Mwenge-Tegeta Road: Poorly designed, poorly constructed! Nani awajibike?

ili ionekane tuna wataalamu wanaojenga barabara za karne hii.
Ili tuonekane tuna wataalam. Tuonekane na nani? Nilidhani tuna tatizo linatuathiri, kumbe ni suala la kuonekana. Ili tuonekane tuna wataalam, kwani tunao?
 
Bagamoyo road nasikia wasimamizi toka TANROADS walikwenda hadi Japan , lakini hiyo michoro yake wala hawakuipitia kuisahihisha.
Matokeo tunayaona, barabara ni substandard wakati wanaitazama tu.
 
acha tu halafu ukisema sana... unaonekana mbaya
 
Inachekesha zaidi kuanzia tangi bovu hadi africana nadhani alama ya uturn imekuwa crossed ikimaanisha hairuhusiwi kufanya uturn, sasa kiuhalisia sijui mtu ukiwa unauhitaji wa kuvuka upande wa pili sehemu sahihi ya kugeuza sijui ni wapi
Hizo alama za kuzuia uturn mtoe tu jmn mana uturn zafanyika kama kawaida popote mtu anapohitaji

Na kuna service road flan hivi wanajenga smwhr around shule across shamo towers kwenda tangi bovu imalizieni basi itumike,asubuhi mara ukute traffic wanakamata watu pale anyway labda coz haijaisha ujenzi, otherwise lengo la service road ni nini,

Mwisho ikitokea mvua kubwa pale masana pale kuja makonde lohh hakufaiiii kwa mafuriko
 
Inaonekana hujui maana ya U-turn...mfano, ukiwa unatokea lugalo ukafika kanisani (mbele ya kwa komba) kuna uwazi unaruhusiwa kuingia barabara ya upande wa pili na kuunganisha barabara inayokupeleka mpaka raibow....(huwezi kuita hiyo ni u-turn)....U turn ni pale unapotokea lugalo afu ukageuza na kurudi mwenge
 
Unachoongea ni kweli kabisa...
 
Uturn kweli ni pale unapogeuza kuelekea mwenge,we umetoa mfano kama unashuka kwenda rainbow, mfano huo huo unatokea lugalo ila unataka kwenda pale NBC tawi la mbezi beach utafanyaje kama sio ku uturn?? Na alama hio ya uturn ndo zimekuwa crossed, Je mtu akageukie wapi
 
Kweli ile barabara ina makosa ya kiufundi mengi sana! Au ndio cha kupewa huna choice? Walipokuwa wana jadili michoro hawakuishauri Japan? Maana sasa imekuwa kero sana!!
 
Kama unataka kwenda NBC, unapaswa kuingia njia ya kwenda rainbow, geuza petrol station ya Puma (zamani Bp) alafu rudi tena barabara ya kuelekea mwenge.
Mmekatazwa kupiga u turn sababu barabara ni ndogo sana...gari ikiwa kubwa kidogo inaweza kushindwa ku negotiate ile kona
 

Kwani nyie hamuelewi kwamba serikali haijali kama mnagongana. Serikali haina motisha yakuwafanya wafanye kazi bora. Wanafanyna ilimradi waonekane wamefanya, ili muendelee kulipa kodi zizizo na maaana ili wao waendeshe mashangingi yao na kuwapeleka watoto wao shule za nje.
 
Yote yaliyosemwa yana ukweli mtupu. Na wahandisi wetu ndio wa kulaumiwa kwa sababu walikuwa wanahudhuria vikao na waliona udhaifu wa upembuzi yakinifu wa barabara hii. Hasa kutokuwa na njia za kuchepukia pamoja na barabara za pembeni (service road). Vilevile ukisema uweke taa za kuongoza magari itakuwa kichekesho kwani ambao hawachepuki watakaa kwenye foleni muda mrefu. Barabara za pembeni zinatakiwa mwanzo mwisho na sio kisehemu kimoja tu! Upana wa hizo service road uongezwe magari yapishane kwa usalama. Makalavati yapanuliwe sehemu zote maji yanapopita juu ya barabara. Taa za barabarani nazo ni muhimu sio kuweka mabomba ya mabango!
 
Nimekuelewa sana ndugu. Na Sio kilometa 3 tu unaweza kwenda hadi kilometa tano na kwako unapaona pale lakini lazima uzunguke ndio uweze kuingia mtaa wako. Sasa wa tz Kila kona mtu anataka aingie apendavyo yeye. Watu wanashindwa kutofautishga high ways na barabara za mitaani. Serikali itilie mkazo watu wakasome udereva na sheria za barabarani
 

U-turn barabara kubwa kama hio sio salama. Inabidi utoke nje ya barabara ndio urudi ulipotoka.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…