GE2025 Mwenyekiti CHADEMA Arusha: Mbowe atoke hadharani na aseme 'No reforms No election'

GE2025 Mwenyekiti CHADEMA Arusha: Mbowe atoke hadharani na aseme 'No reforms No election'

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha, Elisa Mungure, ametoa wito kwa Mwenyekiti Mstaafu wa chama hicho ngazi ya taifa, Freeman Mbowe, kujitokeza hadharani na kuunga mkono kaulimbiu ya chama ya “No Reforms, No Election”, kwa kuwa ndiye mwanzilishi wa msimamo huo.

Mungure amesema kauli mbiu hiyo ilianza kutumika chini ya uongozi wa Mbowe akiwa Mwenyekiti wa Taifa, ambapo ilipitishwa na Kamati Kuu ya CHADEMA na kusambazwa kwa mikoa yote ya chama hicho.

Amesema: “No Reforms, No Election imeanzia kwa Freeman Mbowe. Nikiwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa, nililipokea kama agizo la Kamati Kuu. Kwa hiyo kiukweli anatakiwa atoke na aseme kauli hiyo kwa sababu yeye ni kati ya waasisi wa msimamo huo.”

Ameongeza kuwa Mbowe ni miongoni mwa viongozi waliopambana kwa dhati kuhimiza mageuzi ya kisiasa nchini, hivyo ushiriki wake wa moja kwa moja katika kusimamia kauli mbiu hiyo ni muhimu kwa mustakabali wa demokrasia.

Ikumbukwe kwamba Mungure alikuwa miongoni mwa viongozi wa CHADEMA waliomuunga mkono Mbowe wakati wa kampeni za uchaguzi wa ndani wa chama hicho.

Wanaoweza kusimamia maneno yao katika siasa ni wachache,
Pia siasa ni maslahi kama hakuna basi
 
Kuna jambo moja ambalo vyama vyetu vya siasa havielewi. Sio lazima kila mwanachama akubaliane na kila kitu kinachoendelea ndani ya chama. Ni vizuri kwa chama kama wanachama wasiokubaliana na jambo fulani wakinyamaza kuhusu hilo suala na kuendelea kuunga mkono mambo mengine. Inawezekana NRNE ya Mbowe inatofautiana kiutendaji na hii ya Lissu. Wanao taka aite presa kuelezea tofauti hizo ni kumkosea adabu Mbowe. Sawa na kumuita aliyekuwa Makamu Mwenyekiti. Adui wa Chadema anajulikana na sio Mbowe. Wanapoteza nguvu zao kumuandama Mbowe.

Amandla...
 
Mbowe ndiye shahidi mkuu wa siri aliyeandaliwa na dola kumuangamiza Lissu kisha yeye arudishiwe kikoba chake haya yalithibishwa na kibaraka wake na shahidi namba mbili Yericko Nyerere aliposema kuwa tatizo la Chadema ni Lissu wakishamuondoa watarudi Chadema.
 
Kuna jambo moja ambalo vyama vyetu vya siasa havielewi. Sio lazima kila mwanachama akubaliane na kila kitu kinachoendelea ndani ya chama. Ni vizuri kwa chama kama wanachama wasiokubaliana na jambo fulani wakinyamaza kuhusu hilo suala na kuendelea kuunga mkono mambo mengine. Inawezekana NRNE ya Mbowe inatofautiana kiutendaji na hii ya Lissu. Wanataka aita presa kuelezea tofauti hizo.
Kote huku ni kumkosea adabu Mbowe. Sawa na kumuita aliyekuwa Makamu Mwenyekiti. Adui wa Chadema anajulikana na sio Mbowe. Wanapoteza nguvu zao kumuandama Mbowe.

Amandla...
CHADEMA anatakiwa kwenda mbele wakiwa na vision iliyokamilika, Mbowe apumzike. Mazuri yake yatumike na mabaya yarekebishwe ili Chama kisonge mbele kwa umakini. Hakuna Malaika wa kuja kuongoza, wote wana mazuri na mapungufu.
 
Kwahyo anatufunza kwamba Walimtoa sadaka Mwenzao..Kama hyo no reforms no election ilianzishwa na Mbowe..kwanini Mbowe mpaka sasa yupo kimya?utajibiwa sahv ni mjumbe wa kawaida hana sauti.. Kwanini Baadhi ya wapokeaji wa hyo kauli waliamua kuhamia CHAUMMA?utajibiwa waliona haina mashiko... kwamuda ulivoenda hata akisimama sahv haina maana bora atulie... Kataa siasa, siasa ni utapeli wa kifikra.....SIJAONA CHAMA CHA KUNISHAWISHI HATA KIMOJA.
 
CHADEMA wanapoteza muda sana kumuandama Mbowe. Waheshimu tu ukimya wake na wao kusonga mbele na agenda zao. Sio busara kugombana wao kwa wao wakati haitawasaidia lolote kwenye kushika dola. Tatizo CHADEMA lengo lao ni kuendelea kuwa chama kikuu cha upinzani ili waendelee kufaidi ruzuku zinazotolewa na serikali ya CCM.
 
Huu mwaka umesema ukweli Mbowe hakuwa mpinzani halisi bali kivuli alikuwa anakula nao mambo yamekuwa tight watu wapo serious na nchi imebidi akae pembeni. Na ndicho tunachotaka akae pembeni walio serious wachukue kiti
 
Back
Top Bottom