Mwenzako anaweza kuondoka bila kuaga? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenzako anaweza kuondoka bila kuaga?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 31, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,392
  Trophy Points: 280
  Kuna watu katika nahusiano wanaamini jatika kuagana. Wengine hawaamini katika hilo. Siyo katika kuaga tu bali pia katika kuulizana. Kwa mfano, mtu akitaka kutoka anaweza kukuuliza "unakwenda wapi" au kama anarudi unaweza kumuuliza "unatoka wapi au ulienda wapi". Na upande mwingine wa hilo unajisikiaje kama mwenzio anakuuliza hivyo. Anakuona unajiandaa na anajua utamwambia lakini anashindwa kujizuia "unakwenda wapi tena?" anauliza.

  Au kuna kiwango gani cha kuulizana kinaruhusiwa? Kwa mfano, kama unaenda "dukani mara moja" unahaja ya kumwambia mwenzio? Ni mipaka gani ipo kwenye suala la kuagana na kuulizana kabla halijawa kero na kuanza kuleta kisirani?
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwasababu sipendi kuulizwa/uliza "unatoka wapi" napenda tuagane. Hata kama hayupo nyumbani na unatoka kwa zaidi ya saa moja unaweza ukamtext tu kwamba "natoka kidogo, ntakurudi nyumbani baada ya muda fulani". Hivyo hata akifika akakukosa hatokua na maswali ya wapi ulipo, wakati gani uliondoka na wakati gabi utarudi. Na swala la kusubiria eti mpaka mmoja ajipare au avae ndio aseme 'natoka' sio zuri sana. Ni vizuri mkaambiana mapema ,let say kabla ya kuingia bafuni ili kama mwenzako nae alikua na mipango mingine hata kama haikuhusishi (huhitajiki kujumuika nae) ujue na yeye ajue yako kisha mkubaliane kama kuna cha kukubaliana.

  Hata "naenda dukani mara moja", "namuona fulani hapo nje" ni muhimu, you never know what might happen. Unaweza ukakabwa kabari nje au hata ukaanguka mwenzio asijue na wala asiwe na wasiwasi maana anajua utakua jikoni tu au uko humo humo ndani unahangaika na mambo yako.
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Hapo ni kuetegemeana na hesabu za kapo hiyo
  Kama ujuavyo, social life haina marking scheme
  Na wala haina formula kwamba tutafuata 'MAGAZIJUTO'

  ni convinience ya wawili hao
  Mfani kwa mtazamo wangu, sitajali mtu kaaga au hakuaga kama anaondoka ili mradi hajasafiri na simu yake iko ON na ana tabia ya kupokea simu akipigiwa.
   
 4. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kuondoa maswali kama ulienda wapi mbona hujanambia au ujataka twende wote bora uage yaishe.
   
 5. R

  Renegade JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 1,072
  Trophy Points: 280
  Hapa watu hutofautiana sana katika mahusiano, wengine wanatoa nafasi ya kutotaka kuulizwa ili wawe huru, wengine hupenda kuuliza kama aina fulani ya udhibiti wa nyendo zisizo za lazima.Lakini katika mahusiano ya mke na Mume ni lazima ujue safari za mweza wako na wakati mwingine kunaweza kuwa hamna ulazima wa safari mtu akataka kasafiri.Mimi Binafsi toka yangu nyumbani mara nyingi ina usumbufu, ukitaka kutoka wakati mwingine unaombwa utoke na watoto, ukiuliza unaambiwa na wao watembee kidogo! kweli? kama dukani utasikia kwanini usitume mtoto! Namna hiyo, kwahiyo nimejifunza kuwa ninapokuwa nyumbani My wife wangu hapendi nitoke toke na huwa najitahidi kutokuwa na vijisafari.
   
 6. Da Pretty

  Da Pretty JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 3,050
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Sijali wala sichukii kuulizwa,
  lakini mimi asiponiaga kwa kweli inakua ngumu kumuelewa.
  Sijawahi kuishi pamoja na mwenzi lakini sio sababu ya kutoniaga/kunijulisha safari zako.
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kama siishi nae, asiniongezee stress ya kujua safari zake, nami nampunguzia kwa kutomwambia zangu
   
 8. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Hivi kina Asha Rose Migiro nao huwa wanaaga eheee!!
   
 9. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kama tunaishi pamoja ni vizuri kuagana ila ishu ya kutoa maelezo wala haina umuhimu labda mtuaapende mwenyewe kujieleza alikoenda au anakotaka kwenda,

  Km hatuishi pamoja wala sina haja ya kuagwa wala kujua chochote kuhusu safari zake,Ila mie najisikia aman zaidi nikimuaga yeye na kumfahamisha safari zangu au mizunguko yangu,

  Labda km anasafiri ni lzm aniage, lkn mizunguko tu ya mjini wala sihitaji kujua as long as kuna mawasiliano likitokea lolote tutafahamishana.
   
 10. Da Pretty

  Da Pretty JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 3,050
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  We nawe mpana...
   
Loading...