Mwenza wangu ana wivu na usingizi wangu.

leiguanan

JF-Expert Member
Jun 24, 2017
620
1,903
Wakuu mpo salama!

Sawa sawa kama mpo salama nisiwapotezee muda. Nianze kwa kuwarudisha nyuma. Mimi jamii yangu nilikotoka tumegawanyika katika koo.

Na hizi koo kila moja inasifa yake. Nitazipa majina bandia Ukoo wa A huu unasifika kwa kufuga na kumiliki mizinga mingi...huu wengi walevi na ukiingia kwao hukosi asali na pombe yake.

Ukoo B huu unasifika kwa usingizi. Hawa wakilala wanakufa. Hata alale mtaroni na maji yapite atalala bila shida. Na bahati nzuri nipo kwenye huu ukoo na uaingizi naupenda saana saana.

Ukoo wa C huu unaakili za wizi. Yaani wao vyao vyao vya koo zingine ni vyetu. Huu ukoo haupendwi saana maana ni mbinafsi. Ok niishie hapa kutaja koo.

Kikubwa huyu shemeji yenu huwa mara nyingi ananisimulia stori nikiwa kitandani. Ni mtu wa stori mobb saana. Sasa mie kwa asili napenda saana usingizi nikisha kaa kitandani nipe dakika 5 hunipati. Sasa nimekuwa namwacha anaongea mwenyewe.

Kesho nikiamka nakuta amenuna kumsogelea hadi nianze kumbebeleza tena. Huu ni wivu au ni kweli nafanya makosa? maana tukikubaliana silali hadi stori zake ziishe kesho najikuta nimelala tena...Na anapenda kuambiwa usiku mwema kama nini... bahati mbaya kwa week najikuta nimemwambia moja tu...zingine nimepitiliza....

..nawasalimu tena wakuu. Asalaam.
 
Kuna cousin yangu huyo tulikwenda club nilimuacha kwenye dance floor kwenda kuchukuwa bia. Narudi namuona kalala kwenye speaker na makelele yote yale aiseee huyu jamaa akipata upepo tu 😴😴.
Kabila zako:-
A = Mhindi
B = Muarabu
C = Mchagga


Nangatukaa🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Kuna cousin yangu huyo tulikwenda club nilimuacha kwenye dance floor kwenda kuchukuwa bia. Narudi namuona kalala kwenye speaker na makelele yote yale aiseee huyu jamaa akipata upepo tu .
Kabila zako:-
A = Mhindi
B = Muarabu
C = Mchagga


Nangatukaa
Mimi mwenyewe nalala mkuu hata mziki uwe mkubwa.

Kuna siku tulikuwa na part kwa jirani nikaalikwa watu wanacheza ukumbini mimi nipo chumba cha jirani nimelala.

Sipo kwenye makabila tajwa.
 
Mimi mwenyewe nalala mkuu hata mziki uwe mkubwa.

Kuna siku tulikuwa na part kwa jirani nikaalikwa watu wanacheza ukumbini mimi nipo chumba cha jirani nimelala.

Sipo kwenye makabila tajwa.
Mkuu huyu cousin yangu sijui kama unampata huyu jamaa akila analala, wakati wa sala analala tunacheza mpira yeye huwa kipa analala aisee. Siku ya harusi yake tulikuwa na maji ya chupa akifumba macho tu maji ya uso.🤣🤣


Nangatukaa 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Yani mwanamke yoyote ukimgegeda vizur wakati wa usiku no stor wala usumbufu ni kulala hapo hapo sijui we unakwama wapi
 
Mkuu huyu cousin yangu sijui kama unampata huyu jamaa akila analala, wakati wa sala analala tunacheza mpira yeye huwa kipa analala aisee. Siku ya harusi yake tulikuwa na maji ya chupa akifumba macho tu maji ya uso.


Nangatukaa
Ni kibonge?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom