Mwigulu: Mimi ni Nyerere

Mwigulu: Mimi ni Nyerere


mkuu iyo spray imechafua mpaka kwenye majabali ya mlima wa senkeke na majengo mbalimbali yaliyopakana na barabara kuu ya kiomboi nk.
yani neno hilo hilo linaandikwa kila mahali naamini ni mtu mmoja amelipwa kufanya kazi hiyo.

Halafu kwa ujinga huo ndo anajiamini anaweza kuwa rais?

Hivi mbona hawa hawakemewi? Hata mi nilipoona vile nilijua tu huyu MTU katumwa makusudi yaani kila apitaye na gari pale atamwona....

Jamaa mshamba Sana Kama nduguye Nyalandu anayelindwa na askari Wa wanyama pori utafikiri yeye faru...

Too low....
 
Huu ujinga hawezi kujifananisha yeye mwenyewe aache watu ndio wamfananishe. Nyerere na Sokoine hawakuwa wanawazushia watu kesi za kijinga za kigaidi kama alivyofanya yeye. Bora angejifananisha na nyoka
 
Juzi nilikua safarini, nilipopita pale Ruvu kuelekea Chalinze kuna daraja ambapo treni inapita juu, kuangalia juu ya ukingo wa lile daraja kuna Mpuuzi kaandika MWIGULU NDIO RAIS 2015. Nikacheka tu maana huyu jamaa ana ndoto za ajabu mno.......na huku ni kuchafua mazingira yetu, huwezi kuandika ujinga kama huu kila mahali. I hate it.
MANI zumbemkuu Chakaza tpaul na wengine huyu kijana ni mzima kweli? lusungo pale ni Vigwaza au ni Ruvu? Kumbe na wewe uliona ule upuuzi eeeh??


Nafikiri ni Ruvu Kama sio vigwaza pamekaribiana hivi...

Niliona mkuu sijui kitu gani kilinifanya niangaze macho yangu pale but nimeona ndo nikaamini huyu kijana anamatatizo ya akili..


anajiona Wa thamani wakati kafanywa naibu Waziri katikati ya mawaziri wengi mbumbumbu....vilaza....low minds na duni....

Hii inadhihirisha pamoja na uduni Wa full ministers hao bado Mwigulu hajawazidi Sifa ndo mana yupo chini yao...

Namwonea huruma mkewe sipati picha adha anazopata kwa ulimbukeni Wa huyu kiazi.....
 
Last edited by a moderator:
Mpwa ngoja tusubiri tuone vioja vya watu kutaka kujivalisha koti la Unyerere wakati hawana hata sifa moja ya Mwalimu. Huyu gaidi sijui anataka kumdanganya nani kuhusu rekodi yake ya uongo wa hali ya juu na ugaidi dhidi ya Watanzania.

Mpwa wangu MANI alipata kusema hivi OCTOBER KAWIA KUFIKA TUONE MENGI hahahhaaaa ni kweli tutaona mengi hadi itakapofika October

Ione pia na BAK
 
Waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba asema watu wanamfananisha na hayati baba wa taifa Julius Nyerere kwakuwa anasimamia maswala yenye maslahi kitaifa bila uoga




CHANZO: NIPASHE

achen mzaha jaman hakuna mwanaccm hata mmoja kwa sasa anayeweza kufananishwa na nyerere,jamaa siku hizi kawa komedian wa siasa,hv kweli mwigulu anayeweza kufananishwa na mtakatifu nyerere kwa mfumo upi wa uongozi?kusingizia wtu ugaid na kuvaa sikafu yeny rang flag ya taïfa!!huu ni utan wa kisiasa uliopitiliza,pmj na kubadilika kwake kimtizamo na kimatendo hawez kua kama nyerere wala sokoine!ni ulaghai tu wawanaccm uliozoeleka!!
 
