Mwenyezi Mungu anakuona sema Ukweli Wewe uko Kundi ( Daraja ) lipi ( gani ) hapa?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
44,032
2,000
Ufuatao ni mtiririko wa Ufaulu wa Kitaaluma ( Chuo Kikuu ) kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza ( Bachelor Degree ) na tabia ya Mhusika katika Jamii na hata Maisha yake ya baadae.....

1. FIRST CLASS G.P.A

Hawa huwa ni Watu wenye Akili nyingi ila katika Maisha ya Mtaani ndiyo huwa Wafeliji wakubwa.

Pia ndiyo wanaongoza kwa Ubahili na kutokujua kutumia Pesa zao vizuri.

Hata hivyo hawa Watu huwa ni Wakufunzi wazuri katika Vyuo Vikuu kutokana na kuwa Werevu.

Kutongoza kwao huwa ni Mtihani Mzito na hupenda sana ama Kutongozewa au Kutanguliza Pesa wakiwa Wanatongoza na ndiyo Wachunwaji wakubwa na Dada zetu ( Wanawake )

Hawa Uzeeni Kwao ndiyo huja kuwa Wasumbufu wakubwa kwa Watu kwani wao huwa hawapendi Kujijenga kwa manufaa ya Maisha yao ya baadae.

2. UPPER SECOND CLASS G.P.A

Hawa huwa ni Watu wenye Akili kiasi na huwa hawana papara Kimaisha na ni Wasimamizi Watendaji wazuri Maofisini na hata katika Miradi na Biashara.

Ila Wana Kasoro moja Kubwa wanapenda sana Kuchanganya Ushirikina na Kumjua Mwenyezi Mungu ili wapate Mafanikio maradufu ya Kimaisha.

Uzuri wao si Watu wabaya hasa katika Kumsaidia Mtu ( Binadamu ) kama anacho na hawa ndiyo wale ukimuomba Pesa labda Tsh 5,000/= kama anayo anakutumia Tsh 20,000/= na Ukimshukuru na ukimwambia utamrudishia anakuambia hapana amekupa kwa Moyo Mmoja.

Wana bahati mbaya Kubwa moja wanajua Kupenda ila wanaowapenda Wao huwa hawawapendi na ndiyo maana hufa haraka au hujiua au huua kwa Wivu wa Kimapenzi.

3. LOWER SECOND CLASS G.P.A

Kiasili hawa huwa ni Watu wenye Akili nyingi za Kuzaliwa ila si za Kitaaluma ( Shuleni ) na ndiyo huongoza kwa Sapu na Kusapua Vyuo Vikuu.

Tabia yao ya kuwa Werevu Kiasili huwafanya kutaka kujua kila Jambo na Kutotaka kuachwa nyuma.

Wamebarikiwa zaidi Maarifa, ni Wachapakazi mno ila tokea Utoto huwa ni Watu wenye Kupenda mno Utoro, Wezi wa Kalamu za Wenzao, Wapiga Kelele wakuu Darasani. katika Dala Dala hupanda Kuficha au Kutodaiwa Nauli na hata katika Sherehe mbalimbali ndiyo huwa wazamiaji wakubwa.

Akili za Kitaaluma ( Kishule ) wamewaachia wenye First na Upper Second Class ila zile Akili zao nyingi za Asili ( Kuzaliwa ) huwafanya kuwa ni Watu wajanja wajanja ( na hata Matapeli ) wengi hutokea Kundi hili na Sifa yao nyingine Kuu ni Ushawishi ( halafu kwa Kutongoza ni hatari huwa hawashindwi labda tu Upepo umkatae kwa muda huo ) na Kulazimisha jambo lao litokee.

Na ni Watu wa Kujichanganya Kijamii hali inayowapelekea kuwa na Maarifa mengi, kujua vingi na hata katika Uongozi ndiyo hupendwa zaidi na Wananchi wao.

Pamoja na yote ila ndiyo Watu Waoga mno na Mabingwa wa Mikwara ambayo kama ukiiamini kila Siku unaweza ukawa unawaamkia Shikamoo na unawapa Pesa hata bila ya Kukuomba.

Hata Wachekeshaji ( Comedians ) wengi na Wakubwa Ulimwenguni wametokea katika Kundi hili kwani hata Kiasili tu Maisha yao huwa ni Full Vituko.

4. PASS ( GENTLEMAN ) CLASS G.P.A

Hawa Kisaikolojia huwa ni Weak Kiakili ( hasa Kitaaluma ) na hata Mzazi umpige vipi au umtishie vipi utakuwa unapoteza tu muda wako bure.

Akili za Darasani ( Kitaaluma ) hawana ila ndiyo Mabingwa mno wa kujua Kutafuta, Kujituma, hawana Aibu katika Kutafuta hali ambayo inawapelekea Wao kuja kuwa na Mafanikio makubwa ya Kipesa ( Utajiri ) kuliko Wenzao wote.

