Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kujiuzulu kama Mwenyekiti wa Azimio

Ikaria

Member
Jul 17, 2019
71
195
Aliyekuwa Rais wa awamu ya nne Uhuru Kenyatta anatarajiwa kujiuzulu kama Mwenyekiti wa Muungano wa Azimio, aliobuni pamoja Mhe' Raila Odinga katika kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita.

Hatua hii ina maana kuwa sasa Raila Odinga na mgombea mwenza Martha Karua ndio watakaondelea kuongoza Muungano huo ambao kwa kiasi kikubwa unaonekana kuwa ndio upinzani rasmi nchini Kenya kwa sasa.

Inasadikiwa kujiuzulu kwa Uhuru Kenyatta kunatokana na Hali halisi kuwa sasa hivi ana jukumu kubwa kama mjumbe wa amani katika Ukanda wa Afrika Mashariki, kazi aliyopewa na Rais William Ruto kuiwakilisha Kenya.

Hatahivyo wapo baadhi ya watu wanaosema Kenyatta anajiondoa Azimio kwani haoni Sababu ya kuendelea kuwa Mwenyekiti wao baada ya Raila Odinga kushindwa na Rais Ruto kwenye Uchaguzi Mkuu.

Kadhalika Kuna wanasiasa wanaosema Uhuru hakuwa mkweli kipindi cha kampeni na kuwa alimsaliti Odinga.

Kenyatta amekuwa akijishugulisha na harakati za kusaka mwafaka na amani hasa kwenye mgogoro unaoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
 
Back
Top Bottom