Your browser is not able to display this video.
Bibi Khadija anasema wakati akihangaika kusaka haki yake kwenye uwekezaji huo wa ubia, aliunganishwa na mbunge wa zamani wa jimbo la Kijini, mkoa wa Kaskazini Unguja, Yahya Ali Khamis (CCM), akiamini atamsaidia kutatua changamoto hiyo, badala yake aliishia kutapeliwa sh milioni 22.
Akizungumza kwa uchungu huku akitokwa machozi, kikongwe huyo alimwomba Rais Samia kuingilia kati mgogoro wake na mwekezaji huyo pamoja na utapeli anaodai kufanyiwa na mbunge huyo wa zamani.
Anasema umri wake umeenda sana na anakabiliwa na maradhi, lakini anashindwa hata kupata Bima ya afya na hata kununua gari la kumpeleka hospitali wakati kitega uchumi chake kinamnufaisha raia huyo wa Yemen, hivyo anaomba Rais Samia aingilie kati.
"Awamu ya kwanza tulikubaliana ajenge ghorofa saba , mimi nipewe ghorofa tatu na yeye apate ghorofa nne, tulikubalibaliana nipewe fremu tatu za maduka na chumba cha stoo, nilipwe sh 300, 000 za kujikimu kila mwezi, lakini nimeambulia kupewa ghorofa moja tu tena ya juu hata lifti haina, makubaliano mengine yote hakuna".
Kuhusu mbunge huyo wa zamani wa Kijini, anasema alijigamba kuwa anaweza kumsaidia kupata haki yake, lakini aliishia kutapeliwa sh milioni 22, hivyo anataka fedha zake zirejeshwe mara moja.
Alisisitiza kumlilia Rais Samia angilie kati kwani ni mtetezi wa wanyonge wanaonewa kama yeye na anajua hana muda mrefu wa kuishi duniani, hivyo anataka kuacha urithi kwa watoto wake.
Mbunge huyo wa zamani alipoulizwa alikiri kupokea kiasi hicho cha fedha lakini alidai zilitumika kwa kazi ya kufuatilia haki za Bibi Khadija na kazi hiyo bado inaendelea ikiwemo kutaka kufungua kesi.
Mwekezaji kwa upande wake, amesema hataki kufuatiliwa na hana muda wa kuzungumzia malalammiko ya Khadija huku akitoa maneno ya kejeli na dharau.
CHANZO: RAIA MWEMA