Huu ujinga hawezi kujifananisha yeye mwenyewe aache watu ndio wamfananishe. Nyerere na Sokoine hawakuwa wanawazushia watu kesi za kijinga za kigaidi kama alivyofanya yeye. Bora angejifananisha na nyoka


Hata JK wakati anaingia madarakani 2005 alijinasibisha na Nyerere kadiri mambo yalivyomwia vigumu taratibu akanywea.....
 
matukio ya kigaid yanayoendelea kutokea japo kwa shm ndogo nchin chanzo ni mwigulu kwa tabia yake ya uongo il kuua upinzan similarly alikua anaita ugaid kwa njia za kishetan!mungu hajaribiwi ukisema uongo wa kujinufaisha hutokea il kutambua uwepo wake baadae atakuumbua!ndo mana aliamua kutubu kmykmya kwa Joshua,hata hvyo mungu kamponya kwa tabia ovu ya kuwasingizia wenzie ugaidi!
 
Hata JK wakati anaingia madarakani 2005 alijinasibisha na Nyerere kadiri mambo yalivyomwia vigumu taratibu akanywea.....
Alikosea, alitakiwa kujifananisha na Vasco Da Gama
 
Mwigulu ni kiongozi Anayesadifu Fikra za Nyerere

Viongozi wengi wamekuwa wakinena kuwa wao wanaenzi na kuyaishi maisha ya Mwl. J. K Nyerere ilihali matendo yao ni kinzani na maneno yao.
Akiachia misingi mingi aliyoijenga Mwl JK, lakini aliamini katika dhana kama Ujasiri, Uadilifu, Uwajibikaji, Upendo na Uzalendo.
Mh Mwigulu Nchemba ameweza kuyaishi hayo yote kwa Vitendo.
Ujasiri:
Mwigulu ni kiongozi aliyejasiri na mwenye uthubutu wa hali ya juu kama Mwl, tunakumbuka Mwl hakuweza kuvumilia mtu aliyesema ameiweka serikali yake mfukoni na alimchukulia hatua stahiki, Vivyo hivyo Mwigulu hakuogopa kusema kuwa kuna upotevu wa fedha za umma kupitia mishahara hewa na sasa hatua stahiki zinaendelea kuchukuliwa kwa wahusika pia hakuogopa kuhoji uhalali wa kuendelea kwa BMK kama akidhi haitatosha mbele ya bunge.

Uwajibikaji & Uadilifu

Hakika Mwl alikuwa ni mwajibikaji na mwadilifu, alipinga rushwa kwa Vitendo na alianzisha Azimio la Arusha ili kuwafanya viongozi kuwa more conscious kuhusu uwajibikaji na uadilifu.
Mh Mwigulu ameweza kufuta na kupunguza gharama za chai maofisini na pia sasa ataenda kufanya taasisi zote za serikali kununua magari ya aina moja na ya kati.

Upendo& Uzalendo

Hakuna anayeweza kutilia shaka kuhusu Upendo wa Mwl na Uzalendo wake wa hali juu.
Mwl aliamini binadamu wote ni sawa na afrika ni moja ndio maana alitumia gharama nyingi kuzikomboa nchi zote zilizokuwa bado kupata uhuru wake Mfano Afrika Kusini.
Mh Mwigulu amekuwa ni mtetezi wa wananchi wanyonge na yote ni sababu ya Upendo lakini pia amekuwa akija na mipango mbalimbali ya kuweza kuitoa nchi yetu na kuwa nchi ya kipato cha kati.
Mabadiliko ni Vitendo
Mwigulu anaonesha njia tumwamini makundi yote kwa Urais 2015
 
