Mwenye uzoefu na Marekani msaada nahitaji

Mwenye uzoefu na Marekani msaada nahitaji

Series na movie za kimarekani zimekuharibu akili , unadhani huko mambo mtelezo?

Wamarekani wenyewe wanaikimbia nchi yao wanaenda kuishi kwenye nchi ambazo maisha yapo cheap ...wenyewe wanaita " off the grid"
 
Piga kibiriti hiyo hela. Huna plan ya maisha yako. Dola 1500 ndo inakupa akili ya kwenda USA (sounds like USA RIVER)???
Manake ukiendelea kukaa nayo itakupa akili ya kwenda akhera/mbingu.
Usa river! Mjomba we kiboko!
 
Siwezi kumshauri mtu aje Marekani kama hana mpango wa kukaa kihalali muda wote atakapokuwa huku.

Sijawahi kuwa out of legal status Marekani hata kwa sekunde moja. Naona uzuri wa kuwa hivyo.

Na naona watu wanavyohangaika sana kwa sababu hawana legal status.
Usiwatishe watu ndugu! Akiingia atapata akili mpya. .
 
Hapa tz huwezi kupata kazi? au hadi utimize ndoto ya kwenda marekani,any way kama kazi ya nguvu utapata,ila unaweza kupora mapato kwenye show za miziki? welcome in Florida gangsters institute,tukupe nataka kama zote
 
hakuna jambo zuri kama kufuata unachokitamani.

maisha ni nini bhana... kama tamaa zako zinakutuma kwenda merekani nenda mzee baba.

Kikubwa viza inaweza kukuharibia mipango maana hao jamaa hawagawi tu...

$3000 ulizonazo zinaweza kukutosha au zisikutoshe... inategemea unaenda kwa viza gani.
 
Kumdharau mtu usiyemjua wala kujua mchango wake katika jamii ni kitu kibaya sana, moja ya sababu ya umasikini wetu.

Mimi napenda kuongea na washua fulani waliokaa kwenye system na wanaojua dunia inavyoenda ili kuchota busara zao.

Nilikuwa naongea na mshua mmoja wa siku nyingi, kasafiri dunia nzima kwa shughuli za kiserikali. Nikawa namuuliza kuhusu hizi attitudes za serikali ya Tanzania kuhusu kuwekeana ngumu kwenye safari (hii ilikuwa kabla ya Kangi Lugola kusema maneno yake kuhusu human trafficking, so it was not about that).

Mshua akawa anasema tuna historia ya ujamaa iliyotufanya tuwe na mamabo haya, pia tuna wivu wivu wa kijinga sana. Amenieleza kwamba hata enzi zao kwenye East Africa Community Wakenya na Waganda walikuwa wanasaidiana sana kukitokea nafasi za kwenda nje kusoma na kutafuta maisha, Tanzania ukijulikana unafanya mipango ya kwenda nje unaonekana kama msaliti.

Baadhi ya hizi attitudes zipo mpaka leo, na hata kama naelewa officially Kangi Lugola anaongelea kuhusu human trafficking, a legitimate issue, unofficially hizi checks zinatumika ku frustrate watu wenye legitimate reasons kusafiri.

Mimi kwetu tuna historia ya kusaidiana muda mrefu sana, kuna watu wamepata kufanya shughuli za maana sana hapo mjini Dar, wamepitia kwetu.Wamekuja mjini hawana pa kufikia lakini kwa sababu ni jirani, rafiki, rafiki wa rafiki huko nyumbani bush, wamepatia sehemu ya kuanza maisha Dar, angalau pa kufikia, halafu, wakajichanganya kivyao.Leo na wao mabosi wakubwa na wao wamesaidia familia zao na watu wengine wengi. Maisha ni kusaidiana.

Sasa mtu niliyekua huku nayaona haya, maisha yangu tu nilivyokua na kuona wazee wangu wanaishi hivi ni fundisho kubwa kwamba usimdharau mtu anayehitaji kuoneshwa njia leo, muoneshe halafu mpe nafasi apigane mwenyewe, akishindwa, wewe ushafanya sehemu yako ya kumuonesha njia, akishinda, hiyo ni habari nzuri.
Tatizo letu wabongo ni pale unapomsaidia mtu anafanikiwa then anakunya juu.kila mtu apambane na khali
 
Ooh is not that simple lazima unapokwenda kuomba viza ubalozini uwe na documentary proof ya sponsor.....la kama unajidhamini mwenyewe uwe na bank statement yenye ukwasi wa kutosha
Na Ukiwa nayo watakuambia Baki ujenge nchi yako kama entrepreneur
 
Habar Mr&Mrs
Kama ilivyo Ada yakua kila mwenye shida bhas ana hitajika kutatuliwa na aulizae si mjinga haimanishi mdogo either mkubwa na kila mtu Ana ndoto zake binafsi Hakika kiukweli ndoto yangu kwenda Marekani so nahitaj msaada kwa wale wenye uzoefu na nchi ya Marekan.

Nina miaka 20 Education form 4 kuhusu lugha ya kigeni najua kuhusu travel documents it's up to me nahitaj msaada wenu Nahitaj kujua ni sehemu gani itakua nzuri pia na upatikanaji wa kazi ni mzuri iwe ya kutumia nguvu maana kwa Education yangu najua kupata kazi rahisi ni ngumu.


Balance nilio nayo ni kama $1500 kuhusu nauli pia nahitaj msaada kwa anaejua nauli kutoka dar mpka USA itani cost shingapi? $1500 iko nje na nauli pia nahitaj kubahatisha bahati yangu kiukwel maisha ya bongo kutoka ni ngumu ila panapo majaliwa yake Allah unaweza toa sadaka $2000 ukapata zaidi maana bado sijaona biashara gani inaweza kudumu now until the future.

Ahsanten Sana kwa anaejua nauli nahitaj msaada wake na pia mwenye uzoefu na nchi ya Marekan anijuze zaidi na zaidi any comments Ina ruhusiwa
 

Attachments

karibu sana... hapa MIAMI ipo kazi ya kutembeza CHUPI ufukweni..

pia maeneo ya CALIFORNIA...hapa kuna migahawa kibao unaweza ukapata kazi pia katika migahawa ya vyakula vya kiafrika.. sana sana mitaa ya magharibi..


UNA KIPAJI gani kwanza??

alafu swali lingine unamjua TRUMP-ET?
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Back
Top Bottom