mwenyekiti wa AU JK kuwasili kenya kusaidia usuluhishi

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,187
671
mwenyekiti wa AU mheshimiwa JK anatarajiwa kuwasili kenya saa yeyote leo hii ktk kuhimiza harakati la suluhu nchini kenya.

hali hii inatokana na kukwama kwa mazungumzo hayo baada ya vyama vyenye kupinzana kutofikia makubaliano ya kugawana madaraka au kupanga majukumu ya nafasi ya waziri mkuu, hali ambayo imeyaweka mazungumzo hayo ktk rehani.

tumuombee JK aweze kusaidia harakati hizo ili ndugu zetu wa kenya wapate amani na ss tanzania tupate kujenga heshima yetu katika harakati za kuleta amani barani afrika

kila la heri mheshimiwa mwenyekiti wa AU
 
Sina hakika kama amejiandaa vipi kusema walipigwa Kiteto na polisi, Komba kukaa eneo la mkutano kwa mabavu na mauaji ya zanzobari na Karume ni Rais hadi sasa.Haya mambo wakenya waliyaona na wanajua hakuna suluhu chini hadi sasa anaruka ruka .Ali kawapa majibu kamili lakini kaziba masikio je Kenya ataweza maana wale hawaangalia makunyanzi wala uzuri.Kila la heri tuone kama anaweza kusema lolote .
 
Tunamtakia mazungumzo mema..

Kila mtu ana Haiba yake na mvuto wake kijamii na kisiasa...Hata Ndoa wapo wanaokuja kusuluhisha uwezi amini kama hao wanaweza...Muhim AMANI ipatikane kwa majiran zetu...
 
Sina hakika kama amejiandaa vipi kusema walipigwa Kiteto na polisi, Komba kukaa eneo la mkutano kwa mabavu na mauaji ya zanzobari na Karume ni Rais hadi sasa.Haya mambo wakenya waliyaona na wanajua hakuna suluhu chini hadi sasa anaruka ruka .Ali kawapa majibu kamili lakini kaziba masikio je Kenya ataweza maana wale hawaangalia makunyanzi wala uzuri.Kila la heri tuone kama anaweza kusema lolote .

Very well said! Mimi nawaona wakenya jinsi watakavyoenda kuchekea pembeni JK akimaliza speech yake. I hope he has a good speechwriter and that he will stick to the text! Asije akawapelekea porojo huko kama kusema "we are all excited about the end of President's Bush presidency". Ilizua mjadala!
Ngoja aende kuboronga huko - heshima yote ya TZ ita-evaporate! Be smart, JK!
 
Very well said! Mimi nawaona wakenya jinsi watakavyoenda kuchekea pembeni JK akimaliza speech yake. I hope he has a good speechwriter and that he will stick to the text! Asije akawapelekea porojo huko kama kusema "we are all excited about the end of President's Bush presidency". Ilizua mjadala! Ngoja aende kuboronga huko - heshima yote ya TZ ita-evaporate! Be smart, JK!

Susuviri hebu niweke sawa .Kulizuka nini umesema ? Kwa nini ulizuka mtafaruku na ulitoka kwa akina nani ?
 
Mheshimiwa JK mimi naamini wewe ni Kiongozi mwenye uwezo mkubwa,na naamini kuwa uko katika grade ya viongozi wenye hekima na busara.
Katika suala la usuluhishi wa mgogoro wa Kenya inakulazimu kushughulikia suala la mgawanyo wa madaraka,bila kusahau kutilia maanani la jinsi uchaguzi ulivyokuwa na dosari zake, na hiki ndicho kiini cha matatizo yote.
Huko kuna utakabiliana na watu wasiotaka kuleta maridhiano kwa kuwa katiba iliyopo inawafanya miungu wadogo.Hawa ni wale wanaomzunguka Kibaki na kumpa ushauri wa kutoleheza kamba.Hwa hawaoni madhara yaliyojitokeza na wala hawaangalii huko mbele kutatokea nini.Staili yao ni kama ile ya Charles Taylor na wenzake,Mobutu Seseseko,Robert Mugabe na wengineo.

Ugumu wa kupata suluhu uko hapo kwa kina Martha Karua,Michuki,Njenga Karume na wengineo.Kama utaweza kumkabili Mzee Kibaki na kumwambia kuwa huko mbele kuna hatari ya kupelekwa kwenye Mahakama ya Kimataifa kwa kuibomoa amani ya Kenya ili kufuata kundi la Michuki na wenzake,ambao walimlazimisha Kivuitu kutangaza matokeo batili,pengine Mzee kwa kuwa ni Mkristo mzuri anaweza kujirudi na kuamua ku save face kwa kukubali na kuridhia hoja ya ODM.
Ujasiri wa kutangaza matokeo ya uwongo ambayo yalisababisha vifo vya watu wengi na kuwaacha wengine wakiwa wakimbizi katika nchi yao ni dhambi isiyosameheka na yote hii itakuwa ni Kibaki na wale wapambe wake.

Sasa iwapo wale waliopora kura watakubali maridhiano basi kuna bima dhidi ya wao kufikishwa kwenye mahakama ya haki za binadamu huko the Hague na watakuwa wamesalimisha nafsi zao.Vinginevyo historia itakuja kuwahukumu kama ilivyofanya kwa viongozi wengi wa aina hii.

Nakutakia kila la kheri JK.

Hao wengine wanaokubeza kuwa hujui Kiingereza wna chuki tu na katika kila nchi wapo.Dawa yao ni kuwapuuza.Kiingereza ndiyo nini??Si ni lugha tu.
 
KIKWETE KENYA.jpg

Mkuu Wetu Kawaeleza Nn Wakenya Nnaona Kimya Hatujui Kilichoongelewa.

Mwenye Nyuzi Atupe
 
wakuu nnaona mwaka huu JK nyota yake itazidi kun'gara maana ndugu zetu wameweza kufikia muafaka ktk kikao alichokioongoza zaidi ya masaa matano.

mungu wa jaalie amani ya kudumu wakenya
 
wakuu nnaona mwaka huu JK nyota yake itazidi kun'gara maana ndugu zetu wameweza kufikia muafaka ktk kikao alichokioongoza zaidi ya masaa matano.

mungu wa jaalie amani ya kudumu wakenya

Naam,

Hongera JK kwa hili! Naona sasa umepata sababu ya kuhalalisha safari zako. Ni vizuri sana kusaidia jirani yako mwenye njaa huku ukiacha wanao wakilala njaa.
 
Naam,

Hongera JK kwa hili! Naona sasa umepata sababu ya kuhalalisha safari zako. Ni vizuri sana kusaidia jirani yako mwenye njaa huku ukiacha wanao wakilala njaa.

Iwapo unapewa chakula bora na unakikataa, huku jirani wanalala njaa,then ni bora kuwapa hao majirani, ili hapo kwako watie adabu kwa kukataa chakula bora, na hii itawasaidia kujua chakula bora ni kipi...
 
kama chakula bora ni buzwagi, richmonduli, wizi bot, nakadhalika basi afadhali kulala njaa!
 
Hongera sana Raila kwa kujitambua kwamba wewe ni nani na kuamua kuhutubia vyombo vya habari vya Kimataifa kwa Kiswahili , kumbe ndiyo maana Wakenya wanakupenda leo ndiyo nimegundua .
 
Karibu tena Tibwilitibwil,
Naona safari yako Uarabuni ulirudi salama, alhamdulillah!
 
Sina hakika kama amejiandaa vipi kusema walipigwa Kiteto na polisi, Komba kukaa eneo la mkutano kwa mabavu na mauaji ya zanzobari na Karume ni Rais hadi sasa.Haya mambo wakenya waliyaona na wanajua hakuna suluhu chini hadi sasa anaruka ruka .Ali kawapa majibu kamili lakini kaziba masikio je Kenya ataweza maana wale hawaangalia makunyanzi wala uzuri.Kila la heri tuone kama anaweza kusema lolote .

Inawezekana akaweza na kwa mujibu wa habari ziliopo ni kuwa Odinga na Kibaki wamekubaliana kuunda Serikali ya mseto( Tanzania Daima, Ijumaa Fe. 29), lakini kwa vyovyote ni aibu kwake na mwenzake BM kwani uliyoyaeleza hapo juu yote ni kweli, suala la Zazibar hadi leo analipiga kalenda - MKONO WENYE KINYESI ANAENDA KUUTUMIA KUSAFISHIA - inawezekana lakini ni aibu.
 
Wacha kulia lia hapa, sio JK wala BM anaepiga kalenda suala la muafaka. Kumbuka kuwa ni vyama viwili ambavyo vinakaa kuandaa muafaka huo, kwa mpango tofauti kabisa na yale yaliotokea huko kwa jirani zetu. Vyama vyenyewe vipo kimya kuandaa muafaka bora, wengine mnalia lia
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom