Mwenyekiti wa CHADEMA Arumeru Magharibi ahamia ACT

Hawajawahi kuwa mwenyekiti huyo jmni mienikiongozi jimbo la arumeru huyo msaka madaraka amegombea akapata kura 6 gibson meseyeki akapata kura 115 ndyo akaenda chukua kadi ya chadema tuliyo mpa akawape wanachama anakuja nazo star tv ina maana mwanachama mmoja anakuwa nakadi kumi mwanachama anakuwa nakadi 1 tu unavyo kuwa mwongo lazima uwe na kumbu kumbu mbulula huyo sheshe hajui siasa
 
Mbona sijawahi kumwona mwanachama yeyote wa ccm akijunga act? Ina maana act imeanzishwa kutafuta wanachama wa chadema tu? ACT siyo chama bali ni genge la wahuni tu.
 
laki si pesa kama uchaguzi wa CUF ukifanyika leo hii huko pemba asilimia 100 ya viongozi watakuwa ni waislamu na huo wala si ubaguzi bali ni hali halisi. Ukitaka kushinda uchaguzi Mbeya mjini elewana na wachungaji lakini ukitaka kushinda uchaguzi KUsini Unguja kubalika na Masheikh. Huo ni uhalisia unaotokana na Historia na wala si ubaguzi.

Mnapotetea vyama "vyenu" muwe mnaweka maslahi ya nchi mbele na wala si matumbo yenu FaizaFoxy Asalaam Aleykhum Bibie!!
 
Last edited by a moderator:
Lema ni tatizo chadema arusha..Lema amewafanya wana chadema arusha mazezeta
 
Mshamba ni wew, mwenye macho huoni , maskio hausikiii , umekuwa kama mshumaa unaojiunguza wenyewe kuwamulikia watu wengine , watu wanajenga gorofa , na wengine wananunua majumba wew unabaki unapiga miayo na pipoooss pua

Nimecheka sana , halafu nimekuhurumia mno! Hivi malengo ya WASALITI unayajua dogo? Hivi tajiri wa halali kama mh mbowe atakudhulumu nini fukara wa kutupwa kama wewe ?
 
10547468_706867322727165_8559685884016407594_n.jpg

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema akiwa juu ya jukwaa wakati akihutubia ''umati'' wa wananchi.
10533384_706867169393847_3536350669567458958_n.jpg

''Umati'' wa wananchi ukimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema katika mkutano.

MWENYEKITI wa CHADEMA wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Ernest Sheshe na viongozi wengine 10, wameachia ngazi kutokana na kuchukizwa na vitendo vya rushwa.

Sheshe na wenzake hao wamefikia uamuzi huo baada ya makada wengine kumwaga rushwa ya vyakula na vinywaji kwenye uchaguzi.

Makada wengi wa CHADEMA wamekuwa wakilalamika kuchezewa rafu na wapinzani wao, ambao wanatajwa kubebwa na baadhi ya viongozi wa makao makuu, ambapo vitendo vya rushwa vimetawala bila kukemewa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Sheshe alisema ndani ya CHADEMA hakuna demokrasia na vitendo vya rushwa vinapewa kipaumbele.

Sheshe, ambaye alikuwa akitetea nafasi hiyo, alisema kabla ya kuanza kwa uchaguzi ngazi ya wilaya, wagombea walikuwa wakitoa rushwa na hata taarifa zilipofikishwa makao makuu, hakuna hatua zilizochukuliwa.

Alisema Katibu Mkuu, Dk. Wilbrod Slaa, alituma waraka wa uchaguzi unaowataka viongozi wa mkoa na kanda kukemea vitendo vya rushwa, lakini hakuna kilichotekelezwa.

DK.SLAA
Alisema Katibu wa Kanda, Amani Golugwa, alishindwa kukemea rushwa hata za vyakula kwa kuwa wahusika ni wanaowaunga mkono.
"Wagombea wanagawa mpaka pilau na soda kwa wajumbe na viongozi wanaona ila hakuna hatua zinazochukuliwa kwa sababu ni watu wao. Unakaaje kwenye chama ambacho kimeshika hatamu kwa rushwa," alisema Sheshe.

Pia alimrushia kombora, mgeni rasmi katika mkutano huo, mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, kwa kushindwa kukemea wala kuchukua hatua dhidi ya rushwa hiyo.

Kwa upande wake, Lema alisema madai ya Sheshe ni kutapatapa na kuwa iwapo hakuridhika na matokeo, alipaswa kukata rufani na si kuhama.

