Tripo9
JF-Expert Member
- Sep 9, 2009
- 4,352
- 3,533
16/ 06/ 2013
tapeli latafutwa na polisi
mwezi mei, 2013 mtu huyo alipitia shule kadhaa hapa kahama na kuwaibia baadhi ya walimu kwa kuwadanganya akidai anatoka kampuni ya nokia ltd na kufanya promosheni ya kuuza simu na vizuia mionzi kwa bei nafuu sana.
aliandikisha majina ya watu na kukusanya fedha kwa ahadi angeleta bidhaa baada ya wiki moja lakini mpaka sasa ameshindwa kutekeleza ahadi aliyotoa.
tapeli huyo ni mwongeaji sana, mnene, mweusi sana, ana kitambi, ana sura ya duara pia anaonekana ni mtu wa heshima kupitia mavazi anayovaa.
tapeli huyo anatafutwa na polisi kwa jalada na: Khm/rb/3445/2013.
yeyote anayemfahamu tapeli huyo atoe taarifa kwenye kituo cha polisi.
wananchi tushirikiane ili kuwanasa matapeli wengi waliopo hapa kahama.
pia unaweza kutoa taarifa za tapeli huyo kupitia namba zifuatazo:
0755 831576 au 0784 821973