Na hata katika Suala la Usafi na Kujipenda hawa ndiyo Wanaoongoza na hata wakibahatika kuwa Viongozi ( Watawala ) hutokea Kufanikisha na Kuwainua Wenzao Kimaisha ( Kiuchumi )

Akili za Kitaaluma wamewaachia wengine ila Akili za kujua Kutongoza na kuwa na Wake / Waume wazuri na wa maana wanazo.

Wao huwa si Wazuri Kitaaluma ila ndiyo Watu ambao hupenda mno Watoto wao Wasome na hutoa kila Msaada ili Wafanikiwe.

Sifa yao Kubwa hawa ni huwa siyo Watu Wabinafsi ( Wachoyo ) na kutokana na tabia yao hii ndiyo maana hata Mwenyezi Mungu huwabariki upesi na kuja kuwa na Utajiri mkubwa na Mafanikio ya Kiuchumi kuliko wengine.

Haya mwana JamiiForums jiangalie Mwenyewe hapo upo Kundi gani kisha tutambuane na ikibidi tupongezane na tupeane Pole vile vile.

Nikianza nami hapa nipo katika hiyo #3.
 
GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,558
2,000
OK noted

Siamini unachokiongea kabisa, Unaongelea chuo gani hapa Tanzania?

University of Dar es Salaam ( Udsm) mwaka 2004 mpaka 2006 bila Division one ya Point 8 Form Six na Division one Form 4 kusoma Bachelor of commerce ilikuwa hupati nafasi, Wanaume waliosoma kwa Div one ya point tisa ni wale waliofaulu sana Matriculation Exam

Chuo watu wanasoma kwa semister na matokeo hutolewa mwishoni

Mfano kuna Jamaa ana GPA

First year 4.5
Second year 4.7

Third year ana GPA 2.9

Kwa huyo Jamaa unaweza sema hana akili au

GPA sio kipimo cha uwezo wa mtu

Uwezo wa Mtu unapimwa kwa mchango wake alioacha kuendeleza Taifa

Barack Obama ni Professor na amefundisha sana hata siku moja hajajiita Professor wa Sheria

GPA ni upumbavu wa Tanzania tu

Mimi nina watoto hata siku moja sikuwapima kwa wastani au GPA kubwa

Unaweza ukawa na GPA ya 5. 0 umesoma St Augustine University na watu waliokotwa baada ya kukosa nafasi Udsm plus wote mpo class Sekondari wote mlipata Division 3 au aliyejitahidi Div 2

Unaweza ukawa na GPA ya 2.8 Harvard University umesoma Space Engineering na Unafanya kazi shirika la anga la NASA unarusha rocket angani huyo wa udsm ana GPA ya 4.8 hana lolote hata Practical hajafanya

Fuatilia waliogundua chanjo za Corona uone

Hapo Muhimbili University watu wana GPA hawajui kitu wanasubiri mabeberu wawasaidie na GPA zao za Kawaida sana

Mgunduzi wa Facebook au Microsoft hata waliacha shule

Lakini wanaitwa kwenye Graduation za Harvard kutoa midahalo na wamepewa Degree bila kusoma darasan

Professor Bongo hata kutengeneza kibatali hawezi

Jaji wa Bongo mmmmh......

Jaji Bongo anasema najitoa kwenye kesi Halafu muda wa kukamata ni masaa manne, Baadae pingamizi halina mashiko

Shameless Elimu ya Tanzania

Nilipita Udsm kusoma wakati fulani Masters

Professor pale alikuwa Mark Mwandosya na Mathew luhanga

Na Dakatari alikuwa Dkt Mussa Juma Assad

Udsm nzima walimu waliokuwa wanajua Practical ni Dkt Assad ambaye alikuja kuwa CAG

Mark Mwandosya na Mathew luhanga, Wengine wote ni utopolo tu
 
Tough lady

Senior Member
Jul 24, 2013
118
250
Hici kwanini wabongo tunapenda sana kuomba pesa?? Na unayemuomba akisema hana unamuita bahili au roho mbaya. Tena someyime unakuta watoto wa kiume ndo wapiga mizinga mashuhuri..hivi haifiki sehemu tukaona aibu ya kusema eti fulani ana roho mbaya au bahili hajanipa pesa,,,,..Huoni aibu mru mzima kuombaomba???shameful. Nimeishia ya pili ulipoanza kusifi ma eti ukiomba elf 5 unatumiwa 20..
Kuomba ifike hatua iwe ni aibu..ndio maana siku hizi maadili pia yanaporomoka watu wanafanya mambo ya ajabu kupata pesa as if hawana nguvu z kufanya kazi.
 
KIBIKIMUNU

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
331
500
Hahahahahahahahahahahh hii mada hii loooooh , anyway mleta maada siku nyingine tuleteee uchanganuzi kwa sisi wa certificate in primary education Ila ya MIAKA ileeeee!
 
Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
43,564
2,000
OK noted

Siamini unachokiongea kabisa, Unaongelea chuo gani hapa Tanzania?

University of Dar es Salaam ( Udsm) mwaka 2004 mpaka 2006 bila Division one ya Point 8 Form Six na Division one Form 4 kusoma Bachelor of commerce ilikuwa hupati nafasi, Wanaume waliosoma kwa Div one ya point tisa ni wale waliofaulu sana Matriculation Exam

Chuo watu wanasoma kwa semister na matokeo hutolewa mwishoni

Mfano kuna Jamaa ana GPA

First year 4.5
Second year 4.7

Third year ana GPA 2.9

Kwa huyo Jamaa unaweza sema hana akili au

GPA sio kipimo cha uwezo wa mtu

Uwezo wa Mtu unapimwa kwa mchango wake alioacha kuendeleza Taifa

Barack Obama ni Professor na amefundisha sana hata siku moja hajajiita Professor wa Sheria

GPA ni upumbavu wa Tanzania tu

Mimi nina watoto hata siku moja sikuwapima kwa wastani au GPA kubwa

Unaweza ukawa na GPA ya 5. 0 umesoma St Augustine University na watu waliokotwa baada ya kukosa nafasi Udsm plus wote mpo class Sekondari wote mlipata Division 3 au aliyejitahidi Div 2

Unaweza ukawa na GPA ya 2.8 Harvard University umesoma Space Engineering na Unafanya kazi shirika la anga la NASA unarusha rocket angani huyo wa udsm ana GPA ya 4.8 hana lolote hata Practical hajafanya

Fuatilia waliogundua chanjo za Corona uone

Hapo Muhimbili University watu wana GPA hawajui kitu wanasubiri mabeberu wawasaidie na GPA zao za Kawaida sana

Mgunduzi wa Facebook au Microsoft hata waliacha shule

Lakini wanaitwa kwenye Graduation za Harvard kutoa midahalo na wamepewa Degree bila kusoma darasan

Professor Bongo hata kutengeneza kibatali hawezi

Jaji wa Bongo mmmmh......

Jaji Bongo anasema najitoa kwenye kesi Halafu muda wa kukamata ni masaa manne, Baadae pingamizi halina mashiko

Shameless Elimu ya Tanzania

Nilipita Udsm kusoma wakati fulani Masters

Professor pale alikuwa Mark Mwandosya na Mathew luhanga

Na Dakatari alikuwa Dkt Mussa Juma Assad

Udsm nzima walimu waliokuwa wanajua Practical ni Dkt Assad ambaye alikuja kuwa CAG

Mark Mwandosya na Mathew luhanga, Wengine wote ni utopolo tu
Mkinga umetisha and this thread closed.
 
John Joba

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,102
2,000
Ufuatao ni mtiririko wa Ufaulu wa Kitaaluma ( Chuo Kikuu ) kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza ( Bachelor Degree ) na tabia ya Mhusika katika Jamii na hata Maisha yake ya baadae.....

1. FIRST CLASS G.P.A

Hawa huwa ni Watu wenye Akili nyingi ila katika Maisha ya Mtaani ndiyo huwa Wafeliji wakubwa.

Pia ndiyo wanaongoza kwa Ubahili na kutokujua kutumia Pesa zao vizuri.

Hata hivyo hawa Watu huwa ni Wakufunzi wazuri katika Vyuo Vikuu kutokana na kuwa Werevu.

Kutongoza kwao huwa ni Mtihani Mzito na hupenda sana ama Kutongozewa au Kutanguliza Pesa wakiwa Wanatongoza na ndiyo Wachunwaji wakubwa na Dada zetu ( Wanawake )

Hawa Uzeeni Kwao ndiyo huja kuwa Wasumbufu wakubwa kwa Watu kwani wao huwa hawapendi Kujijenga kwa manufaa ya Maisha yao ya baadae.

2. UPPER SECOND CLASS G.P.A

Hawa huwa ni Watu wenye Akili kiasi na huwa hawana papara Kimaisha na ni Wasimamizi Watendaji wazuri Maofisini na hata katika Miradi na Biashara.

Ila Wana Kasoro moja Kubwa wanapenda sana Kuchanganya Ushirikina na Kumjua Mwenyezi Mungu ili wapate Mafanikio maradufu ya Kimaisha.

Uzuri wao si Watu wabaya hasa katika Kumsaidia Mtu ( Binadamu ) kama anacho na hawa ndiyo wale ukimuomba Pesa labda Tsh 5,000/= kama anayo anakutumia Tsh 20,000/= na Ukimshukuru na ukimwambia utamrudishia anakuambia hapana amekupa kwa Moyo Mmoja.

Wana bahati mbaya Kubwa moja wanajua Kupenda ila wanaowapenda Wao huwa hawawapendi na ndiyo maana hufa haraka au hujiua au huua kwa Wivu wa Kimapenzi.

3. LOWER SECOND CLASS G.P.A

Kiasili hawa huwa ni Watu wenye Akili nyingi za Kuzaliwa ila si za Kitaaluma ( Shuleni ) na ndiyo huongoza kwa Sapu na Kusapua Vyuo Vikuu.

Tabia yao ya kuwa Werevu Kiasili huwafanya kutaka kujua kila Jambo na Kutotaka kuachwa nyuma.

Wamebarikiwa zaidi Maarifa, ni Wachapakazi mno ila tokea Utoto huwa ni Watu wenye Kupenda mno Utoro, Wezi wa Kalamu za Wenzao, Wapiga Kelele wakuu Darasani. katika Dala Dala hupanda Kuficha au Kutodaiwa Nauli na hata katika Sherehe mbalimbali ndiyo huwa wazamiaji wakubwa.

Akili za Kitaaluma ( Kishule ) wamewaachia wenye First na Upper Second Class ila zile Akili zao nyingi za Asili ( Kuzaliwa ) huwafanya kuwa ni Watu wajanja wajanja ( na hata Matapeli ) wengi hutokea Kundi hili na Sifa yao nyingine Kuu ni Ushawishi ( halafu kwa Kutongoza ni hatari huwa hawashindwi labda tu Upepo umkatae kwa muda huo ) na Kulazimisha jambo lao litokee.

Na ni Watu wa Kujichanganya Kijamii hali inayowapelekea kuwa na Maarifa mengi, kujua vingi na hata katika Uongozi ndiyo hupendwa zaidi na Wananchi wao.

Pamoja na yote ila ndiyo Watu Waoga mno na Mabingwa wa Mikwara ambayo kama ukiiamini kila Siku unaweza ukawa unawaamkia Shikamoo na unawapa Pesa hata bila ya Kukuomba.

Hata Wachekeshaji ( Comedians ) wengi na Wakubwa Ulimwenguni wametokea katika Kundi hili kwani hata Kiasili tu Maisha yao huwa ni Full Vituko.

4. PASS ( GENTLEMAN ) CLASS G.P.A

Hawa Kisaikolojia huwa ni Weak Kiakili ( hasa Kitaaluma ) na hata Mzazi umpige vipi au umtishie vipi utakuwa unapoteza tu muda wako bure.

Akili za Darasani ( Kitaaluma ) hawana ila ndiyo Mabingwa mno wa kujua Kutafuta, Kujituma, hawana Aibu katika Kutafuta hali ambayo inawapelekea Wao kuja kuwa na Mafanikio makubwa ya Kipesa ( Utajiri ) kuliko Wenzao wote.

Na hata katika Suala la Usafi na Kujipenda hawa ndiyo Wanaoongoza na hata wakibahatika kuwa Viongozi ( Watawala ) hutokea Kufanikisha na Kuwainua Wenzao Kimaisha ( Kiuchumi )

Akili za Kitaaluma wamewaachia wengine ila Akili za kujua Kutongoza na kuwa na Wake / Waume wazuri na wa maana wanazo.

Wao huwa si Wazuri Kitaaluma ila ndiyo Watu ambao hupenda mno Watoto wao Wasome na hutoa kila Msaada ili Wafanikiwe.

Sifa yao Kubwa hawa ni huwa siyo Watu Wabinafsi ( Wachoyo ) na kutokana na tabia yao hii ndiyo maana hata Mwenyezi Mungu huwabariki upesi na kuja kuwa na Utajiri mkubwa na Mafanikio ya Kiuchumi kuliko wengine.

Haya mwana JamiiForums jiangalie Mwenyewe hapo upo Kundi gani kisha tutambuane na ikibidi tupongezane na tupeane Pole vile vile.

Nikianza nami hapa nipo katika hiyo #3.
G.P.A ndiyo nn?
1. Granulomatosis with polyangiitis(GPA)
2. Grade Point Average (GPA)

Next time ni vyema ukatoa abbreviation ya Key words unazozitumia kwenye uzi wako.
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
44,032
2,000
G.P.A ndiyo nn?
1. Granulomatosis with polyangiitis(GPA)
2. Grade Point Average (GPA)

Next time ni vyema ukatoa abbreviation ya Key words unazozitumia kwenye uzi wako.
Pumbavu acha Kunipangia nini cha Kufanya na kwa Mtu aliyepita Chuo Kikuu ukiandika tu GPA anaelewa na wala hakuna haja ya kuja na hizi Shobo na Sifa zako za Kishamba na Kijuha ulizozionyesha hapa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom