Mwenzi mwenye mtoto nje ya ndoa

Mwenzi mwenye mtoto nje ya ndoa

Namba 3&4 huwa muda mwingine inaleta mfarakano ndani ya familia...Sababu ya manyanyaso, husababisha mtoto kumchukia mzazi wa kambo
 
Changamoto ya mtoto wa kambo, alafu use unaishi na Shemeji ambae kila dakika anaona ukimkosoa mtoto wako wa kambo unamuonea ni shida kubwa mno....!!!
 
Mngekuwa mnaoana basi kama mmeshindwa kuachana. Sio mnakuja kuoa/kuolewa na watu wengine afu mnaishia kuwaumiza tu huku bado mnategemea wawalelee watoto wenu kwa upendo. Ikifika stage mnaona mmeshindwana basi amueni kweli sio haya ya kuachana huku bado mnapasha viporo hadi mimba tena. Ahsante kwa ushauri mwaya na Mungu anisaidie
Dada huwa naona una busara na unajitambua kwa kweli. Ungekuwa ni mwanaume ningesema mkeo amepata mume kweli ila kwa vile ni mwanamke nakuombea km huna mwenza upate wa kufanana nae.
 
Dada huwa naona una busara na unajitambua kwa kweli. Ungekuwa ni mwanaume ningesema mkeo amepata mume kweli ila kwa vile ni mwanamke nakuombea km huna mwenza upate wa kufanana nae.
AMEN. Nimepokea mpenzi[emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Hayo yote ni swala la uwazi na makubaliano baina yenu wawili mkimtanguliza MUNGU, tena iwe ni mapema tu baada ya kukubaliana kuanza mahusiano yenu.
Nakumbuka nikiwa bado Mtoto, kuna siku Wazazi wangu walikuwa wanasuluhisha kesi ya rafiki zao...ilikuwa mida ya saa tatu tatu usiku hivi, sisi Watoto tukalazimishwa tukalale, ila tukawa tunazunguka zunguka pale sebuleni (wao walikuwa nje barazani)

Sehemu ya maneno niliyosikia na bado nayakumbuka ni yule Mama alivyokuwa anawaka "uliwahi kuniambia una Watoto?" tena akawa anarudia rudia...na hapo wao tayari wana Watoto wawili.

Sikuelewa saana kwa utoto ule, mimi kilichonivuta ni kuwa kuna ugomvi....ila baada ya kuwa Mtu mzima ndio nimejua kweli jamii ina changamoto.
 
Kabla ya yote natangaza interest; Nilikuwa mwingi saana saana na hao watoto nilozalisha waweza anzisha kijiji chao cha ujamaa. Lakini hakuna mtu anayechukia kulea mtoto wa mwingine ka mimi. Usiulize kwa nini kwani sintakujibu.
Sasa nilipokuja kuoa, nilimkuta binti yupo kwao. Kaja tu likizo shule imefungwa nikachukua juu juu hadi kwangu. Msianze ohhh uliponaje hayo siri yangu lakini Mungai hakunipata. Ingelikuwa Ndali leo ningelikuwa Segerea. Usijaribu.
Tangu siku hiyo nilipompata huyu binti, nimedata. Wivu hadi masikioni unaimba kwangu. Ndo maana sitaki kuwajibika na hao wengine kwani mama zao walinizingua. Siwezi ku shea kifua kimoja na mwingine.
Ushauri.
Tuwekane wazi mapemaaaa kabla ya hatua ya kuishi pamoja. Akiisha ingia nyumbani ukamgundua kuwa alikuwa na mtoto, hakika asikudanganye mtu. Uaminifu haupo.
Ukimfunulia mwenzio mapema, wataitana wazazi wenza wajadili hatma ya mtoto. Uamuzi ukiwa kaa na mtoto basi, ni mwisho wa kuja kumwona au kumletea chochote. Atakuwa wangu kabisaaaa. Sitaki jama kumwona aliyemiibia. Kama aking'ang'ania kuwa anamtaka mtoto wake, achukue kabla hujamchukua mwenzi wako na mawasiliano yakatike hata kama ni nyumba ya jirani na hapo kwenu. Kinyume cha hapo ni kuuendeleza uasherati tu. Mavi ya kale hayanuki na kiporo cha moto ni chakula tu

Asante kwa ku-share uzoefu wako. Nimejifunza kitu.
 
Na kwa nini mkutane kwenye mazingira yanayoruhusu? Umeshajua nia yake, kwa nini unaentertain mitego yake badala ya kuikimbia kama na wewe hutaki kweli kulala naye? Kwa hiyo nyie wanawapaga tu ila mnapokea huku hamtaki?
Reckless men will always put the blames on others
Nimependa ulivyom-cross examine keep it up girl!
 
Wanasema wanawake huona aibu kutongoza lakini wanatongoza kwa vitendo vizuri namna ambayo mwanaume si rahisi achomoke. Elewa kuwa huyo ni mzazi mwenzio sio rahisi umkatalie kuonana nae na awali alishakuambia kuna kitu anataka akuambie.... Mwanaume huwa siku zote ni dhaifu mbele ya penzi, ndo maana Samson alinyolewa kilaini na Delila. Daudi aliangalia chini toka ghorofani akamwona mke wa uria anaoga saa hiyo hiyo akamwita mahali akamshughulikia.
Nimekuelewa sana kaka, jumla ya unachosema ni kwamba, asilimia kubwa ya wanawake ndo wanaopenda kukumbushia penzi kutoka kwa wazazi wenzao. Nadhani hii inatokea kama mwanaume ana hela, kwa hiyo anatoa penzi ili apewe hela. Vilevile wengine kama huyo mzazi mwenzie ndiye aliyembikiri...anaweza kuwa anatamani kusex nae ili kukumbushia, hasa kwa kuzingatia wana mtoto anayewaunganisha.
 
Mkuu lakini wanaume wengi wanachagua kutuficha badala ya kutueleza ukweli kabla,

Mfano mimi nilifunga ndoa ya kikristo sijui km kuna handsome baby boy out there... Mwanangu akiwa na miezi 7 tumboni niligundua tena kwa kukuta SMS yy bado hakuwa tayari kuniambia.

Nilichukua jukumu la kutoa onyo Kali na kumsamehe na pia tumemchukua kutoka kwa mamaye baada ya kutetereka sana kiafya. Tumeamua kuishi nae jumla.

Changamoto ni kwamba mama yaje anataka *eti aje nyumbani kumuona* msimamo wangu ni kwamba akija kumuona mwanae mahali ninapoishi aondoke nae maana sitapenda kuendelea kumuona machoni pangu..

Samahani km nitakuwa nimemkwaza yeyote kwa maneno yangu.

Again am sorry.
Uko sahihi aende kumuona kwa mama yake alipo Hakika yataka moyo
 
Back
Top Bottom