vamda
JF-Expert Member
- Aug 1, 2012
- 858
- 533
Ndugu wana JF na watanzania wengine kuna TAPELI mmoja anayejiita Phinias Aloyce huzunguka mikoa na wilaya mbalimbali na kuwaibia watu kwa njia za udanganyifu akijifanya yeye ni mfanyakazi kutoka kampuni ya Nokia Ltd. Hivi karibuni TAPELI hilo lilipita kwenye shule za msingi na sekondari wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga na kuwatapeli walimu wengi kwa kuwauzia vizuia mionzi feki na kudai kampuni ya Nokia Ltd imeamua kuwakopesha walimu mkopo nafuu wa simu za nokia kwa muda wa miezi sita.
TAPELI hilo hutembea na nyaraka zenye jina la kampuni ya Nokia Ltd. Namba zake za mawasiliano ni: 0784 298085/ 0719 434700/ 0766 103008/ 0784 953914/ 0719 434699 na 0715 298085.
Mtu huyo ni mwongeaji sana, mnene, mweusi, ana kitambi, ana sura ya duara pia anaonekana ni mtu mwenye heshima kupitia mavazi anayovaa. Aliowaibia fedha wanapomfuatilia huwatisha kwa kuwaambia endapo wataripoti kwenye vyombo vya usalama fuatilia wataumia.
TAPELI hilo linatafutwa na polisi kwa jalada namba KHM/RB/3445/2013.
Mwenye taarifa kuhusu TAPELI hilo atoe taarifa kwenye kituo chochote cha polisi akitaja namba ya RB iliyotajwa hapo juu. Au apige simu zifuatazo: 0713 758165/ 0755 831576/ 0784 821973. Tushirikiane ili tuyaangamize MATAPELI haya.