Ilihali joto likizidi kupanda ndani ya chama chetu cha mapinduzi CCM kuhusiana na utangazaji nia ya Urais,mpaka sasa mh Mwigulu Nchemba amezidi kuwa kielelezo cha aina ya Rais ambaye Tanzania ni lazima iwe naye ili tuweze kuyaona mabadiliko chanya ya uchumi wetu hususani kuelekea nchi ya kipato cha kati pia Mwigulu Nchemba ametuandaa kisaikolojia kuwa nchi pendwa ya Tanzania inaweza kujiendesha bila kuwategemea wahisani na hili linawezekana kwa kukusanya kodi sahihi na kusimamia vema fedha za umma.
Mwigulu amekulia na kuishi katika misingi ya Haki hivyo ni Rais ambaye ana uwezo mkubwa wa kutuunganisha kama Taifa pia ana uwezo mkubwa wa kutatua matatizo na changamoto zinazowakabili wananchi kwa wakati
Mabadiliko Ni Vitendo,Mwigulu for Tz 2015
 
kwa upande wangu hivi ndivyo ninavyomfahamu
Mtafuta Urais wa JMT Mzee Edward Ngoyai
Lowassa a.k.a mzee Mamvi mbunge wa Monduli
mkoa wa Arusha
1) . Namfahamu Lowasa akiwa nyuma yangu
chuo kikuu NI TAPELI NA MSANII BY
PROFESSION
2 . Namfahamu Lowasa akiwa mkurugenzi
AICC Arusha aliyechota hela za WB za
ujenzi wa AICC estates hususan
mabarabara ya estate ya KIJENGE
3 . Namfahamu Lowasa wa Boyz - t 0 -Men
ambao walikataliwa na marehemu JKN kwa
sababu nzuri tu kuwa hawakui
wanajilimbikizia mali kwa kutumia nafasi
zao za uongozi . Au tuseme wanatumia
vibaya nafasi zao za uongozi kwa madhila
ya nchi na wananchi
4 Namfahamu Lowasa wa Richmond na
Dowans
5 . Namfahamu Lowasa ambaye hakukutana
na JK barabarani
6 . Namfahamu Lowasa anaehongo viongozi
wa dini mbali mbali na boda boda ili
uaupate uraisi
7 . Namfahamu Lowasa anaecheza faulo za
uchaguzi Monduli ili mradi CCM ionekane
inashinda na vyombo vya dola vinamlinda
kwenye kufanya hayo
8 . Namfahamu Lowasa mwenye ukwasi wa
kutisha ( aliotuibia kama nchi ) ambao
umefanikisha kuwanunua wajumbe corrupt
wa CC na wa mkutano mkuu ili wampitishe
kwenye kugombea urais .
9 . Namfahamu Lowasa mgonjwa ambae
yuko tayari suala la urais limtoe roho

Tunashukuru kwa taarifa. Ila siku zote ulikuwa wapi mpaka leo ndio utueleze haya? Au tumbo joto la urais
 
Lipumba anasema "Mwigulu huyu ni mtu wa
HAKI,amelitendea HAKI Bunge la
Katiba,ameitendea HAKI hazina kwenye
usimamizi wa fedha na Ukusanyaji wa
kodi,Ametutendea HAKI watanzania kwenye
Sakata la ESCROW,Ameitendea HAKI nafasi
aliyopewa na Mh:Rais,na sisi CUF siku zote
tunasema HAKI KWA WOTE."Profesa Lipumba
anaendelea kumfahamisha kijana mmoja
aliyekuwa amekaa karibu yao kuwa "Mimi
Lipumba ndiye Mwalimu wa Kijana huyu
Mwigulu,Nimepima ajenda zako naona
nizatofauti,Mimi Mwalimu wako nakwambia
Usirudi Nyuma.
You are the best Material in your party.Umejua
matatizo ya Watanzania,Umeona makosa kwenye
Mapato na Matumizi,Unazijua njia za kuyatatua
matatizo haya,Umevaa moyo wa Ujasiri wa
kutetea Wanyonge na Uthubutu ndio maana CUF
tunasema HAKIIIII,Wewe unagusamioyo ya
watanzania wote,Mwalimu wako nasema Usirudi
Nyuma"
 
alianza kujiita sokoine, sasa anataka kuitwa Nyerere, muda sio mrefu atatuambia watu wanamwika nabii, baada ya hapo atasema yeye ni mtume, uchanguzi ukikaraibia zaidi atakuwa malaika, na akishinda uchaguzi atataka kuitwa ana kuabudiwa kuwa yeye ni Mungu.
 
"Hatuwezi kumsamehe tajiri kodi, na kuanza kukimbizana na mama mjane anayeuza vitumbua au matembere"
By lameck madelu nchemba
 
Ukicheza kama ronaldo ukafunga kama ronaldo lazima utaitwa ronaldo tuuu...
Bwanaeeeeh kiukweli huyu jamaa ananikosha sanaa
 
Mwigulu Nchemba
Akumbuka yatima, wenye uhitaji siku yake ya kuzaliwa
*Awataka wenye uwezo kusaidia makundi hayo


Claudia Kayombo

WATOTO yatima na makundi mengine yenye uhitaji maalumu wanatamani huruma ya wengine wakati wote, badala ya nyakati za sikukuu pekee.

Wanahitaji huruma kwa kuwa, wao hawajiwezi kujitafutia mahitaji ya msingi kama vyakula, malazi na mavazi.

Uzoefu unaonesha kuwa, jamii imekuwa ikiyakumbuka makundi hayo nyakati za sikukuu za kidini pekee, huku nyakati nyingine yakisahaulika.

Hata hivyo, wapo miongoni mwetu ambao wanadhani kuwa, jukumu la kuyasaidia makundi hayo si lao, bali ni la watu fulani tu, dhana ambayo si kweli.

Wanayasahau makundi hayo licha ya uwezo wa kipato ambao Mwenyezi Mungu amewakirimia hata kama uwezo huo si wa kiwango kikubwa.

Mtu moja aliwahi kusema, iwapo Watanzania ambao Mungu amewawezesha kipato wangejitoa kuwasaidia wengine, Tanzania ingekuwa mahala salama pa kuishi kwa yatima, wagonjwa wasio na msaada na makundi mengine yenye mahitaji maalumu tofauti na ilivyo sasa.

Jukumu la kuwasaidia watu hao ni la kila mtu na si la mtu mmoja, hivyo kila mtu aone anao wajibu wa kuyasaidia makundi mbalimbali ya wahitaji.

Mapema Januari 7, mwaka huu Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alitembelea Hospitali ya Mwananyamala Dar es Salaam na Kituo cha Kulelea Watoto Yatima, Chakuwama kilichoko Sinza.

Pamoja na mambo mengine nathubutu kusema kuwa,- alijitahidi kutimiza wajibu wake kwa makundi hayo.

Nasema alitimiza wajibu kwa sababu, kama yupo atakayesema alifanya hivyo ni kwa vile alikuwa akifanya kumbukumbu ya tarehe yake ya kuzaliwa, alikuwa akitimiza miaka 40, kwa nini hakufanya kumbukumbu hiyo kwa namna nyingine kwa kuandaa sherehe katika eneo fulani la ufahali akawaita huko marafiki zake matajiri na kisha kula na kunywa nao.

Lakini, aliona ni bora akawaone wagonjwa na watoto yatima, makundi ambayo yanahitaji zaidi huruma ya wengine.

Tuache mambo mengine kando, tutazame ukweli wa jambo hili. Awali, nilisema watu hawa tunawakumbuka mara nyingi katika sikukuu za kidini pekee kama Krismasi, Idi na Pasaka, huku wakati mwingine tukiwaacha wakiteseka.

Iwapo wengi wetu, hususan wanaojiweza kila mtu wakati wa siku yake ya kuzaliwa angetimiza wajibu wake kwa kutoa misaada kwa makundi mbalimbali ya wahitaji, wasingebaki wakiteseka.

Kwa sababu, kama ilivyo kila siku watoto huzaliwa ndivyo zilivyo tarehe tofauti za kuzaliwa za watu mbalimbali nchini na duniani kote.

Akiwa katika hospitali hiyo, alitoa msaada wa vifaa mbalimbali vya kuwasaidia akina mama kwenye wadi ya wazazi. Alifanya tendo hilo la huruma na upendo wakati akitimiza miaka 40 ya kuzaliwa kwake.

Miongoni mwa alivyowagawia akina mama hao wazazi ni sabuni za kufulia, mabeseni ya kuogeshea watoto wao lakini pia alifanya tukio lingine kubwa zaidi la kuchangia damu.

Nimesema ni tukio kubwa kwa sababu damu ni bidhaa adimu katika nyakati hizi, bila kuongezwa damu mgonjwa mwenye hitaji hilo anaweza kufariki dunia.

Hivyo, alichangia msaada mkubwa utakaosaidia kuokoa uhai wa wengine.

Kwenda kwake katika hospitali hiyo pamoja na kutoa misaada hiyo, Mwigulu amekumbana na changamoto mbalimbali zinazoikabili Hospitali ya Mwananyamala.

Uhaba- mkubwa wa wadi zikiwemo za akina mama kwenye hospitali hiyo ni kilio kikubwa, kwani katika wadi ambayo inatakiwa kulaza wagonjwa 18 hulaza- 70 hadi 90.

Kutokana na hali hiyo, Mwigulu anaahidi pia kuvalia njuga kuhakikisha kuwa, changamoto zinazoikali hospitali hiyo na nyingine nchini, zinaondolewa kwani ndiyo India na London ya walalahoi wengi.

Akizungumza na wanahabari muda mfupi baada ya kutembelea baadhi ya wadi hizo, Mwigulu anasema- ataweka mkazo katika ukusanyaji wa kodi kwa wafanyabiashara wakubwa ili kuzimaliza changamoto hizo.

"Nitazungumza na wataalamu wenzangu tuwekee kipaumbele katika kuziondoa changamoto hizi, tusipowasemea jambo hili, mawe yatalisemea kwa sababu hii ndiyo India yao," anasema.

Anaongeza kuwa, ziara yake katika hospitali hiyo ni ya mafanikio makubwa kwa sababu amejionea changamoto zinazoikabili.

Anabainisha kuwa, ili kutatua changamoto katika hospitali mbalimbali nchini, ataelekeza nguvu katika kuhamasisha ukusanyaji wa kodi kwa wafanyabiashara wakubwa.

Akiwa katika Kituo cha Chawama, aliwapa watoto hao gunia la mchele, unga kilo 100, lita 40 za mafuta ya kula, katuni 5 za sabuni za kufulia na mbuzi mmoja.

Ziara ya naibu waziri huyo ilionesha dhahili kumkuna Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Sophinias Ngonyani, ambaye kama ilivyo tabia ya waungwana alimshukuru waziri kwa kutembelea katika hospitali hiyo na kutoa msaada huo utakaoleta chachu na msukumo kwa viongozi na mashirika mengine.

Anasema msaada huo utasaidia kupunguza baadhi ya changamoto za kiafya zinazowakabili katika hospitali hiyo.

Hata hivyo, Dk. Ngonyani anasema changamoto ya uhaba wa wadi katika hospitali hiyo inatokana na uhaba wa eneo, ambapo mkakati uliopo ni kujenga maghorofa katika eneo hilo.

Alisema hospitali hiyo kwa sasa inategemewa na watu milioni mbili, wakazi wa Manispaa ya Kinondoni ambapo miondombinu iliyopo haikidhi mahitaji.

Mmoja wa akina mama wenye watoto, Hidaya Yusuph aliyelazwa katika wodi ya wazazi ambayo Mwigulu alitembelea, anasema ziara ya Naibu Waziri, Nchemba ilitoa faraja kwao.

Anasema iwapo viongozi mbalimbali wangekuwa na moyo kama wa naibu waziri huyo wa kutembelea katika maeneo kama hayo, ingesaidia kuondoa changamoto za wagonjwa na wafanyakazi wengine katika maeneo kama hayo.
 
Back
Top Bottom