Mwenzenu, usiku leo silali........................ !

Enzi hizo (1982) ndio nilikuwa najifunza kufukuzia visichana kijijini, halafu unatembea kilomita 5 kwenda kijiji cha jirani kufuata walimbwende na tochi yenye mwanga hafifu ukipita katika msitu mnene.............LOL

Wakati huo akina Ngina na Ngano wakiwa wa kusadikika!
 
sobhuza Enzi hizo kulikuwa na:
Maalimu Muhidin Gurumo
Shaaban Dede
Hassan rahani Bitchuka
Michael King Enoch (Marehemu)
Cosmas Chidumule
Abel Baltazari (Marehemu)

Kama sikosei hao wote walikuwa waimbaji, vipi kuhusu keyboard, saxophone, guitar la solo na kadhalika, najua Sikinde uwanja wao wa nyumbani ulikuwa DDC Kariakoo.
 
Last edited by a moderator:
Senksi mkuu, mimi ni kizazi cha dot.com, unaweza kunipa line-up ya Sikinde wakati huo?

Vocals: Maalim Gurumo, Bichuka Hassan, Khamisi Juma, Cosmas Chidumule
Solo: Abel Baltazar, Joseph Mulenga
Rythim: Abdallah Gama
Bass: Mwanyiro Suleimani
Organ: George Kessy
Sax: Ninja King Enoch, Lendi
 
So sad so true..ila walau mi nna nafuu sina shahidi...
Unalo Mtambuzi .....
 
Last edited by a moderator:
Yaani nimekuja kasi kujua kulikoni kumbe wimbo. Haya huwe unajikaribisha kwenye blog yetu ya Mallechela utakuta hizo nyimbo na za kina Kasongo kyanga na Lesi wa nyika
 
Mhhhhh.........yaani we mzee nilikuwa tu nasikia vituko vyako, haya habari ya mkesha wa wimbo wako?
 
oooh mme wangu eee ulinitaka radhi eee wataka oaaa mke mwingine wa pili
uwezo huo wa kututunza unao
aaah aah matokeo ya penzi
umezidi elekea kwa mke mdogo eeh
:ranger:
 
Uzuri wangu wa tausi mama malingo kwetu kawaida,
wenzangu wananisengenya nikipita mara hukonyezana ooo,
wamesahau kazi zao kutwa nzima kunichunguza,
malingo kwetu kawaida hamuwezi kunyamaza ooo.

wasi wasi wako wa nini wacha niseme ukweli,
mwili wangu mzuri kila vazi linakubali,
uzuri wangu wa kuzaliwa malingo kwetu kawaida,
nikigeuka utakubali, nikicheka utakubali nikicheza utazimia wazi wazi... Nimeshindwa kuendeleza, nimesahau.
Mtambuzi huu wimbo uliimbwa na kina nani?
 
Last edited by a moderator:
Vocals: Maalim Gurumo, Bichuka Hassan, Khamisi Juma, Cosmas Chidumule
Solo: Abel Baltazar, Joseph Mulenga
Rythim: Abdallah Gama
Bass: Mwanyiro Suleimani
Organ: George Kessy
Sax: Ninja King Enoch, Lendi

Senkyu mkuu, duru zinaniambia kuwa King Enoch hakuwa mzawa wa Tanganyika, ila alikuwa maestro, yani alikuwa mnoma!
 
Uzuri wangu wa tausi mama malingo kwetu kawaida,
wenzangu wananisengenya nikipita mara hukonyezana ooo,
wamesahau kazi zao kutwa nzima kunichunguza,
malingo kwetu kawaida hamuwezi kunyamaza ooo.

wasi wasi wako wa nini wacha niseme ukweli,
mwili wangu mzuri kila vazi linakubali,
uzuri wangu wa kuzaliwa malingo kwetu kawaida,
nikigeuka utakubali, nikicheka utakubali nikicheza utazimia wazi wazi... Nimeshindwa kuendeleza, nimesahau.
Mtambuzi huu wimbo uliimbwa na kina nani?
TaiJike Wimbo huu bila shaka atakuwa ameimba Juma Nature...........................LOL

Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom