Mwenye kujua kuhusu chuo Cha afya Kolandoto

Mwenye kujua kuhusu chuo Cha afya Kolandoto

Kaluluma

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2019
Posts
474
Reaction score
622
Habari za jumapili wakuu,

Kijana wenu naomba kuuliza mwenye kujua chochote kuhusu chuo Cha Afya Kolandoto kwenye upande wa utoaji maarifa.

Maana kijana wangu anataka kwenda, Kusomea diploma ya radiology katika taasisi hiyo,

Je, chuo hicho kina uwezo mzuri katika utoaji wa kozi hiyo?

Japo nasikia wanafunzi wa kozi hiyo ngazi ya diploma wanapewa mkopo na serikali,

Na kama kuna chuo kingine ngazi ya diploma ambacho ni kizuri pia naomba mnitajie hapa ili niweze kufanya mizania kwenye upande wa ada na maswala mengine,

Natanguliza shukrani zangu za dhati.
 
Majibu kama ifuatavyo.

Kwanza hiyo kozi vyuo vingi ndo vimeanzisha mwaka huu hivyo unakosekana ushahidi wa wazi kuhush ubora ila nashauri yafuatayo.

1.Radiology ni kozi inayohitaji mazoezi ya mara kwa mara na ya kina sana ,na vyup vingi vimeanzisha hiyo kozi lakini hawana vifaa vya kujifunzia (Ultrasound,X ray nk) hivyo wanafunzi hawatakua competent maana watasoma tu notes.

2.Vyuo vingi vinategemea mazoezi katika hospital za serikali ambazo nazo vifaa vichache na wanafunzi wengi inapelekea kua na shida katika kujifunza.

3.Kama mtoto ana ufaulu mzuri sana mpeleke Bugando na Muhas hivi ni vyuo vianzilishiwa hiyo kozi na vina miundo mbinu ya maana ya kujifunzia achana na vyuo vya uchochoroni.

4.Kama ukifeli hivyo basi atleast asome vyuo vya serikali vyenye kozi hiyo japo nao ni vimeanzisha kwa mara ya kwanza ila angalau vipo ndani ya hospital hivyo walimu wanao na mafunzo yatakua rahisi.
 
Tulipita huko last yr...jamani ni kubayaa..
 
Back
Top Bottom