Alisema wagombea wote waliridhika na matokeo hayo kasoro yeye na kwamba, chakula kilichotolewa kwenye mkutano huo kwa baadhi ya wajumbe ni fedha zilizochangwa na wajumbe wa mkutano huo.

"Chakula na vinywaji haikuwa rushwa ili mgombea fulani ashinde, bali kiliandaliwa kwa sababu wajumbe wasingeweza kukaa na njaa, aache umasikini," alisema.

Mkoani Tabora nako mambo si shwari kutokana na Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa, Kansa Mbarouk, kujiengua ndani ya chama hicho.
Mbarouk alisema amechukua uamuzi huo kutokana na mambo kutokwenda vizuri huku akiwashushia lawama viongozi wa ngazi za juu kuvunja Kanuni.

Chanzo: Uhuru newspaper
 
Viongozi wakuu wa CHADEMA hawakuamua kwenda kukificha chama kwenye kikundi kinachojiita UKAWA kwa bahati mbaya, la hasha. Mazingira ya kisiasa ndiyo yamewalazimisha kufanya kitendo hicho na kula matapishi yao.

Huwezi kuwa mwanasiasa mlaghai kama huna kipaji katika fikra na mitazamo mipana ya kilaghai.

Baadhi ya Viongozi wakuu wa CHADEMA wamebarikiwa na shetani taranta ya kilaghai. Kila siku wanawalaghai wanachama wao na wananchi kwa ujumla ili waendelee kusimama katika ulingo wa kisiasa ndani ya chama.

Huhitaji kuwa political analyst kutambua hali ya Chadema ilivyo mbaya kwa sasa katika ulingo wa siasa za ndani ya chama na nje ya chama.

Kwa sasa baadhi ya viongozi wakuu wa CHADEMA ambao wanakabiriwa na tsunami ya uchaguzi katika uongozi wao wameanza kutengeneza maigizo ili kuwaaminisha wanachama na wananchi kuwa wanakubarika hata maeneo ambayo wana msukosuko wa kiongozi. Haishangazi kuona hata uchaguzi wa viongozi wakuu wa kitaifa umeahirishwa mara tatu.

Kuna wengine eti wanachukuliwa fomu na wanaombwa kugombea uongozi kana kwamba walishatangaza kuwa hawana pesa za fomu au hawatagombea. Kinachochekesha na kushangaza ni aina ya watu wanaowaomba kugombea. Ulaghai wao umefikia kiwango ambacho kinawafanya hata washindwe kupambanua mantiki ya ulaghai wao.

Kwa nini Wazee kutoka Kigoma na siyo Wazee kutoka Hai?. Why Kigoma?

Kuna angalizo linalosema, mtu mwenye akili, akijua kuwa na wewe una akili akakueleza jambo la kipumbavu na wewe ukakubali atakudharau sana. Hawa viongozi wa CHADEMA wanawadharau sana wanachama wao.

Siasa za kilaghai huishia ukingoni!
 
Mbona Umati wa watu wanasubili 2015 na chaguzi za mitaa kama mwenyekiti wao alivosema wakati wahongwa wakimkabidhi form ya kugombea uenyekiti wa chama hicho .
 
hapo ilikuwa ni kwenye ufunguzi wa tawi.. tuambie ufunguzi wa tawi unahitaji watu wangapi?
 
Hivi kweli yale maisha bora mliyowalaghai wananchi yako wapi?
 
Lema wana arusha wamemchoka baada ya kudidimiza uchumi wa arusha kutokana na mavurugu yake. Wanasubiri uchaguz mwakani wamuondoe.
 
Kama vurugu za mtu mmoja tu zinaweza kudidimiza uchumi wa mkoa mzima, basi hiyo serikali iliyoko madarakani itakuwa ni dhaifu kupindukia.
 
Mbona Umati wa watu wanasubili 2015 na chaguzi za mitaa kama mwenyekiti wao alivosema wakati wahongwa wakimkabidhi form ya kugombea uenyekiti wa chama hicho .
Ndugu,
Siwezi nikashangaa maneno ya Mh. Mbowe kwa sababu CHADEMA kinaongoza nchi ya kufikirika!

Nchi wanayoiongoza imejaa watu wanaowaita wasaliti na mamluki.

Maneno kama wasaliti na mamluki ni kawaida sana kuyasikia yakisemwa na hawa baadhi ya viongozi wa juu ndani ya CHADEMA.

Huwezi kupata maneno kama reality check ndani ya ofisi na fikra za hawa baadhi ya viongozi wa CHADEMA.

Baada ya mwaka 2015, utaanza kuwasikia wakipiga kelele huku wakisema, TUMEIBIWA KURA ZETU.
 
Back
Top Bottom