Mwigulu: Membe, Sitta Hawatapata Urais

Mwigulu: Membe, Sitta Hawatapata Urais

Status
Not open for further replies.
anaota na kujidanganya kwa utashi upi awe ndo mgombea? kweli naamini nchi haiko salama hata kidogo kama kauli hii imetoka kwa nchemba....tusubiri
 
Ina maana Lowasa akiwa rais Mwigulu Atakuwa Waziri Mkuu!
Bora kutatawaliwa Na mbuzi Kama Hakuna watu Wa kuongoza nchi
 
mwigulu nakuunga mkono 100%,ni lowasa tu 2015,hao wengne ni wanafiki wakubwa membe na sitta,!lowasa lowasa lowasa lowasa hata ukimuuliza mtoto mdogo anajua rais atakuwa edward lowasa 2015

Itakuwa rahisi mno ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko EL kuwa Rais. Take it to the bank!
 
jembe Dr. Saa ndo rais wa nchi na Mwanza si ndo kule kwa Kiwia na yule wa Nyamagana siyo? hayo majimbo magamba msahau ever maboya nyie
 
Hivi ule mkwala wa nape kuhusu wanaotangaza nia kabla ya muda ulikuwa kwa ajili ya wengine tu na sio lowassa? Watanzania wenzangu tukiruhusu mtu huyu kuwa rais wa nchi yetu tutalia na kusaga meno kabla ya kiama hapahapa nchini kwetu tumkatae kwa nguvu zote
Hivi bado kuna watu wanachukulia maneno ya Nape serious.
 
Baada kuulizwa maswali na vijana wa iramba walioko Mwanza kuhusu nyendo za wana CCM kuanza kupigana vikumbo kuelekea 2015 hasa mtoto wa rais kuwa mstari wa mbele kumsaidia mgombea mmoja, Bw. Mwigulu alisema kwamba wanairamba wasidanganyike. Huyo mtoto wa Rais anahaha kuikoa ngozi yake kutokana matendo yakw ya kifisadi. Yeye siyo rais. Baba yake ndio Rais. Rais ni mmoja tu 2015. Na kama walivy idhibit chadema na kuisambaratisha cuf, hao-wengine, sijui, Membe, sijui, sita, wote tutawadhibiti. Rais ajaye kila mtu anamjua. Juzi mmemuona hapa mwanza. Anaitwa rais kabla haja apishwa.
Mwigulu anadhani akili za watanzania zipo kwenye chupa kama zamani?
Asome maandishi yanayosema.. aliyesimama aangalie asije akaanguka
 
Mtu kma huyu sio wa kujadili, maana mnampa mileage bila sababu...huyu sawa na kinyesi ukinya hujui tena kimeenda wapi mwacheni huyu...
 
Ndoto za mchana. Sijui kapewa shs. ngapi. Ni haki yake kubwabwaja. Lakini asipuuzwe. Si wengi wanaemwelewa jinsi alivyo.
 
Karibu tutashudia vita ya wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama cha mafisadi.
 
mwigulu nakuunga mkono 100%,ni
lowasa tu 2015,hao wengne ni wanafiki wakubwa membe na sitta,!lowasa
lowasa lowasa lowasa hata ukimuuliza mtoto mdogo anajua rais atakuwa
edward lowasa 2015

Hata akifa kabla ya 2015 bado atakuwa rais?
 
Binafsi kwa mtazamo wangu namuona Mh Lowasa kama ndio anaweza kuvaa viatu vya uraisi. Achilia mbali propaganda zinazoenezwa na wana siasa kwa ule mtindo wa siasa za maji taka. Unajua alichokifanya Lowasa kwa kuitii na kuitetea serikali ya CCM ndio kilimponza na kuwa hapa alipo sasa. Lakini ni vyema alipoamua kuwa mbuzi wa kafara kwani alijua madhara ya kuanguka kwa serikali hasa kwa serekali changa kama ilivyokuwa wakati ule anajiuzulu uwaziri mkuu.

