Mwezi umeonekana Saudia

Mwezi umeonekana Saudia

Leo ni mwezi shawal tarehe moja, mwezi wa ramadhani uliisha jana. Mnaoeendelea kufunga Leo mjue mnaafunga nje ya mwezi wa ramadhani.
 
Eid Mubarak ustadhjuma dunia nzima inakula eid leo,ingalia Islamic Chanel ya London inafanya coverage ya nchi mbalimbali duniani. We subiri eid ya bakwataccm
 
Sijui kama unajua unachokiandika, umetawaliwa na jazba tu masikini. Hivi ulisoma somo la geography kweli? Hebu rudi ukaangalie tena suala la MUDA.

Inaonekana hata television za Saudia huwa haangalii. Maana hatujapishana hata dakika 1.
Eid Mubarak
 
Uelewa wako kabla ya teknolojia na LEO hii ni muda gani umekuwa zaid?sasa hivi kusoma Dini ni rahisi kuliko zaman lakin pia mashekhe wazaman walikuwa waadilifu sana LEO hii utaambiwa rais ameshapewa mwaliko wa baraza LA idi bila kuzingatia mwezi utaandama lini.sasa rais hawez kubadili ratiba kirahisi itabidi tu mzibe masikio hata kama mwez umeonekana ili rais ahudhurie.nmemsikia SHEKHE Mohammed IDD kwamba mwez pia umeonekana kondoa eneo LA pai source redio imaan.Mimi sina imani na bakwata baadhi ya mashekhe wameingiwa sana userikali zaid wakaweka Dini pemben bakwata ndo wametudidimiza hawana maendeleo labda maulidi ya kata wilaya na taifa ila tuko pamoja ndugu yangu yote khet

UAMSHO mnatabu sana nyie
Semeni tu mnapenda kula,we nani kauona Mwezi Kondoa?aisee jamaa ongo kweli hili
 
Very simple logic, saudia na Tanzania we're on the same longitude 45E, inawezekana kweli wao kuwa one day ahead of Tanzania? Logically is impossible! !! Kwanza dunia nzima hamna sehemu zinazotofautiana siku nzima haipo! !! Sie tuendelee tu kujifariji ila ukweli ndo huo tarehe no moja dunia nzima ila tunatofautiana kuianza na kuimaliza! !

Mkuu ulienda Madrasa kweli wewe au ndio unafuata Mkumbo?
Issue ni Umbali na sio muda,Kuna Nchi zimeona mwezi kabla ya Saudia,lakini kwanini Mamlaka ya Saudia haipo Tayari kufuata Mwezi ulioonekana nchi nyingine?
Jibu fupi,wanaangalia masafa na kitabu kinavyosema.

Mamlaka ya Saudia inajitegemea na inafuata taratibu zoote,na ndio maana hata kama mwezi umeonekana nchi nyingine wao hawapo Tayari Kufungua hata kwa Polisi,ni lazima uonekane ndani ya Ardhi ya Saudia.La sivyo wakamilishe siku 30.

Halafu usipotoshe watu kwamba Tarehe ni moja dunia nzima,we umeona wapi,au uliruka darasa la nne mkuu?
Sie na Kenya tu Wilson tunapishana dakika kadhaa
 
Inaonekana hata television za Saudia huwa haangalii. Maana hatujapishana hata dakika 1.
Eid Mubarak

Taqaballa Llahu minna waminkum. Hawa ndio wavivu wa kusoma na pia kufuatilia mambo. Wao hoja zao ni zile za "nasikia" kisha anaanza kutoa povu. Enjoy your eid mkuu
 
Taratibu Mkuu Kipilipili, ni kweli sie na Saudi tuko time zone moja lakini muda wa sunrise na sunset hutofautina kufuata latitude kutegemea majira ya mwaka na position ya jua wakati huo; northern or southern hemisphere.

Mkuu nikuulize tu, hebu tuambue Tanzania na Saudia zipo katika latitude ngapi? Tuanzie hapa...

Halafu nikujuze tu, ibada ya swala inazingatia kuchomoza na kuzama jua ILA ibada ya swaum inazingatia muandamo wa mwezi.

Suala la kuchomoza na kuzama kwa jua hata sisi tuliopo ndani ya Tanzania mikoa hutofautiana. Je machweo ya jua kigoma na Tanga ni sawa? Je ikiwa yanatofautiana basi mtu wa kigoma asifunge/kufungua kwa kuwa tu mwezi umeonekana tanga ambako mawio na machweo hutofautiana na kigoma?

Ni wazi jibu rahisi kuwa mtu wa kigoma na tanga watatofautiana tu mida ya SWALA lakini hawawezi kutofautiana kufunga/kufungua kwa kuwa mwezi mwandamo ni mmoja, same to Saudia!
 
Last edited by a moderator:
Sijui kama unajua unachokiandika, umetawaliwa na jazba tu masikini. Hivi ulisoma somo la geography kweli? Hebu rudi ukaangalie tena suala la MUDA.
Kukusaidia wewe na Wenzio tafuta mzoefu atakuambia kwamba hata Arusha tu hapo,kuna minutes wamepishana na Dar.Inahitajika shule ya Zaida hapo kujua hili.

Acheni kukariri
 
Yote kwa yoote.

Watu mmepima.

Wale waliokula leo na kusali EID leo hembu muwauliza kwanini walijifungia ndani wakisubiria wenye EID yetu kesho ili tuwape kampani.

Sasa subirini kesho muone EID inavyokuwa ndio mtajua kwamba kuna wenye EID na waleee wa mwezi wa kwenye Dish la sembe.
 
Back
Top Bottom