi ni Nyerere

Hakika anastahili. Ni Mtanzania, Msomi, Ana uzoefu na nyadhifa mbalimbali nchini, ni mwanasiasa anayejua demokrasia na anaejua kushughulikia matatizo ya nchi na wananchi, ni Mzalendo.

Hizi sifa zote alikuwa nazo Mwalimu!

Ni gaidi sifa ambayo mwalimu hana
 
Hapana bana. Hata mimi nilimwona na kwa mara ya kwanza nilivutiwa kumsikiliza kwa makini sana. Aliongea kwa uangalifu mkubwa na ukomavu sana. mwandishi ndiye aliyetaja maneno hayo kwamba anasikia akipita huko mitaani watu wanamsema au wameandika kwenye kuta kuwa Mwigulu ni Sokoine wa pili au Nyerere. Alichofanya Mwigulu sio kujisema bali alikazia kwamba amekuwa akitajwa hiyo tanu akiwa shule ya msingi, sekondari, vyuo vikuu na hata kwenye kwenye makongamano kama Nirobi. Si sahihi kumchomekea maneno mdomoni mwake kwa sababu tu mnatofautiana naye. Hata mimi sina lolote la kuambatana naye kwa vyovyote. In fact nilimchukia sana kwa ufyatu wake dhidi ya vyama vya upinzani, lakini amejipambanua kwa namna anavyoangalia watu wanataka nini kifanyike kwa manufaa ya Taifa na hapo naanza kumwangalia kwa jicho tofauti na mwanzo. Sina maana kwamba nampigia debe na uraisi anaosemwasemwa, lakini siku hizi hafanani na tabia za CCM kwa kuwa ukweli ndio anaoutaka uonekane kwa sasa hata ikibidi kwenda kinyume na chama chake anachokiongoza. Kama ni usanii tutayaona tu mbele maana kama halipo kwenye damu hawezi kujifanya hana mguu milele, akichoka atatembea kwa asili yake.
 
Huyu jamaa ana tuhuma nyingi sana, hawezi kuzikwepa
Lazima kwanza arudi Igunga akaombe radhi kwa yale aliyoyafanya wakati wa kampeni za ubunge.
Lazima arudi pia Arusha akawaombe radhi wananchi wa kule kwa yaliyotokea
Lazima arudi Singida akaombe msamaha kwa yale yaliyotokea huko.

Tukishasikia kauli za kumsamehe toka wa wananchi wa majimbo haya - basi na sisi watanzania wa ujumla tutamfikiria kumsamehe.

Kiukweli wananchi tulikwazika sana na huyu jamaa - hadi wengine wakampachika jina la SAVIMBI. Siasa zilikuwa zinampeleka kubaya inawezekana kaanza kujistukia kwamba alianza kupoteza dira.
 
Mwigulu kwanza ataje watu waliochukua pesa za Escrow Account kutoka Stanbic bank kwenye sandarusi, visalfeti, viroba na lumbesa, hata kama ni mawaziri wenzake au mabosi wake, ndipo aanze mchakato wa kujiita majina ya watu wengine.
 
Mimi pia huku Kijijini kwetu naitwa Nyerere. Hebu nyie wapambe wa huyo mjinga anzeni na Mimi kunitangaza KUGOMBEA URAIS. Ebooo
 
Mijitu mijambazi inaweza kikaa majukwaaani na kujifananisha na mwl.Kambarage?hivi kwl serkali ipo watu hawa wanamdhihaki mwl.Hivi???

Huyu jamaa ni zero brain kabisa, mwanzo alikuwa anajiita Sokine, sasa amejipandisha cheo hadi kuwa Nyerere! Nyambafu Mwigulu.
 
Kumfananisha mwigulu na nyerere ni ukosefu wa akili, mwigulu hana chembe hata moja ya unyerere. Asingefanya kazi na wezi wenzie.
 
Waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba asema watu wanamfananisha na hayati baba wa taifa Julius Nyerere kwakuwa anasimamia maswala yenye maslahi kitaifa bila uoga

CHANZO: NIPASHE

Insanity atits best

Huyu jamaa ni zero brain kabisa, mwanzo alikuwa anajiita Sokine, sasa amejipandisha cheo hadi kuwa Nyerere! Nyambafu Mwigulu.

Baadae utasikia mimi ni kama Mandela mara Mimi ni K. Nkurumah akimaliza Africa atahamia Ulaya.

Chezea kuuwa watu at the sametime unajidai wewe ni mcha mungu, akili lazima ikae upande
 
Hakuwahi kuomba msamaha kuwa mauaji kwa kutumia bomu yaliyotokea Arusha kwenye mkutano wa Chadema hakuhusika!! Cheo chake kakipata kwa Juhudi za kutukana watu na kuua! Anachokifanya kwa sasa kwenye jamii ni Mtakatishaji wa mauaji kuwa mtu wa mikono safi!!
 
anatakiwa afanye kazi ili baadae watanzania wamkumbuke kama mwigulu sokoine hakujiita nyerere na wala nyerere hakujiita jina la mtu mwingine aache kutafuta sifa magazetini
 
Hata shetani naye huwa anajifananisha na Mungu,
kwa hiyo si jambo geni kwangu.
 
Jitu halina aibu hili

Huyu kijana mpuuzi na limbukeni asiye na mfano....

Juzi nimepita pale vigwaza kwenye daraja la train inayopita juu chini MAGARI nikaona kwenye kingo za daraja wameandika Mwigulu 2015 kote kote tena kwa wino Wa kupuliza(spray)

Nilijiuliza Sana kufanya rafu zile sehemu za umma hilo ni moja tu Kati ya mengi yafanywayo na huyo mnyiramba mshamba Wa wakutupwa.....
 
Juzi nilikua safarini, nilipopita pale Ruvu kuelekea Chalinze kuna daraja ambapo treni inapita juu, kuangalia juu ya ukingo wa lile daraja kuna Mpuuzi kaandika MWIGULU NDIO RAIS 2015. Nikacheka tu maana huyu jamaa ana ndoto za ajabu mno.......na huku ni kuchafua mazingira yetu, huwezi kuandika ujinga kama huu kila mahali. I hate it.
MANI zumbemkuu Chakaza tpaul na wengine huyu kijana ni mzima kweli?

mkuu Elli kuanzia sasa kuelekea uchaguzi wa oktoba tutasikia mengi...unajua kuna wengine wanatumiwa kama kondomu lakini wakisha kutumika watatupwa. kwa hiyo, usishangae kuwaona watu wazima na akili zao wanajitoa akili na kuota ndoto za mchana. mwigulu kafanya nini hadi ajifananishe na nyerere na kufikiria kuwa rais wa nchi hii? msimu huu hata vichaa watataka kuingia magogoni. jk ameufanya uraisi wa nchi hii uonekane ni rahisi sana. heshima ya ikulu imeshuka sana kipindi hiki cha jk.
 
Last edited by a moderator:
Mpwa wangu MANI alipata kusema hivi OCTOBER KAWIA KUFIKA TUONE MENGI hahahhaaaa ni kweli tutaona mengi hadi itakapofika October

Ione pia na BAK
mkuu Elli kuanzia sasa kuelekea uchaguzi wa oktoba tutasikia mengi...unajua kuna wengine wanatumiwa kama kondomu lakini wakisha kutumika watatupwa. kwa hiyo, usishangae kuwaona watu wazima na akili zao wanajitoa akili na kuota ndoto za mchana. mwigulu kafanya nini hadi ajifananishe na nyerere na kufikiria kuwa rais wa nchi hii? msimu huu hata vichaa watataka kuingia magogoni. jk ameufanya uraisi wa nchi hii uonekane ni rahisi sana. heshima ya ikulu imeshuka sana kipindi hiki cha jk.
 
Last edited by a moderator:
Huyu kijana mpuuzi na limbukeni asiye na mfano....

Juzi nimepita pale vigwaza kwenye daraja la train inayopita juu chini MAGARI nikaona kwenye kingo za daraja wameandika Mwigulu 2015 kote kote tena kwa wino Wa kupuliza(spray)

Nilijiuliza Sana kufanya rafu zile sehemu za umma hilo ni moja tu Kati ya mengi yafanywayo na huyo mnyiramba mshamba Wa wakutupwa.....

mkuu iyo spray imechafua mpaka kwenye majabali ya mlima wa senkeke na majengo mbalimbali yaliyopakana na barabara kuu ya kiomboi nk.
yani neno hilo hilo linaandikwa kila mahali naamini ni mtu mmoja amelipwa kufanya kazi hiyo.
 
Back
Top Bottom