Willy,
Sina uhakika kama umeuliza swali, umeshangaa, umehamaki, au hujaelewa unajua mwenyewe.
Ningependa kuchangia, chadema haipendi umasikini inaupiga vita haiutaki wala haitaki kuiusikia.Chadema ingependa kila mwenye kufanya kazi kwa bidii na kupata kipato halali aishi maisha ayapendayo kutokana na jasho lake. Chadema haijawahi kumchukia mtu kwa mali zake, au vito vyake vya thamani alivyopata kwa halali.
Chadema inapiga kelele matumizi makubwa ya serikali pamoja na matumizi mabovu ya mali za yakiwemo magari ya kifahari yanayonunuliwa kwa kodi za wananchi na kuendeshwa kwa kodi za wananchi. Ni kweli kabisa Chadema kinapokea ruzuku kutoka serikalini na michango ya watu wa kawaida.
A) Huwezi kutumia picha ya miaka ya 80 mazingira maisha na wakati ukafananisha na sasa. ndio baba yangu alitembea kwa miguu kilomita ishiri na tano kwenda shule kila siku nakurudi hivyo wanangu watembee?
B) Mbowe ni Mbunge, Mfanyabiashara kama niko sawa magari ya wabunge ni mali yao binafsi na kila mbunge hununua gari alipendalo kwani ni mali yake na analihumia mwenyewe. Pili Mbowe ni mfanyabiashara na anautajiri ambao sijasikia ukipigwa kelele hivyo ni fedha halali ana uwezo wa kutumia gari alipendalo kwa fedha zake.
C) Tuletee ushahidi kwamba gari analotumia Mbowe ni mali ya Chadema. Swala la walinzi naona hapa ni wivu kwenye watu wengi vile unataka Mbowe asilindwe? Swala la walinzi sio mapenzi yake kila mtu angependa kulala bila nondo kwenye madirisha yetu ije kuwa Kiongozi anayetafutwa na CCM usiku na mchana ile wamzuru?
D) Tuletee ushahidi wa matumizi mabovu ya fedha za Chama (CDM) kama unao.
Chadema wakiingia madaraka kwa taarifa yako hakuna mtumishi wa serikali anakuwa na gari la serikali zaidi ya Ikulu. Wengine wote watapewa mishahara wafike kazini kwa ungo, bodaboda watajijua, atakayetaka kununua bajaji au Range kwa mshahara wake hatapigiwa kelele.
Tatizo kubwa la maisha magumu sio Mbowe anaendesha nini au ataendesha nini kama ana uwezo wake binafsi hilo sio shida. Tatizo letu kama nchi ni kuendelea kuwanunulia kina Sumayi, Lowassa, Malecella, warioba nk magari ya thamani ma VX kwa fedha zetu wavuja jasho wakati wamestaafu badala ya kuwapa corolla kuendea sokoni. Wizi, ufisadi na matumizi mabovu ya ofisi kwa manufaa ya watoto na jamaa zao.
Sina matatizo kama unaushahidi yale ni magari ya CDM (VXs) kama huna utakuwa ni wivu wa mtu mzima. Nijuavyo mimi wabunge wa CDM wanamagari yao waliyokopeshwa fedha kila mmoja akanunua na mkopo analipa kila mwezi. magari yale ndio wanajitolea kwenye shughuli za chama. Mbowe anajitolea magari yake binafsi mengi sana kwenye shughuli za chama. Kama hujui fika ofisi za chama ulizia. Chadema wengi wanajitoa kusaidia ukombozi huu.
Chief Mkwawa wa Kalenga