Ndugu wana JF na watanzania kw jumla kuna mtu mmoja anayejiita Phinias Aloyce anatafutwa na polisi kwa jalada namba KHM/RB/3445/2013 kutokana na tuhuma za kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu wilayani kahama. Mtu huyo anayejifanya ni mfanyakazi wa kampuni ya Nokia Ltd akiwa na nyaraka zenye jina la kampuni hiyo, hivi karibuni alipita kwenye maofisi mbalimbali zikiwemo shule na kuwaibia watu kwa kuwauzia vizuia mionzi feki. Pia aliandikisha majina na kukusanya fedha nyingi kwa ahadi ya kuwaletea simu kutoka kampuni iliyotajwa lakini mpaka sasa zaidi ya mwezi mmoja umepita hakuna mawasiliano yeyote na simu zake zote amezima. Namba zake za simu ni: 0784 298085/ 0719 434699/ 0766 103008/ 0784 953914/ 0719 434699/ 0715 298085. Mtu huyo ni mwongeaji sana, mnene, mweusi, ana kitambi, ana sura ya duara, umri wake unakisiwa kati ya miaka 45 hadi 55, anaonekana ni mtu wa heshima kupitia mavazi anayovaa. Yeyote anayemfahamu mtu huyo atoe taarifa kwenye kituo chochote cha polisi akitaja RB iliyoandikwa hapo juu ili atiwe mbaroni mapema. Au wasiliana nami kwa namba 0713 758165/ 0755 831576/ 0784 821973.