Binafsi naamini kabisa Lowasa ni mchapa kazi na mtu wa mipango ya kupata maendeleo hasa ya nchi kwa ujumla. Kinachotusumbua sisi kukubali kama Lowasa anaweza kuvaa viatu vya uraisi na vikamtosha ni chuki zetu tulizonazo kwa utawala wa CCM. Kama tukifanya kosa tukamuacha kando basi tujue tutakuwa na miaka mingine kumi ya kupoteza na kuendelea kudorora katika nyanja ya maendeleo katika taifa letu. Tumuunge mkono Mh Lowasa ili atuvushe hapa tulipo sasa, ni kweli Tanzania inamuhitaji sana Lowasa kuliko tunavyodhani sisi kuwa Lowasa anauhitaji sana uraisi. Lowasa anaweza akaukosa uraisi lakini akaendelea na maisha yake na wala asitetereke, lakini kama Tanzania ikimkosa Lowasa kuwa raisi basi itakuwa imepoteza kitu kikubwa sana. Tuunganishe nguvu tumchague Mh Lowasa atuvushe hapa tulipo.
 
Mimi sitampigia kura yeyote ili mradi anagombea kupitia CCM hadi mwisho wa maisha yangu, kiapo hiki nakishuhudia JF...Eeh Mwenyezi Mungu naomba unisaidie.
CCM hatawasimamishe malaika mimi siwezi kumpa kura yangu.
 
Ni heri job lusinde awe rais, kuliko lowasa kuwa rais!

ziara ya obama imembeba sana lowasa kama hutaki hulazimishwi.wengi wanajiuliza iweje leo mitambo ambayo iliharibu sana mustakabali wa kisiasa nchini leo iwe bora?mbaya zaidi wale walioikashifu wameshiriki kwa kila hali ktk ziara ya obama tena na kushangilia wakati jamaa anaenda kuizindua.cdm walishiriki kuiponda mitambo ya dowans,kiukweli kama wanataka kurudisha imani ya watu wanaoanza kumuonea huruma lowasa kuwa alionewa basi na waje hadharani waieleze jamii ilikuwaje na nini kinaendelea.kitu kingine,wautoe huo ushahidi wa bomu la arusha coz bila hivyo watapotezwa sana na ccm.kama mnasubiri mtu mnayemtuhumu aunde hiyo tume ya kimahakama ndio mpeleke ushahidi basi imekula kwenu.cdm acheni imani za kijinga kuwa wananchi watakuwa wanawasapoti tu kwa kila jambo bila kuhoji au kutokubaliana na nyie ktk baadhi ya mambo.ni wakati wa kujipanga upya ili kusonga mbele kwa kasi kubwa zaidi.
 
........Afadhali Yusuph Makamba agombee Urais kuliko.....
 
Binafsi kwa mtazamo wangu namuona Mh Lowasa kama ndio anaweza kuvaa viatu vya uraisi. Achilia mbali propaganda zinazoenezwa na wana siasa kwa ule mtindo wa siasa za maji taka. Unajua alichokifanya Lowasa kwa kuitii na kuitetea serikali ya CCM ndio kilimponza na kuwa hapa alipo sasa. Lakini ni vyema alipoamua kuwa mbuzi wa kafara kwani alijua madhara ya kuanguka kwa serikali hasa kwa serekali changa kama ilivyokuwa wakati ule anajiuzulu uwaziri mkuu.

Binafsi naamini kabisa Lowasa ni mchapa kazi na mtu wa mipango ya kupata maendeleo hasa ya nchi kwa ujumla. Kinachotusumbua sisi kukubali kama Lowasa anaweza kuvaa viatu vya uraisi na vikamtosha ni chuki zetu tulizonazo kwa utawala wa CCM. Kama tukifanya kosa tukamuacha kando basi tujue tutakuwa na miaka mingine kumi ya kupoteza na kuendelea kudorora katika nyanja ya maendeleo katika taifa letu. Tumuunge mkono Mh Lowasa ili atuvushe hapa tulipo sasa, ni kweli Tanzania inamuhitaji sana Lowasa kuliko tunavyodhani sisi kuwa Lowasa anauhitaji sana uraisi. Lowasa anaweza akaukosa uraisi lakini akaendelea na maisha yake na wala asitetereke, lakini kama Tanzania ikimkosa Lowasa kuwa raisi basi itakuwa imepoteza kitu kikubwa sana. Tuunganishe nguvu tumchague Mh Lowasa atuvushe hapa tulipo.

Angalizo
Siungi mkono mambo yanayofanywa na Mwigulu Nchemba kwa kuwa ni hatari sana kwa taifa letu. Naamini hata yeye Mh Lowasa haungi mkono hayo mambo na anamtumia tu kama harakati zake za kuingia ikulu bali akishapata uraisi atamuweka kando na kutenda mambo ambayo kama taifa tutaneemeka na kujutia kwa nini hatukumpata siku nyingi ili atufanyia hayo yote. Hatujachelewa tuchukue hatua.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom