GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,466
- 108,621
Ufuatao ni mtiririko wa Ufaulu wa Kitaaluma ( Chuo Kikuu ) kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza ( Bachelor Degree ) na tabia ya Mhusika katika Jamii na hata Maisha yake ya baadae.....
1. FIRST CLASS G.P.A
Hawa huwa ni Watu wenye Akili nyingi ila katika Maisha ya Mtaani ndiyo huwa Wafeliji wakubwa.
Pia ndiyo wanaongoza kwa Ubahili na kutokujua kutumia Pesa zao vizuri.
Hata hivyo hawa Watu huwa ni Wakufunzi wazuri katika Vyuo Vikuu kutokana na kuwa Werevu.
Kutongoza kwao huwa ni Mtihani Mzito na hupenda sana ama Kutongozewa au Kutanguliza Pesa wakiwa Wanatongoza na ndiyo Wachunwaji wakubwa na Dada zetu ( Wanawake )
Hawa Uzeeni Kwao ndiyo huja kuwa Wasumbufu wakubwa kwa Watu kwani wao huwa hawapendi Kujijenga kwa manufaa ya Maisha yao ya baadae.
2. UPPER SECOND CLASS G.P.A
Hawa huwa ni Watu wenye Akili kiasi na huwa hawana papara Kimaisha na ni Wasimamizi Watendaji wazuri Maofisini na hata katika Miradi na Biashara.
Ila Wana Kasoro moja Kubwa wanapenda sana Kuchanganya Ushirikina na Kumjua Mwenyezi Mungu ili wapate Mafanikio maradufu ya Kimaisha.
Uzuri wao si Watu wabaya hasa katika Kumsaidia Mtu ( Binadamu ) kama anacho na hawa ndiyo wale ukimuomba Pesa labda Tsh 5,000/= kama anayo anakutumia Tsh 20,000/= na Ukimshukuru na ukimwambia utamrudishia anakuambia hapana amekupa kwa Moyo Mmoja.
Wana bahati mbaya Kubwa moja wanajua Kupenda ila wanaowapenda Wao huwa hawawapendi na ndiyo maana hufa haraka au hujiua au huua kwa Wivu wa Kimapenzi.
3. LOWER SECOND CLASS G.P.A
Kiasili hawa huwa ni Watu wenye Akili nyingi za Kuzaliwa ila si za Kitaaluma ( Shuleni ) na ndiyo huongoza kwa Sapu na Kusapua Vyuo Vikuu.
Tabia yao ya kuwa Werevu Kiasili huwafanya kutaka kujua kila Jambo na Kutotaka kuachwa nyuma.
Wamebarikiwa zaidi Maarifa, ni Wachapakazi mno ila tokea Utoto huwa ni Watu wenye Kupenda mno Utoro, Wezi wa Kalamu za Wenzao, Wapiga Kelele wakuu Darasani. katika Dala Dala hupanda Kuficha au Kutodaiwa Nauli na hata katika Sherehe mbalimbali ndiyo huwa wazamiaji wakubwa.
Akili za Kitaaluma ( Kishule ) wamewaachia wenye First na Upper Second Class ila zile Akili zao nyingi za Asili ( Kuzaliwa ) huwafanya kuwa ni Watu wajanja wajanja ( na hata Matapeli ) wengi hutokea Kundi hili na Sifa yao nyingine Kuu ni Ushawishi ( halafu kwa Kutongoza ni hatari huwa hawashindwi labda tu Upepo umkatae kwa muda huo ) na Kulazimisha jambo lao litokee.
Na ni Watu wa Kujichanganya Kijamii hali inayowapelekea kuwa na Maarifa mengi, kujua vingi na hata katika Uongozi ndiyo hupendwa zaidi na Wananchi wao.
Pamoja na yote ila ndiyo Watu Waoga mno na Mabingwa wa Mikwara ambayo kama ukiiamini kila Siku unaweza ukawa unawaamkia Shikamoo na unawapa Pesa hata bila ya Kukuomba.
Hata Wachekeshaji ( Comedians ) wengi na Wakubwa Ulimwenguni wametokea katika Kundi hili kwani hata Kiasili tu Maisha yao huwa ni Full Vituko.
4. PASS ( GENTLEMAN ) CLASS G.P.A
Hawa Kisaikolojia huwa ni Weak Kiakili ( hasa Kitaaluma ) na hata Mzazi umpige vipi au umtishie vipi utakuwa unapoteza tu muda wako bure.
Akili za Darasani ( Kitaaluma ) hawana ila ndiyo Mabingwa mno wa kujua Kutafuta, Kujituma, hawana Aibu katika Kutafuta hali ambayo inawapelekea Wao kuja kuwa na Mafanikio makubwa ya Kipesa ( Utajiri ) kuliko Wenzao wote.
Na hata katika Suala la Usafi na Kujipenda hawa ndiyo Wanaoongoza na hata wakibahatika kuwa Viongozi ( Watawala ) hutokea Kufanikisha na Kuwainua Wenzao Kimaisha ( Kiuchumi )
Akili za Kitaaluma wamewaachia wengine ila Akili za kujua Kutongoza na kuwa na Wake / Waume wazuri na wa maana wanazo.
Wao huwa si Wazuri Kitaaluma ila ndiyo Watu ambao hupenda mno Watoto wao Wasome na hutoa kila Msaada ili Wafanikiwe.
Sifa yao Kubwa hawa ni huwa siyo Watu Wabinafsi ( Wachoyo ) na kutokana na tabia yao hii ndiyo maana hata Mwenyezi Mungu huwabariki upesi na kuja kuwa na Utajiri mkubwa na Mafanikio ya Kiuchumi kuliko wengine.
Haya mwana JamiiForums jiangalie Mwenyewe hapo upo Kundi gani kisha tutambuane na ikibidi tupongezane na tupeane Pole vile vile.
Nikianza nami hapa nipo katika hiyo #3.